Skip to main content

Posts

Mzunguuko wa Ngono kwa Mwanamke...

Jambo! Kama unakumbuka niliahidi kuwa nikipata muda nitaandika kuhusu Mzunguuko wa Hedhi ambao unaendana na Mzunguuko wa Kufanya Ngono/Mapenzi kwa Mwanamke. Nilielezea kuwa Mwanamke sio kama Mwanaume, kwamba tunakabiliana na mambo mengi ukiachilia mbali Homono(Pengine ni Homono tu). Kuna siku Mwanamke analianzisha, inaweza kuwa mara moja au tatu kwa mwezi. Pia kuna siku mwanamke anataka kuwa Juu sio kwasababu wewe Mkibaba unataka bali mwili wake unamtuma kutaka kuwa in-control na hii inaweza kutokea mara kadhaa ndani ya mwezi lakini sio kila siku. Hali kadhalika zipo siku(ambazo ni nyingi) mwanamke anataka kuhisi kupendwa  na kujaaliwa kwa vitendo(kitandani)......vinginevyo Tendo halitokuwa na maana na halitokuwa la kufurahia. Wale Wanawake na Wanaume mabingwa wa kuwalaumu wanawake kuwa ndio sababu ya Waume zao kutereza nje ni ama hawaujui Mwili wa Mwanamke, kwamba mwanaume ataka na kutegemea Mwanamke awe in control kila siku......au kungojea Mwanamke alianzishe ili afurahi

Kulazimisha Mtoto awe na Mawazo....

Pengine ni ngumu kujua tofauti ya ku-share information kwa nia ya kuwafanya watambue "Asili" yao, wajifunze kuhusu Upande wa pili(kwa wale waishio Ughaibuni) na kuwapa watoto mawazo. Natambua kuwa kila Mzazi ana namna yake ya kulea na kufunza wanae, na kamwe sitokufundisha namna ya kulea wanao tangu mie mwenyewe  najifunza kila siku. Lakini tukumbuke kuwa kuna "Common Sense".....huitaji Elimu wala Uzoefu kuitumia. Unakumbuka ulipokuwa Mdogo na Mama au Baba au mtu yeyote wa karibu anaanza Hadithi za "Kaka/Dada" yako aliezaliwa na kufariki.....kisha ukaanza kuwaza ingekuwaje hivi sasa kama angekuwepo? Unawaza huko aliko je anafuraha, ana-toys,? unakuwa na Maswali kibao ambayo hayana Majibu. Mtoto anakosa usingizi kwa Mawazo au Uoga na akilala anamuota "dada/kaka". Wazazi hapa hudhani/amini kuwa Mtoto ana connection na "mwenzie"....lakini ukweli ni kuwa anasumbuka Kiakili na Kihisia. Pia umewahi kutambulishwa kwa Ndugu ya

Era ya Kulazimishana ku-react!

Heiyaaa! Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia  unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k. Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe. Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k. Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe&

Wasichana tuliokulia miaka ya 90...

....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao. Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90. Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza  miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).