Skip to main content

Posts

Chanya....Wanaume na tofauti zao (SY2)!

Hai? Baada ya sehemu ya kwanza iliyofunikwa na Hasi (bado ninazo kibawo though)nimeona sio mbaya tukiangalia zile tofauti ambazo ni Chanya. Bila kupoteza muda twendeeee! Wanakufia kimahama mpaka hawajielewi lakini sio ki-Romeo....hawa jamaa hawajui kuweka wazi hisia zao wazi kwa kukuambia wanakupenda na kukunidi na kukumisi kila siku, na Kamwe hutowasikia wakisema "bila wewe maisha yangu ni bure". Utakuwa umeambiwa/umesoma mahali kuwa Mwanaume asipokuambia hivyo ujue hakupendi.....sio kweli! Pili, wanafurahi kuonekana kama Familia, yaani siku hizi zile "date night" sijui "outings" hazipo.....kila mkitoka basi na wanenu pembeni. Ukimkumbushia "sisi"anakuambia "watoto bado wadogo kwanini tuwe wa binafsi na kujitoa wenyewe?"(family man?). Tatu, Tangu mmefunga Ndoa hakaribishi rafiki zake ambao ni Single na ukaribu wake kwao unapungua. Sio kwamba anaogopa watakuiba bali anajihisi kuwa kwenye era nyingine ya Maisha yake. Nne, Mara ya m

Baba/Mama yao Mzungu.....?

Watu(Wazungu) wanapouliza kama Mumeo/Mkeo ni Mzungu kwasababu watoto ni weusi na sio WEUSIiiiiii tii, unafurahi? Unakwazika?  au unapata (mie)nafasi ya kutoa Elimu kuwa Weusi wetu Waafrika unatofautiana na kwanini? Nilikwisha wahi gusia kuwa kuna baadhi ya watu Shuleni kwa Babuu wanadhani Baba yake ni Mzungu......nikiwa na Kibibi ambae hana rangi ng'avu sana kama Kaka yake bado watu wanadhani Baba yake ni Mzungu. Halikadhalika watoto wakiwa na Asali wa Moyo (baba yao)bado wanauliza "is their mother white"? Inafikia mahali unachoka kutoa Elimu ya tofauti ya Weusi......jamaa wanadhani Waafrika wote tuna rangi moja kwamba wote ni Chocolate au Dark Chocolate. Ikitokea unakarangi ka Caramel au umepauka zaidi basi wewe ni mixed race(toa macho kwa mshangao)! Sasa hili ni Jepesi kwa Mimi mkimama wa Kitanzania(sikwaziki kirahisi).....ilimtokea Mkimama mmoja wa USA ayeeee alikasirika mpaka akaamua kwenda public(youtube).....Weusi wa USA wapo verevere demaged na Ubaguzi. Pamoj

Kiswahili kwenye Matangazo UKtv

Sema, mambo! Kiswahili kimekuwa Common sasa kama Kiinglish, yaani inakuwa taabu kuwateta watu(not that i teta watu....). Natumia Kiswahili zaidi kuficha ukali wa maneno pale wanangu wanapoleta ujinga. Mfano tupo mtaani na watoto halafu wakawa hawasikii....unawaambia "do you want to chapwa au am going to chapa you"......wanajibu "no dont chapa us" na kuacha ujinga hehehehe. Sasa ukisema neno kuchapa kwa Lugha yao bana utaitwa abuser na unaeza nyang'anywa watoto. To the nukta: Kuna Matangazo mawili ya Kiswahili moja la Holiday (lastminutes.com) na lingine la Bank linalomhusisha Mmasai(Co-operative Bank).....nenda kaguge. Siangalii Tv kihiiiivyo ila wanangu wamenishtua niliposikia wanaimba sijui 'ninini matako'.....nkauliza "where did you learn that word?"......nikaambiwa "its only an advert mum, dont be silly". Nka-rewind si nkakutana na Tangazo la holiday jamaa anaimba kwa Kiswahili pamoja na maneno mengine akatamka "matako&

Wanaume na tofauti zao....

Kuna wale wanaodhani kuwa na wewe ni "Feva" hivyo ushukuru Mungu. Aina hii huwa wanategemea uwafanyie kila kitu kuanzia kuwapikia mpaka kutafuta mbinu za kuendeleza "moto" kwenye ndoa yenu. Unafanya yote hayo na pengine zaidi.....yeye ana-chill tu. Yaani hata ukiumwa hakutengenezei Uji. Inafikia mahali unajiuliza "nafanya yote haya kwa ajili yake, yeye ananifanyia nini? Pili, Wanajifanya wanaujua Usawa kuliko Feminist (well wanaume pia wanaweza kuwa mafeministi as in wanasaidia kupigania Usawa kwa wote). Lakini sasa kwanini ni wewe tu ndio umnunulie Zawadi ghali na wewe kupata Kadi tu kutoka kwake kwenye ile siku yenu Maalum? Tatu, Wazee wa Mipango aka wazito.....huyu bwana ana plans lundo halafu nzuri zinazotekerezeka lakini utekerezaji Sufuri. Sasa si unipe mgao mie nikutekerezee? Mpaka nikuombe....Aiii! Nne, Wadaku.....kila stori ya Mjini anayo yeye....kila mwanajamii wa jamii yake ama anamjua au rafiki yake ni rafiki yake. Anashadadia(bado mnatumia hil