Skip to main content

Posts

UK ya leo sio ile ya 1998-2006

Habari? Unajua enzi hizo kuishi Ulaya(ya UK) ilikuwa raha sana na tulikuwa na mahela ya kumwaga.....hata mie nilikuwa tajiri Mwanafunzi. Unakumbuka enzi zile tulipokuwa summer holiday(kipindi kama hiki) unagoma kurudi kwenu na badala yake unabaki Ulaya kupiga Kazi siku 7 za Wiki ili "kufuga" pesa? Wakati wa term mtu kutoka Bongo anakuomba senti.....unamwambia nipe wiki nitakurekebishia......unaenda chukua kazi kwa Wakala na unamaliza tatizo la mtu just like upepo. Fast foward mpaka 2008.....wa Ulaya Mashariki wakaanza kumiminika nankujaza kazi zote za Mawakala tena kwa malipo chee(wanachukua mpaka £3 kwa saa)......sasa mimi Muafrika na yule Mbritish (kiwango cha malipo ni tofauti na wa Ulaya Mashariki)! nikufanyie kazi lwa £3 sijipendi?? Siku hizi ni kama Bongo tu.....kama hujapata bonus kazini kwako basi utabaki na Mshahara ule ule......siku hizi hata zile overtime hazipatikani. Mkurugenzi anachukua extra hours hihihihihi. Sasa mtu akikuomba msaada na  ukamwambia....e

Chunga Ulimi usimuudhi Mpenzi....

Hello! Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Mambo tunayoambiwa tuyafanye kwenye Ndoa ili tuishi kwa Amani ni mengi mno na yanachukua "utambulisho" wetu......halafu vipi kuhusu Ndoa yenye furaha? Mambo kama "usilopokea....soma nyakati kwanza ili usimuudhi mwenza wako", hii inakufanya uwe mtu mwingine na sio wewe.....katika hali halisi ni task itakayokukosesha furaha kwasababu utakuwa unaishi kama mtu mwingine na sio wewe. Unasoma nyakati only kama issue unayotaka kuiwakilisha kwa mwenzio ni ya kubomoa au kujenga Ndoa yenu. Lakini mambo ya kawaida kama vile kutaniana na kuzungumzia watoto hayahitaji "kusoma nyakati". Kingine ni kusema unavyojisikia baada ya kuvumilia vya kutosha.....ujue wakati wote sisi ni wepesi kuona makosa  madogo madogo ya Wenza wetu kuliko kuona yetu(sio rahisi kuona makosa yako). Na ikitokea Mwenza sio mwepesi kukuambia pale unapokosea basi wewe unadhani kuwa ni kawaida tu na unasonga na maisha. Siku yakimfika shingoni anakuambia ras

Ujidhaniavyo sivyo....

Heiyaaa. Mara zote huwa tunaamini tupo vile ambavyo hatupo. Nitakupa mfano:-  Unapoenda kununua Foundation(matope ya kupaka Usoni kabla ya mengineyo) unachagua rangi ambayo sio yako na huwa waaaay lighter. Sio kwamba unakusudia bali hutaki kukubali ile yako ambayo pengine inaonekana ni nyeusi sana kwenye Chupa kuliko unavyoamini(kithihitisho ni Picha zako). Enzi nilikuwa na "Wifi" wa Kiarabu na kwenye familia yao kulikuwa na waliozaliwa nje ya "uarabu" kwamba mzazi mmoja alikuwa Muarabu mwingine Mweusi halafu mtoto (binti) katokea mweusiiii mwenye nywele za kiarabu. Basi tukijikusanya tumapiga stori huyo binti alikuwa anapenda kuwasema wadada wengine kuwa ni Weusi mno kiasi kwamba hawavutii. Kwasababu mzazi wake mmoja ni Muarabu na anaishi kwenye Familia Kiarabu aliamini kuwa na yeye ni Muarabu. Hiyo pia huwatokea watoto waliochanganya na Wazungu na kuishi Uzunguni zaidi kuliko Weusini...huwa wanajidhania kuwa ni Wazungu(rangi wise). Kingine ni uwingi wa nywel