Skip to main content

Posts

Mzazi Mkali Vs Mpole....

Hello! Utakoma na Post za Wazazi na Watoto mahali hapa, ni maisha niishiyo sasa na sio mbaya kama nikichangia uzoefu wangu ambao pengine unafanana na wako na hivyo kukufanya kujisikia nafuu kuwa haupo peke yako au ukanishangaa. Vilevile inawezekana kabisa ukajifunza jambo! Hofu yangu kuu ni Waanangu kuwa na Tabia mbaya chini ya uangalizi wangu, kutokuwa na Heshima kwetu Wazazi wao na Watu wengine. Hofu hii ndio iliyochangia mimi kujitolea Mhanga na kuwa Mama wa nyumbani kwa Miaka 3.  Sikutaka Wanangu waje na tabia za "Nursery assistant".....Babuu alianza Nursery akiwa Mchanga as bado nilikuwa na ile " I can do all, independent woman".....untill Mwanangu alipoanza kunikataa na kulia kwa Uchungu kila nilipokuwa naenda kumchukua! Vilevile alipofikisha Miezi 8 akawa na "vijitabia" ambavyo siku pendezwa navyo.....Solution? nikapunguza Masaa ya Kazi na Nursery(so kutoka full time akawa anaenda kwa 5hrs). Niliamini(bado naamini) kuwa Mtoto anahitaji

Mtoto wa Kiume vs Wa Kike....

....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi. Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja). Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume.  Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika  kuwa huyu

Mpenzi akuone uKizaa vs uKinya.....

Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora  Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi. Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake. Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki). Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni. Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka &quo