Skip to main content

Posts

Watoto wanahitaji role Model sio Model!

Ah! Nimekua busy kweli....unajua umri ukienda Majukumu yanazidi/yanaibuka kila kukicha. Hapana sio majukumu kuhusu Watoto, Baba yao na Bills ni majukumu ya kuutunza Mwili na Uso ili kurudisha Miaka nyuma. Si nilikuambia by the time nafikisha Miaka 40 nataka kuwa kama Gabriel Union!! (Au niliota tu?). Nataka wanangu wawe proud of my "look" nikienda wadondosha na kuwachukua Shule hihihihi....sio wakikuona tu wanakimbia kwa aibu au wanasema "that's not my mummy, she's my Shangazi/Bibi". Eh! Nilipokuwa Msingi kuna mdada mmoja (sasa maarufu kwenye MaTv huko kwenu) alimkimbia Mama yake, tena akawa analia kabisa kuwa yule sio Mama yake....si wajua Mama wa Kinyakyusa alietoka Mbeya beak ya kwanza Shuleni hihihi hi akina Mwakaninini(naambiwa ninyi ni watani wangu upande wa Mama so usi-panic)! Eti "Children need role model Not a Model"....wacha uvivu, hebu jipende huko.....you can be both! By the path I AM FAR

Mwanaume ka' Mwanamke na Nyumba Ndogo!

Only Mwanaume husika akifanya jambo baya, la kizembe au akionyesha "emotions"! Mfano akisema ukweli pasipotakiwa (Umbea), akilia baada ya kuumia, akizimia Msibani (Wanaume hawazimii, huwa wenda wazimu hihihihihi) n.k. Tabia hiyo huwafanya Watoto wa Kiume kuwa na Tabia mbaya za Baba zao, kwasababu wanaogopa au hawataki kufananishwa na Wanawake. Kwenye Jamii yetu (Tz) Baba kuwa na Kimada siku hizi imekuwa suala la kawaida, jamii imelikubali hilo na kuwapa jina zuri eti "Nyumba Ndogo" which is sooooooo annoying, Yaani ndio kukata tamaa au?!! Sasa nyumba ndogo huwa haijengwi kwa siku moja, na mara zote Mtoto wa Kiume huwa wa kwanza kujua ikiwa Baba ana Kimada.....Vijana hujua mengi sana Mtaani/Vijiweni. Wengi huwa wanaumia kuona kuwa Mama zao wanakuwa cheated na Baba zao lakini kwa vile wanaogopa kuitwa "Wanawake" wanaamua Kuuchubua (do you still use this word??). Baadhi ya Vijana (watoto wa kiume) husi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mungu ni wa Afrika tu?

Umewahi kujiuliza kwanini sisi Waafrika Mataifa Mengine ambayo ni Masikini kuwa pamoja na kuamini Mungu na kusali kwetu kote bado hakuna Maendeleo? Kwanini Mataifa hayo yanaendelea kuwa Tegemezi wa Nchi za Ulaya Magharibi na Marekani?(Wacha sababu za Kisiasa na Historia hapa sio mahali pake).... Leo hapa (kwako itakuwa Jana) Mimi na Asali wa Moyo tulikuwa tunajadili kuhusu Ubinafsi wa sisi wanadamu, tukafikia mahali tukakubaliana (kwa kawaida huwa hatukubaliani)! Wazungu ni Washenzi kote-kote na wengi wao hawaamini Mungu as in kusali kucha kutwa na kwenda kutoa Sadaka kanisani kila J'2 lakini linapokuja suala la kusaidia Binadamu wengine wenye Matatizo huwa mstari wa Mbele! Huenda hilo ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa, kwamba hawakai(kupoteza muda) kusali na kutegemea Mungu awashushie Mahela ili wawasaidie wengine au kukesha na kuomba ili Mungu awape Makazi wakimbizi mahali palipo na Vita. Wanafanya yote hayo kwa Vitendo.... kuna Maduka kibao ya Misaada ambapo watu hujitole