Skip to main content

Posts

Matiti Makubwa(asilia) Vs Madogo....

Hi! Matiti ni fuko la Fat ambalo halina umuhimu....well zaidi ya kunyonyesha watoto. Sasa kama umemaliza kuzaa what do you do with them hasa yale Makubwa? Sie tulionyimwa matiti bana tukimaliza kunyonyesha tumatiti twetu tunapotea, yaani unabaki na alama ya matiti ambayo hayahitaji Brazia....well inategemea na umbile la titi, maana kama yako ni yale Papai shape au Embe sindano Shape mwenzangu hadithi ni ingine. Kwasababu ukubwa uliongezeka mara 3(mara mbili) kutoka B mpaka D na kifua kutoka 28-34inch.....yes nilikuwa 34D!!, hofu yangu kuu ilikuwa ni matiti kulala baada ya kumaliza kunyonyesha. Lakini baada ya watoto wawili yapo pale pale kati japo sio firm kiviiiiile lakini hayajalala (too small to sleep hahahahaha to sleep). ***Faida chache za kuwa na tumatiti tudogo ni kama ifuatavyo:- -Unanunua Sidiria Duka lolote kwa bei chee(japo huitaji one).....Ile shughuli ya kunyanyua Titi ili kujiswafi chini yake huwezi kuipata -Mambo ya kulala chali na matiti kukimbilia Kwapani haitok

Wanataka uwe single Milele....

Watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki).....heiyaaa! Happy Bank Holiday wa hapa nilipo. Kama bado hujagundua basi utagundua muda si mrefu. Uhusiano wako unaponawiri tu, unaanza kusikia maneno maneno kuhusu Mpenzio au watu wanaomuhusu iwe Familiani au Kazini. Pengine hakukuwa na vijimaneno lakini tangu umefunga Ndoa wameanza kujitenga au kuanzisha urafiki(kufahamiana na watu wengine.....wale ambao wewe hupatani nao aka maadui zako). Au kila kitu kipo sawia na hayo hapo juu hayajawahi kutokea lakini tangu umejifungua au Mkeo kazaa basi na wao "marafiki" wanaanza kupunguza ukaribu kwako. Marafiki hao(watu unaofahamiana nao) wote au nusu na robo yao huwa kwenye Ndoa na Familia na wewe ulikuwa the only SINGLE one or the few of that robo ya mzunguuko wenu wa urafiki. Unaendelea ku-effort-ika(make an effort) kuwatafuta kwa simu au kutafuta muda ili kubadilishana mawili matatu kuhusu maisha yako mapya na yale ya enzi. Hawapatikani au hawatokei kwenye mihadi ya  kufurahia

Ni kweli wa Ughaibuni wajuaji....

Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa? Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu). Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia. Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu  kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa. Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri. Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "stat

Kwanini Weusi sana huenda na Wazungu?

Herooo heri ya J'3! Unakumbuka ile vita ya Weusi na Weusi wenye rangi ng'avu(wewe unawaita Weupe) niliyoigusia hapa mawiki kibao yaliyopita?....haiwezi kuisha hasa kwa nchi hizi za mbele. Kufunga ndoa na mtu Mweupe zaidi yako ni kupoteza muda, Baadhi ya wanadamu (Weusi) wanaamini kuwa unless mwenza wako ni Mzungu.....uhusiano wenu hautodumu. Mmmh come to think of it.....Weupe(Wazungu) wengi(niwaonao) wakiamua kuoa au kuolewa huenda Darker. Umewahi kuona Wazungu wangapi wanafunga ndoa na Waafrika ambao ni a bit lighter/fair. Halafu ukifanya Uchunguzi wako binafsi ambao sio rasmi (obviously)kwenye Sosho Media utagundua au utaona walio na Wazungu kama wenza wao ni weusi sana(deep dark). Lakini pia Ndoa au Mahusiano hufikia mwisho kwasababu nyingine nyingi na Rangi sio moja ya sababu hizo. Hivi ujawahi kujiuliza kwanini wanaume wa Kizungu hujibebea wadada Weusi warembo kweli (model like kiumbo) tofauti na Wanaume Weusi ambao hujikusanyia wamama_____well hurudi home na