Skip to main content

Posts

Wasichana tuliokulia miaka ya 90...

....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao. Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90. Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza  miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).

Mzazi kukupenda zaidi ya wenzio...

Habari ya sasa! Kwa kawaida Mtoto wa Kwanza na yule wa Mwisho kwenye Familia nyingi hutokea kupendwa zaidi na wazazi au Mzazi......wakati mwingine wadogo/wakubwa zake. Sababu ya kuwa "favourite" angalau kwa muda hapa ipo wazi. Mtoto wa kwanza ndio kifungua Familia na huwa peke yake kwa muda mrefu au ikitokea kuna mdogo wake kaja fasta basi ile "huruma" huwafanya Wazazi waongeze attention kwa yule wa kwanza. Mtoto wa mwisho ni mdogo kuliko wote hivyo Wazazi na dada/kaka huwa over protected. Pamoja ya kupendelewa au kupendwa zaidi bado Wazazi wengi huwa hawaonyeshi hilo kwa uwazi ili kuepusha ugomvi au kuwafanya watoto wengine kujiona hawapendwi kwa kiwango sawa. Lakini mnapofikia umri mkubwa unaweza kuona kabisa kuwa Baba na Mama wanampendelea fulani zaidi na hivyo kuanza kujenga chuki au ushindani dhidi ya mwenzenu ambae mnahisi kuwa anapendelewa. Hali hufikia pabaya, mpaka anaependelewa kuanza kujidai na kutumia kupendwa zaidi na Waza

Bora alama ya Mstari kuliko F.....Miaka 20 Tangu Secondary

Mambo! Ijumaa Mpya(ya Kwanza Mwezi huu) na Maalum kabisa kwani ni Wiki ya Kwanza tangu kuanza kwa Mitihani ya Kumaliza Kidato cha Nne Tanzania, na ndio Mwanzo wa Mwisho wa Series hii(inaonekana kupedwa/somwa zaidi), inapendeza! Utakuwa unajua by now kuwa Mie na Hisabati sio marafiki, Biology niliipenda kwenye kuandika Essay kuhusu Maambukizo au Magonjwa(niliyajua haya kutokana na Somo la Sayansikimu kutoka Msingi), mengineyo nilikuwa sielewi(nilikuwa nasinzia). Mwalimu wetu wa Biology Kidato cha Tatu-Nne alikuwa a bit Boring au alikuwa  na Mapepo(hihihi). Yule mama alipokuwa akiingia na kufungua Mdomo "Good afternoon" mie yuleeeee Uzaramoni.....yaani macho yanakuwa mazito halafu nalala ule usingizi Mzito m paka Udenda! Nikaona aah isiwe shida bana, nikawa siingii kwenye Kipindi chake unless kuna Essay hehehehe. Sikufanya Mitihani Miwili  nayo Hisabati na Biology, kwasababu nilijua wazi sitofanikiwa kufanya vizuri na matokeo yake nikaamua ni Bora nipate alam