Monday, 23 February 2015

Kuzaa(naturally) ni kupoteza dignity....

Heroooo!

Tangu umezaa kiasili hujahisi hali ya kujiamini zaidi kuonyesha mapaja yako(kama nguo fupi sio zako)? Au huoni big deal kuvaa vyovyote.....unaeza kwenda Sokoni na huku gagilo ljnachungulia au mkanda wa sidiria umeshuka.....pengine na night dress kabisaaaa.


Wengi husema mwanamke akizaa anapoteza hali ya kujipenda na kujijali......mie nasema sio kwamba hatujipendi na kujijali isipokuwa tumeacha DIGNITY hospitali baada ya kujichanua na kupiga makelele mbele ya watu baki ili mtoto atoke.


Halafu ukizaa nothing seem to matter but your child au children. Unapoteza ile jali ya "mimi"......maisha yako yanakuwa yamefunikwa na watu wengine ambao wanakutegemea wewe ufikirie na kufanya maamuzi kwa ajili yao.


Miezi michache ya mwanzo hali huwa mbaya sana lakini hujui wakati huo mpaka uvuke miezi 6 au mwaka hivi baada ya kujifungua hasa mtoto wa kwanza.....kwa uzoefu wangu.


Baada ya mpoto unaanza kurudi kama ulivyokuwa japokuwa dignity hairudi......Binafsi napenda kuvaa nguo fupi. Sina gauni au sketi ndefu inayovuka magotini.....ni ama gotini au juu yake au chini mpaka mwisho(well maxi).Sasa siku Asali wa Moyo akanambia eti "Dinah wewe ni mama sasa inabidi uvae kama mama" nika hihihihihihihi halafu nikamwambia nimeshapiteza dignity wakati wa kuzaa wala sijali watu watanijajije kutokana na vijigauni vyangu.

Tunaishi kwa ajili yetu na sio kuridhisha watu wengine. Watu hawaridhiki.....utaishi wewe kama wewe lini eti.

Nikuache sasa.

No comments: