Skip to main content

Posts

Nafurahia kuwa Mama...

Lazima umeisikia hii kwa Wanawake wengi wa kileo....Mimi sifurahii kuwa Mama (way too hard) ila najivunia kuwa Mama kwa wanangu. Kuna wale wanawake ambao wakikua tu wanatamani kuwa Mama (kuzaa) yaani kuwa mama ni muhimu kwenye "list" ya mambo wayatakayo Maishani. Mimi sikuwa hivyo, yaani kuzaa haikuwemo kabisa akilini mwangu....nilijua siku moja nitazaa, lakini sikuwa na haraka au niseme urge/desire ya kuwa na Mtoto. Hata nilipojifungua Wanagu sikupata ile hisia wanazopata wanawake wote(wengi waogo hehehehe) "falling in love like never before" au "falling in love all over again"....nilijipa "hi5" in my head nikafurahi na kuwa-proud huku nikujiuliza "kapitapitaje pale"? Haina maana siwapendi Wanangu la hasha! Nawapenda sana na siwezi kuishi bila uwepo wao....hata kwa masaa machache yaani SIWEZI. Ila Mapenzi kwa wanangu hayakuhitaji mimi ku-fall in love na Mapenzi kwa Mtu baki ndio huitaji

Rafiki wa kweli...

Haitaji kuku-support kwenye kila jambo hata kama ni baya! Kama ukikosea atakuambia ukweli hata kama unauma....akiku-support kwenye kila kitu ujue ni MNAFIKI. Ndio maana Mimi sina Rafiki bali nafahamiana na watu....oh wait! Actually ninarafiki Mfamasia nilikuwa nae Chuo in olden days....labda kwavile ni Mghana so tofauti ya Kacha imefanya Urafiki Udumu. Sijui wenzangu mlilelewa vipi lakini kukosolewa ni muhimu kama kusifiwa. Ilikuwa unakosolewa kwa kinachokosoleka (ujinga/upuuzi ulioufanya) mbele ya wenzio so that usirudie tena upuuzi wako. Usiogope kuitwa "double standard" akienda ovyo mpe cheupe ajirekebishe. Babai... Mapendo tele kwako...

Kujiremba....

Kipajiiii....heri ya Alhamisi! Nilipokuwa Msichana 10-17 sikuwa najali mambo ya kujiremba....Mama hakuturuhusu kupaka Rangi ya Kucha Ijumaa kisha tuondoe J'pili jioni. Eti tulikuwa tunaharibu Rangi zake... Basi tukawa tunapaka Wino mwekundu(Pen nyekundu) au ukitaka Rangi "clear" au kucha zing'ae basi unachukua Marumaru au Vipande vya China (sahani, vikombe n.k vilivyovunjika) unasugua kwenye Sakafu ya Sementi kisha ile vumbi yake unaisugua kuchani. Nilipofikia Miaka 18 nikaanza kupaka Wanja na Lip gloss. Nimeanza kujipangusa Poda usoni, kutinda Nyusi na kupaka Mascara nilipokuwa na miaka 28....anyways! Baada ya kuwa addicted na Beauty Vlogger nikaamua kujitutumua kwenye kujiremba bana....basi siku ambayo najua sitoki nje mwenyewe napanga nitakavyo vyaa the next day na Vipodozi gani vya kujipaka....(Ninavyo kibao kwani kila Birthday napewa zawadi ya Vipodozi....watu wachokozi)! Naamka mapema, nafanya shughuli zangu za ndan