Skip to main content

Posts

Stop....Africa is NOT a Country.

Mtukome...... Wamarekani ndio zao....sijui hawakuwa na waalimu wa Jiografia. Wakija UK wanasema wanakuja EU.....wakienda Tanzania wanasema wapo Afrika. Mbona Canada hamuirifai kama America au Marekani ya Kaskazini? Humkuti mtu kutoka Bara la Ulaya anarifaa Nchi yake kama Ulaya....atakuambia moja kwa moja yeye anatoka wapi. Afrika ni Bara sio Nchi. Halafu waafrika wenyewe ndio mamwehu kabisa yanaona raha au sijui sifa au aibu ku reffer Nchi zao walikotoka na kuishia kusema Afrika....."back home in Africa nlanlanlaaaa". Sema Nchi yako kama hawaijui waambie wakaGUGE......acheni kutufanya as if Waafrika wote tupo sawa. Nchi yeyote iliyotawaliwa na Muingereza inafuata mambo fulani ya Kiingereza.....kuna Tamaduni tume-adopt na kufanya zetu....mfano Ukristo, uvaaji wa nguo na baadhi ya Uendeshaji wa shughuli za Kimahakama bila kusahau sheria. Hii ndio faida pekee ya Jumuiya ya Madola(in my head). Halikadhalika waliotawaliwa na Mreno....Mwarabu....Mjerumani au Mfaransa

Kwanini___haonyeshi mtoto wake?

Hujawahi kujiuliza kwanini huyu fulani anapenda kuzungumzia mwanae lakini hajawahi kuweka picha ili na mimi angalau nipate picha ya alivyo kila anapomzungumzia. Well shauri yako ila najua mie nimeisha jiuliza to the point napata hasira(hihihihi sio hasira bali whys lundo). Kuna dada mmoja (enzi zile bado nipo kwenye social media) alikuwa ana-share mengi wakati wa Mimba....alimalizia na baby shower na habari ya mtoto kuzaliwa halafu ndio ukawa mwisho.....akawa anamzungumzia tu na kushare zawadi alizompatia kwenye Siku ya kuzaliwa n.k....mapaka leo sijui sura wala rangi ya mwanae......sio muhimu kihivyo lakini muhimu. So kama mimi enzi nilikuwa nahisi hivyo hakika hata wewe ungependa kuona sura za wananhu si eti eeeh. Nili-share picha kiasi nilipokuwa kwenye Sosho media so walionifuata wengi wanakumbukumbu kwa mbali ya wanangu walivyo japo sasa wamekua mmno. Kuna sababu nyingi zinazofanya watu kuzuia picha za watoto wao kuzagaa mitandaoni hasa kama wazazi ni maCeleb..... .....maana

Kuzaa(naturally) ni kupoteza dignity....

Heroooo! Tangu umezaa kiasili hujahisi hali ya kujiamini zaidi kuonyesha mapaja yako(kama nguo fupi sio zako)? Au huoni big deal kuvaa vyovyote.....unaeza kwenda Sokoni na huku gagilo ljnachungulia au mkanda wa sidiria umeshuka.....pengine na night dress kabisaaaa. Wengi husema mwanamke akizaa anapoteza hali ya kujipenda na kujijali......mie nasema sio kwamba hatujipendi na kujijali isipokuwa tumeacha DIGNITY hospitali baada ya kujichanua na kupiga makelele mbele ya watu baki ili mtoto atoke. Halafu ukizaa nothing seem to matter but your child au children. Unapoteza ile jali ya "mimi"......maisha yako yanakuwa yamefunikwa na watu wengine ambao wanakutegemea wewe ufikirie na kufanya maamuzi kwa ajili yao. Miezi michache ya mwanzo hali huwa mbaya sana lakini hujui wakati huo mpaka uvuke miezi 6 au mwaka hivi baada ya kujifungua hasa mtoto wa kwanza.....kwa uzoefu wangu. Baada ya mpoto unaanza kurudi kama ulivyokuwa japokuwa dignity hairudi......Binafsi napenda kuvaa n

Nakaribia kuwa 40yrs old...

Habari ya leo, Nimeamka naumwa kichwa. Mara mtu abisha mlangoni. Nafungua mlango huku mnyororo umeshikilia kwa usalama wangu.....Mbabu ananiambia yupo na Mbunge na wangependa kuongea nami. Nkasema naumwa kuchwa so sitaki kuongea. Akanambia Uchaguzi utakuwa May 7 je nimepanga kuchagua Chama gani?.....nkamwambia(sisemi hapa kwasababu)......Mbunge akaja mlangoji na kuniambia ahsante kwa support. So alijificha akidhani nina-suport Chama kingine.........back to 40yrs ols me. Fashion bloggers na Vloggers wa miaka 35-40 mpo wapi kwani? Au wote bado ni 28 au 32....unakuwa na miaka hiyo kwa miaka 7 hihihihihi. Sitaki mtu wa 20s au over 40s aniambie natakiwa kuvaaje. Nataka mwenye umri husika au anaekaribia sio nyuma miaka 10 au mbele miaka 10. Unavutiwa na fashion blogger au vlogger  halafu anakuja kukwambia anamiaka 27 how annoying? Vaa umri wako kashenzi wacha kuvaa kama mkimama wa 40s. Sio nakaribia 40 kihiiiiivyo ila sio mbaya kujiandaa si eti. Mambo ya kuanza kujipakaza maanti makunyanzi