Tuesday, 24 November 2015

Kulazimisha Mtoto awe na Mawazo....


Pengine ni ngumu kujua tofauti ya ku-share information kwa nia ya kuwafanya watambue "Asili" yao, wajifunze kuhusu Upande wa pili(kwa wale waishio Ughaibuni) na kuwapa watoto mawazo.
Natambua kuwa kila Mzazi ana namna yake ya kulea na kufunza wanae, na kamwe sitokufundisha namna ya kulea wanao tangu mie mwenyewe  najifunza kila siku. Lakini tukumbuke kuwa kuna "Common Sense".....huitaji Elimu wala Uzoefu kuitumia.Unakumbuka ulipokuwa Mdogo na Mama au Baba au mtu yeyote wa karibu anaanza Hadithi za "Kaka/Dada" yako aliezaliwa na kufariki.....kisha ukaanza kuwaza ingekuwaje hivi sasa kama angekuwepo? Unawaza huko aliko je anafuraha, ana-toys,? unakuwa na Maswali kibao ambayo hayana Majibu. Mtoto anakosa usingizi kwa Mawazo au Uoga na akilala anamuota "dada/kaka". Wazazi hapa hudhani/amini kuwa Mtoto ana connection na "mwenzie"....lakini ukweli ni kuwa anasumbuka Kiakili na Kihisia.

Pia umewahi kutambulishwa kwa Ndugu yako ambae Baba/Mama alizaa wakati wa "ujana" na sasa anaishi na Mzazi mwingine ambae sio Baba/Mama yako. Unaanza kuwaza na ku-wish ama ungeishi kule au yeye angekuja kuishi hapo kwenu. Unatamani kuwa Wazazi wenu wangekuwa wamoja(baba na mama mmoja). Kwa Mzazi mmoja ambae ni Mzazi wa Mtoto wa Upande wa pili huona ni Jambo jema kwamba Mtoto huyu ana-value undugu wake na mtoto yule wa kabla ya Ndoa......Ukweli ni kuwa unateseka Kiakili na kihisia kuhusu Jambo hilo.
Halafu unakumbuka ile hofu uliyokuwa nayo pale Mzazi wako anapokuambia hana Pesa na XMas imekaribia, sio tu mtakula Ugali badala ya Pilau pia hakuna Sare  Mpya za Shule, Madaftari wala Kalamu....yaani unaenda shule na Sare zako zilizochakaa. Unapata Donge rohoni(unaijua ile hali ya kutaka kulia lakini huwezi kulia, huwa kuna maumivu  si maumivu fulani sehemu ya Koo hihihihihi)....Roho inakuuma na unakosa Amani kabisa kila Baba/Mama anaporudi Mikono Mitupu na ni tarehe 22 Dec!!....kwa Mfano.
Mzazi hapaswi kumuambia Mtoto kuwa hana Pesa, hilo ni jukumu lako kwasababu wewe ndio ulieamua "kumleta" ama kwa Uzembe au kwa Kupanga. Kwanini huamishie "Hatia" zako kwa mtoto na hivyo kumpa mawazo? Kama mzazi tafuta namna kwa uwezo wako wote  na kuhakikisha unatimiza mahitaji ya Mtoto. Mtoto haitaji kujua kama una Pesa ama huna au unazipataje.Kuna wakati unakuta Mtoto anakuwa Mkimya sana(anakuwa na mawazo au depressed), lakini kutokana Umri wake unadhani kuwa hana Mawazo na hivyo ameamua tu kutulia leo(ameamua kuwa  mtoto Mzuri). Ukweli ni kuwa Mtoto anaanza kuwaza akiwa na Umri Mdogo sana kuliko tunavyofikiria.
Wazazi ndio chanzo cha Mengi Mabaya au Mazuri linapokuja suala la Ukuaji wa mtoto Kiafya, Kiakili, Kisaikolojia n.k. hivyo ni muhimu kutafakari na kujua Mipaka ya Info gani zinapaswa kuwa shared kwa umri husika.
Mtoto anapozaliwa huwa Mtupu akilini. Kila siku hujitahidi kujaribu na kufanya mengi, Mtoto huyu haitaji kuwa "feeded" masuala mengine ambayo hayamhusu kwa Umri alio nao! Muache mtoto awe mtoto.....muache awe huru. Mtoto anakabiliana na mengi katika kujifunza na hivyo haifai kuanza "kupandikiza" hatia zako za Mtoto uliemuacha kwa Baba/Mama yake, kwa mtoto huyu kwa kisingizio cha "nataka ajue kuwa ana Kaka/Dada" hai au katangulia.
Pia sio sahihi "kupandikiza" hatia za ukosaji wako wa pesa kwa mtoto kwa kisingizio cha "nataka ajue ugumu wa kutafuta" au "nataka ajifunze mapema kuhusu utafutaji wa Hela". Subiri mpaka afikishe Miaka 8, pale unapoanza kumshikisha Pocket money(pesa ya kutumia shule) tena unamfunza kutunza sio "kutafuta".Wacha niishie hapa, Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa,  ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

No comments: