Imepotelea wapi? Au ndio kwenda na Wakati?
Juzi kati nimekutana na Picha ya Maiti ya Mpendwa wangu....pamoja na familia kufanya kazi ya ziada kuzuia upigaji Picha wa shughuli nzima ya Mazishi achilia mbali Mwili wa Marehemu wa mpendwa wetu zaidi ya alieajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo....bado kuna jitu likapiga picha na ku-share online.
Kwasababu hana Uhai tena haina maana kapoteza Haki zake kama Mwanadamu mpaka atakapozikwa(Fukiwa).
Maiti ingeweza ingejisitiri na kupozi ili apendeza au kutokea vizuri zaidi....pia angechagua ni Picha gani itumike kutangaza Tukio lilipolekea Mauti kumfika.
Unapata faida gani ku-publish au ku-share picha ya Maiti?.....kwanini unataka tumkumbuke Marehemu kama Maiti na sio alivyokuwa Hai na mwenye furaha?!!
Unaweza kusema naegemea kwa Waingislishi kwa vile naishi huku na wao hawana utaratibu wa kuonyesha Maiti au kuiaga zaidi ya Jeneza na Picha ya Marehemu alipokuwa hai....nia ni kubaki na kumbukumbu ya yeye