Skip to main content

Kutenganisha jinsia....

Za watoto wakati wa kuoga au kubadilisha.

Siku koja Mwanangu wa kwanza alipokuwa na miaka 3.....well bado ananiaka hiyo, aliuliza "mummy why baby doesnt have ______ like me?"......nkamwambia kwasababu ni binti, mabinti hawana_____(au unataka niseme kwa kiingereza...).

Kuanzia siku hiyo siwaogeshi pamoja wala kuwabadilisha nguo wakiwa chumba kimoja.


Je unadhani muda gani muafaka kutenganisha watoto Kijinsia linapokuja suala la kuokoa kuwabadilusha pamoja?.


Maswali anayouliza babuu kuhusu mwili wake ni magumu sana.....lakini yupo kwenye umri wa kujifunza so hatuna budi kujibu kiuwazi na sio kumkalipia au kumarufuku asiulize maswali kuhusu mwili wake.

Siku kauliza kwanini akikojoa Uume unakua....."mummy when i take pee my _____ grows.....but why?"

Siku nyingine (nilicheka mpaka nikaanguka chini) katoka mbio chooni eti " i went for a poo but then pee want to come so i stopped"......baba mtu akamwambia sometimes it happens so he shouldnt stop.....kwani alirudi chooni!

Akijaiona hii post hukoo baadae anaeza kunisuu kwa kumuaibisha.

Babai.

Comments

Unknown said…
hellooo ,
heri ya mwaka mpy a( ilochelewa)... maana sijapita avenue hii siku nyingi.

Nimecheka na hii post maana mwanangu mie wa kike. Saasa mwaka fulani alipotembelewa na binamu zake toka hukohuko uliko, akamuona binamu yake ( a year older than her by then , kumbe hadi sasa gap ni hiyo hiyo, issshhh but walikuwa wadogo kiasi by then), ana pee kwa kubenjulia kiuno kwa mbele as he was and still is a boy...

Naye si akaanza kung'ang'ania kubenjua ka..... kwa mbele anasema I want to weeeeeee just like S ... does...
na for like two months ilikuwa ni taabu kumwambia akae kwenye toilet seat for a peee.
Aliendelea ku maintain kuwa atasit wakati wa 'big F' tuuu which was her conventional name for a poo.

Wana wana mambo na ndo sehemu ya burudani ya uumbaji wa Mungu.

siku njema kwako na endelea kusukuma mpira mama ( kick the ball)

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao