Skip to main content

Posts

Inapendeza sana na unapata hisia maalum za kipekee unapokutana na "High End" new publication wanazugumzia kitu ambacho wewe(Mimi) "nisiejulikana End" nimekizungumzia Mawiki na Mawiki yaliyopita! Unakumbuka Feminisim?hiyo ilikuwa Wiki iliyopita so achana nayo!....unakumbuka "kujilinganisha/fananisha"?.....aaah Dinah naona mbali sana ujue, nafaa kuwa Rais wa KissWay?!!! (*nimeacha kuchapa nacheka kwanza*). Pengine bila kujua unachapisha maelezo ya siku yako ilivyokuwa "njema" au unaweka picha au unaweza tu ku-share ulichonunua wiki hii kwa ajili ya wanao au mwenyewe n.k.....ni sehemu ya maisha yako hivyo unadhani ni poa tu uki-share na watu wanaofuatilia "kurasa" yako popote ulipo kwenye Social Media. Kuna mahali unafikia unakuwa karibu sana na watu hao ambao huwajui(mnakuwa connected), sometimes mna-miss-iana.....Jinsia tofauti hapa lazma "lust" au hata "love" hujitokeza....duh! Niliku

Zawadi kutoka kwa Mwenza!

Kwa siee wa Ulayani huwa tunapenda sana zawadi kutoka Nyumbani, zawadi (Radha ya Nyumbani) kama vile Ubuyu, Mahindi Mabichi*, Matembele ya Kukausha, Dagaa wa Kigoma, Viuongo vizima vya Pilau, Maembe Dodo au Embe Tanga bila kusahau Embe Ngong'a(unazijua?!!), Maharage ya Mbeya au yale ya Njano, Njugu Mawe n.k. Mimi binafsi huwa napata hizo mavitu moja kwa moja kutoka kwa Mama, lakini kwa wale wenye Wenza wanaopenda kwenda Bongo Mara kwa Mara huwa wanavipata moja kwa moja kutoka kwa Wenza wao. Tatizo ni kuwa Mwenza anapokuletea zawadi wakati mwingine inakuwa imetoka kwa Mme/Mke mwenzio bila wewe kujua. Inasemekana wenzetu walioungana na "rangi" tofauti huwa wana-miss sana "rangi" yao hivyo wanaporudi Nyumbani huwa rahisi kupata wanawake/wanaume ambao huwapatia kile wanachokikosa kutoka kwa wenza wao Weupe....Maisha yaha....namaanisha Haya!!! Halafu kuna wale ambao wanapenda tu kulala hovyo(Malaya)....Ujue! Ili uendelee k

Kuaga au kutokuaga Marehemu!

Hiyaaaa! Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu. Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo! Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo! Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti? Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja! Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona"