Skip to main content

Posts

Mama yangu alikuwa Kimada!

Uishie hapo hapo!! Najua umekuja mbio hasa kama wewe ni Kimada aka Mwizi au mtoto wa Kimada. Mama yangu alikua Mke wa haki na sote tumezaliwa Ndoani.....alikuwa* kwasababu Baba ni Marehemu, huko Ahera sijui kaoa tena? Roho itaniuma sana nikijua kaoa tena. Anyway. Kuna wale watoto wa Vimada ambao huja na mijisababu kibao ili kutetea Mama zao Vimada au Baba zao Malaya....wengine wanakuja na "Wake wanajibana wakati Vimada wanajiachia miili yao"....wengine wanajifanya wamefanya "Utafiti" na kugundua kuwa Vimada wanajua Mapenzi kuliko wake n.k. Hakuna ku-justfy hapa, kama wewe ni mtoto wa Kimada utabaki kuwa hivyo!! Tena ngoja nikolezee Mama yako ni kamwizi na baba yako ni kamalaya....tuliache hilo kwanza. Hivi unajisikiaje kwa mfano Umeolewa/Umeoa mtoto wa Kimada, yaani Mama mkwe wako ni "mwizi" wa mume wa mtu na huyo Mume(Baba mkwe) ni Malaya.....hihihihihi mie nisingekuwa comfortable yaani ningekuwa nawakwepa m

Kupotea Suna!

Mara ya kwanza kumiliki "SmartPhone" ndio ikawa mwisho wa Mimi kupotea(in my head)....leo 2014 na Tech yote ya Ramani na Gadgets zote zilizopo za "Directions" bado napotea.....Hapo ndio Suna inakuja sasa(sina sababu nyingine). Kwa kawaida nikipotea huwa sioni aibu kumuuliza mtu au kuomba anielekeze....tofauti yangu na wewe ni hivi; huwa sisimamisha mtu yeyote tu, nategea wale ambao sio attractive (at least machoni mwangu). Kwanini nachagua unattractive watu(Wake kwa Waume)? Hata sijui....ila nahisi kama wao ndio wanatoa maelezo vizuri kuliko wale "attractive"....wanakuelekeza utadhani unawatongoza(mie mwanamke, mke na mama nikutongozee nini wee fala...). Naweza nikaenda mwendo mrefu kutoka sehemu niliyopotea mpaka nikutane na unattractive person ndio nimuombe "directions". Nishakuwa stereotyped sana, hivyo wala siogopi kustiriotaipu watu.....ndio maisha...heri umejua kuliko ningekudanganya. Si eti?

Macho yane...

Jana si nilikuambia "nalikizoka" sehemu- sehemu ya Ulaya?....nkaenda kwenye Shopping Centre yao kubwa na wanangu wawili! (Siku zote huwa napita kwa nje tu). Simlituambia wa Ulaya hatuwezi "kulikizoka" Tanzania, sababu tukija huko sio Likizo tena bali tumerudi nyumbani, ni ukweli kabisa (sijui hili limekujaje hapa, tuliache)! Basi humo ndani (shopping centre) Macho yangu yamesifiwa na watu kibawoooo....hee! Mwanamke nikashanga....(Najua nina tumajicho tuzuri ila sio kiviiiiile)! Mkaka mmoja akashindwa kujizua akaniuliza "where are you from"? Nkamwambia "England" hihihihiihi nkaona NOMA! nkasema Tanzania, East Afrika, I have 2 kids and a husband....akasema "are all grown women look like you?....Fit, Nice skin and beautiful eyes?" Nkasema Yes! (Nimeitangaza Tanzania hapo) England hawayaonagi Macho yangu au dharau tu washenzi kabisa wale, mmmh! Ila inawezekana ni u-busy wa Maisha. Watu hawana habari, akili yote ina-focus kwenye £ ili kulipa

Siri...

Unawajua wale akina "nilificha/nilifanya SIRI kwasababu nilikuwa nalinda hisia zako"....."Kwasababu sikutaka kukuumiza" mifano ya watu the shenzi kind of people? Halafu sasa umejua! maumivu ni zaidi kuliko ungejua siku aliyoifanya hiyo siri....well in my case, reaction yangu ni ileile ufiche siri kwa miaka 10 au uniambie masaa machache yaliyopita....AM GONE!! Siri uliyofichwa kwa Miezi/Miaka huuma zaidi kuliko kuambiwa moja kwa moja! The thing is kuendelea kuishi na mtu huyo ni sawa na kuishi maisha ya "Uongo". Usikute hapa nafichwa mambo kibao alafu kimbelembele na-blog hihihihihi, siku nikijua hata kama nimefikisha miaka 50, sisamehi aisee...hii ni karne ya 21 sio Enzi za Yesu!! Aah. Kuna mambo ya kifamilia hupaswi kumueleza mwenza wako unless unajua kabisa yatamu-affect yeye na watoto. Vinginevyo yaache huko huko "familiani". Sasa hizo sio Siri ninazozungumzia hapa, maana hazikuhusu! Si