Skip to main content

Nakaribia kuwa 40yrs old...

Habari ya leo,

Nimeamka naumwa kichwa. Mara mtu abisha mlangoni. Nafungua mlango huku mnyororo umeshikilia kwa usalama wangu.....Mbabu ananiambia yupo na Mbunge na wangependa kuongea nami. Nkasema naumwa kuchwa so sitaki kuongea.


Akanambia Uchaguzi utakuwa May 7 je nimepanga kuchagua Chama gani?.....nkamwambia(sisemi hapa kwasababu)......Mbunge akaja mlangoji na kuniambia ahsante kwa support. So alijificha akidhani nina-suport Chama kingine.........back to 40yrs ols me.



Fashion bloggers na Vloggers wa miaka 35-40 mpo wapi kwani? Au wote bado ni 28 au 32....unakuwa na miaka hiyo kwa miaka 7 hihihihihi. Sitaki mtu wa 20s au over 40s aniambie natakiwa kuvaaje. Nataka mwenye umri husika au anaekaribia sio nyuma miaka 10 au mbele miaka 10.


Unavutiwa na fashion blogger au vlogger  halafu anakuja kukwambia anamiaka 27 how annoying? Vaa umri wako kashenzi wacha kuvaa kama mkimama wa 40s. Sio nakaribia 40 kihiiiiivyo ila sio mbaya kujiandaa si eti. Mambo ya kuanza kujipakaza maanti makunyanzi cream usiku ndio huu.


Nahisi nimekuwa nikivaa vilevile tangu nina miaka 28.....yaani najivika kama 20s wakati nipo kwenye my 30s. (Haya nimekupa wazo la kuanzisha blog.....sema ahsante). Mambo ya mid skirt sijui sitaki....wengine miguu yetu inapendeza ikionekana yote sio nusu wala robo. #minnies ( duh ka nipo twita).

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao