Skip to main content

Baba zetu nao...

Wiki Mpya oyee!

Nimeacha kujivunia Tanzania kama Taifa(Kisiasa) miaka kadhaa iliyopita, najivunia Tanzania kama Nchi na baadhi ya Tamaduni zake, kama vile kuvaa Vibwaya (vile vifupi, kuachia tumbo na kufunika Matiti), Ngoma na nyingine nzuri nzuri.




Kuna unataratibu wa baadhi ya wanaume kudai kuwa mwanamke yeyote atakaelala nae ni Mama yako na mtoto yeyote atakaezaliwa na mwanamke ambae sio Mama yako ni Ndugu yako. Sina uhakika kama ni Utamaduni,Tabia au pure______!




Mama yako ni yule aliekuzaa au "kisasa" aliekulea tangu ukiwa na umri wa masaa au siku chache.....sio random women aliolala nao Baba yako.



Pia ndugu yako ni yule mliotoka tumbo Moja, wengine ni Jamaa (tena ukiamua kuendeleza ujamaa huo kwani sio lazima).




Tabia ya Baba kulazimisha watoto wao kuwaita wanawake wengine Mama au watoto waliozaliwa huko (kabla au baada ya Ndoa) wadogo/kubwa zao sio haki na sio sahihi kwa mtoto/watoto husika.



Huyo ni Mkeo na hao ni watoto wako wewe na huyo Mkeo na hao watoto ndio ndugu,




Ku-share Baba haina maana ninyi ni ndugu wa Damu kwani asilimia kubwa ya Damu yako/yake ni kutoka upande wa Mama sio baba......(In my head).




Kwani Mbegu za Mwanaume huwa na Damu? Lile yai la mwanamke ni Damu na jinsi Mimba inavyokuwa Mama na Mtoto wana-share Damu.....sasa Damu ya Baba (in my head) haina uzito linapokuja suala la "undugu wa Damu" kutoka upande wa Baba bali Mama si eti?.




Nukta hapa ni kwamba, Baba wa Kibongo acheni ku-bully watoto wenu na kulazimisha undugu au "ufamilia"....ili kufurahisha Ego zenu(nina wake/watoto wengi).



" Mimi Yakhe? Ninao kumi na Tano na mwingine anakuja hivi karibuni hehehehe familia kubwa sana hii Yakhe, mama zao wapo 7"....hapo hata Tofali la choo huna.



Usichukue au kutumia maelezo haya kama kielelezo cha Kitaalamu mie sio Mjuzi, nimesema tu kilichonijia kumkichwa.


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao