Skip to main content

Posts

Wanyumbani na Wanje....

Heri ya Wiki Mpya! Siku hizi wa Nyumbani na wa Nje zimekuwa "jamii" mbili tofauti wakati zamani tulikuwa kitu kimoja ailimradi tu sote tunatoka Nchi mmoja iitwayo Tanzania. Kuna kama kaushindani au kaubaguzi ka chini kwa chini hivi....well, nilishakuambia kuja Nje siku hizi sio deal labda ndio maana wa nje tunadharauliwa hihihihihi. Alafu tunajifanya tunajua sana utatuzi wa matatizo yanayojiri nyumbani wakati wengine hatujagusa huko mwaka wa Tano huu....kazi kufananisha tu "Kwa mfano huku blablabla" sort of people. Pia kuna wale ambao wapo Nyumbani kazi yao kulinganisha pia....wale akina "when I was in London" kind of people...."Hata wenzetu wa Ulaya blablabla" wakati hujawahi kuishi huko au ulikaa si zaidi ya tumiaka 3. Wote hamna tofauti linapokuja suala la kujifanya mnajua utatuzi wa matatizo yanayojiri Tanzania (hasa kijamii, kisiasa na kiuchumi). Sie wenye watoto wadogo haturudi moja kwa moja

Hoarders....

Hello! Mambo! Wadogo zangu wa Kike enzi zile walikuwa wakiniita....wacha ni seme tu bana....najulikana kwetu kama "mchafu" sio kwamba siogi, sishafishi nyumba au kutandika kitanda la hasha! Nilikuwa nafanya hayo yote in my own time....sio ukiamka tu unakimbilia kuosha vyombo(which I hate) au kupiga deki na kupangusa vumbi incase wageni watakuja.... So nilikuwa na-swap kazi hizo na yeyote mwenye zamu ya Kufua au kunyoosha....nazipenda kwavile zinafanywa baadae....pia napenda kusafisha choo/bafu (huwa nasafisha usiku)....hihihihi. Asa siku moja mume wa mimi na mimi tulikuwa tunaangalia kipindi kuhusu Hoarders....hee, mkibaba akaniambia wee mwenyewe ni "hoarder" aiiii niliumiaaaa mpaka nikakaribia kulia! Wacha nianze kubisha(vere mbishi nikiwa na uhakika, tabisha mpaka kesho yake) na kuthibitisha maana ya Hoarders....nikisisitiza kuwa ni Ugonjwa wa Akili. Kesho yake nikaenda "store" nikakutana na Masanduku na M

Lete Ushahidi wa unachoongelea...

Hello DHB/DHW member....year 2003 lazima umezaaka hihihihi maana mie tu niliekua katoto mekuwa kibibi(no, not princess, ni kibibi as in Mzee).....drop me a line please!! Enzi hizo bana, kulikuwa na malimbukeni wa Elimu ya juu kibawoo au niseme Wasongo....ukisema kitu online lazima wakuambie uwape/utoe vielelezo au statistics. Yaani walitufanya sie wa Elimu ya Chini going on to Elimu ya Juu(enzi hizo) tujione "hamna kitu" kabisa, tulinyimwa haki ya Msingi ya kusema tulichojisikia au tulichotaka au kukijua . Ukiongelea kitu bila kuwapa "ushahidi" wanakuambia unaongelea mambo ambayo "unadhani" unayajua, lazima mtu uwe na ushahidi wa kuthibitika kuwa unachozungumzia "umesomea" au unakisoma. Siku hizi aiii unapewa kielelezo cha picha inayotembea na sauti kabisa tena bila kuomba....shukurani kwa Teknolojia na urahisi wa ku-share yale tutakayo/ujisikiayo. Kwaheri kwa sasa. Mapendo tele kwako...

Celebs

Hii jamii ina power ya ku-normalize kila kitu, hata vile ambavyo ni normal lakini jamii nyingine hawavifanyi, wao hu-normalize. Mfano ni "attachment parenting" ambapo mama analala na mtoto wake na kumnyonyesha for as long as possible. Hiyo "attachment parenting" si ni kitu cha kawaida kwenye jamii ya Kitanzania(na Afrika kwa ujulma)....nimezaa mwanangu wa kwanza nikapigwa marufuku kulala nae ili kuepusha cot death. Nikakumbuka Mama alipozaa wadogo zangu 3 wa mwisho, wote alikuwa analala nao kitanda kimoja na hakuna aliepoteza maisha.... Aii....nikawa na lala na mwanangu ka' ifuatavyo na amenyonya mpaka mwaka na miezi 3. Siku hizi analala chumbani kwake lakini akiota ndoto mbaya anakimbilia kwetu so tunalala wote wanne. Huyu wa pili bado analala na sisi na bado ananyonya (mwaka na miezi 3) tena huyu ni king'ang'anizi kuliko kaka yake ambae hakujali kulala peke yake au kulala na sisi.. Kingine ni Kuzaa kwa kupasu