Skip to main content

Posts

Make up artists....

Ukiingia kwenye Department stores au Boots (Duka la Dawa na Vipodozi) kubwa kwa sie wa Ulaya hii hapa....unakutana na MUA kwenye "viOSK" vyao wenyewe wamejiremba wamependeza....er kwa mbali! Asa sinilikuambia tangu nigonge miaka 30....sasa ni 30na nimeanza "kuipenda" ngozi yangu ya usoni! "Mambo ya mwanamke reception".....sasa kama mtu hukujaaliwa "reception" nzuri au kurembeka(mimi) basi angalau Ngozi iwe nzuri na yenye afya kuwapotezea watu "focus". Mwanamke nimejaribu bidhaa kibawoo za kufanya Uso wangu uwe laini na wenye rangi moja....maana...mmh! Sijawahi kutumia Mkorogo (na sina mpango huo), sina tatizo na Chunusi (mpaka nile Chocolate), yaani ngozi yangu inakaribia ukawaida tu japo inatoa mafuta ya kutosha kukaangia Vitumbua....anyway! Nimejaribu skin care nilizokuwa nikitumia miaka ya nyuma in my late 20s, sasa zinadunda, kitu cha uso ama kimekomaa au kimekuwa Sungu (Kisayansi ngozi hupoteza n

Kabla hujafa, hujaumbika!

Ni kawaida ya watu (wengi) kucheka matatizo ya wenzao au kuyazungumzia katika mtindo wa "kichekesho". Mimi napenda sana kucheka na kuchekesha (japo kuwa sichekeshi....yaani nikitoa kichekesho watu hawacheki mpaka nielezee kwanini nilichosema kinachekesha)....hihihihi achana na hili! Matatizo nayogusia hapa ni yale ambayo mtu hana uwezo wa kuyazuia, sio matatizo ya kujitakia(kuchagua) kama vile Utumiaji wa Madawa (japokuwa hata hawa mie huwa siwacheki). Kama huna utu na huna mpango wa kumsaidia mwenye matatizo kwanini uzungumzie matatizo yake kwa watu wengine katika hali ya "kumcheka"? Wengine wanapoleta habari za mtu za kusikitisha kutokana na matatizo yake yaliyobadilisha Mwili au Akili (Ulemavu) yake hawacheki kwa kukenua Meno, lakini jinsi wanavyoelezea unagundua kabisa wanamcheka mhusika. Mf; "Eh bwana unamkumbuka Elia? Daah jamaa yaani kaisha halafu sasa anatembelea Mgongo. Yule jamaa alikuwa anajifanya mjanja sana"....umeona? Hakenui meno laki

Kuvaa Wig!

Nimekugaya eti?!! Well kwani tulisaini mkataba wa mimi kuwepo hapa kila siku? Hihihihi usiache kusoma bana, hebu baki hapa upate stori ya Wig. Ujue kuna siku akili inachoka alafu kunakuwa kama "empty" hivi kichwani kwa ndani, yaani hata yasiyo na maana nayo huondoka basi inakuwa ngumu kidogo kuandika ili ueleweke. Ikifikia mahali unaandika (huku unasoma bila shaka) lakini unahisi hakileti maana....basi tambua kuwa unahitaji Mapumziko kiakili! Anyway.... Wanangu na Baba yao wamelala....Joto limewachosha, maana leo ka' tupo Kisarawe.....achana na hilo. Nimekaa hapa nikakumbuka Wig langu la kujinyonga wenyewe mnaita Curl sijui Karikiti. Kwa kawaida mie sio mvaaji wa hayo mavitu, ila baada ya "issue" ya nywele nkasema ngoja nami niwekeze kwenye "Afro Wig". Siku (2.5yrs ago) nkalivaa, baada ya kutoka Kazini nkaenda Chekechea kumchukua Babuu ....hee! Mtoto wacha alie alafu anaangalia juu (lilipo Wig) hehehehe....nikazuga bana mbele ya Wazungu as walijua nim