Nakupenda kwa kuichagua Blog hii...
Unajua wale wadada wakubwa inatokea unawapenda, unatamani kuwa kama wao (Kielimu) utakapokuwa Mkubwa?!!
Mie nilikuwa nawapenda sana Wadada Wanasheria, Waandishi wa Habari na Young Docs (au tuliwaita Medical assistants sababu walikuwa hawajafuzu).....sasa kuna mmoja alikuwa jirani yetu enzi hizo bado kabinti, alikuwa anasoma Russia.
Kwasababu alikuwa Mkubwa sana kwangu hatukuwa na utaratibu wa kuongea lakini tulikuwa karibu sana na alionyesha kunipenda kweli-kweli!
Kila J'Mosi alikuwa ananiita "Dinah Mdogo wangu unakazi?(Za shule)... ukimaliza naomba uje unikwangue Mba"!! Usicheke tafadhali (hihihihihihihahahahahaha)...Basi mwenyewe nafurahi naenda kumkwangua "dada MA" Mba....honestly!!!
Namkwangua, nikimaliza nampaka mafuta halafu namsuka....heee! Najua kusuka blaa tangu nina miaka 7 shukurani kwa Bibi na MSesere(Doll) wangu....nika-master Kusuka Mitindo nilipofika miaka 1