Hello!
Utakoma na Post za Wazazi na Watoto mahali hapa, ni maisha niishiyo sasa na sio mbaya kama nikichangia uzoefu wangu ambao pengine unafanana na wako na hivyo kukufanya kujisikia nafuu kuwa haupo peke yako au ukanishangaa. Vilevile inawezekana kabisa ukajifunza jambo!
Hofu yangu kuu ni Waanangu kuwa na Tabia mbaya chini ya uangalizi wangu, kutokuwa na Heshima kwetu Wazazi wao na Watu wengine. Hofu hii ndio iliyochangia mimi kujitolea Mhanga na kuwa Mama wa nyumbani kwa Miaka 3. Sikutaka Wanangu waje na tabia za "Nursery assistant".....Babuu alianza Nursery akiwa Mchanga as bado nilikuwa na ile " I can do all, independent woman".....untill Mwanangu alipoanza kunikataa na kulia kwa Uchungu kila nilipokuwa naenda kumchukua!
Vilevile alipofikisha Miezi 8 akawa na "vijitabia" ambavyo siku pendezwa navyo.....Solution? nikapunguza Masaa ya Kazi na Nursery(so kutoka full time akawa anaenda kwa 5hrs). Niliamini(bado naamini) kuwa Mtoto anahitaji Mama yake 24/5 (ondoa Masaa ya Nursery) Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake(mie sio Feminist so nisamehe kama sitomtaja sana Baba).
Kiasilia Mimi ni Mkali(sipendi ujinga), inawezekana ni kwasababu ya kuwa na wadogo wengi zaidi kuliko kuwa na wakubwa(mie ni wa Pili kuzaliwa na ni Dada mkubwa). Ukali wangu ni kwa watoto wote sio wadogo zangu tu(walipokuwa wadogo) bali hata kwa watoto wa Watu niliokua na "babysit" au wale waliokuwa wakija kunitembelea kutokana na kufahamianakwangu na Wazazi wao.
Pamoja na Ukali pia mimi ni Manners "fanatic"(usiende kuGugo), nachukia watu/watoto wasio na Manners. Mara zote huwa napitisha Hukumu kuwa Mama zao hawakuwafunza, kwasababu naamini mtoto anajifunza "manners" kati ya Miaka 2 na 5, uki-"lemaa" katika Umri huo basi wewe na wao are done!
Kuanza kumfunza mtoto Manners katika Umri mkubwa ni kazi zaidi kuliko umri nilioutaja hapo juu, umri wa Miaka 2-5 mtoto hujifunnza "misingi" ya mambo mengi na kuitunza, hivyo ukianza mapema inakuwa rahisi "kumkumbushia" akivuka umri huo kuliko kuanza upya.
Kumbuka mtoto anapozaliwa huwa hajui kitu(well labda kunyonya), Ubongo wake huwa "pure", sasa yote mfanyayo kama wazazi au Mlezi(kwa wale wanaoachia watoto watu wengine) huwa ni mara ya Kwanza kwa Mtoto. Mungu anisaidie na kunipa nguvu ili Wanangu wakue wakijua umuhimu wa kuwa Wema, kuheshimu, kuomba na kushukuru.
Kwenye Familia yetu ya watu Wanne, Mimi Mama ni Mkali/Mnoko) na Baba yao ni Mpole(laid back)....kuna mahali tulikuwa tunapishana kwenye malezi, kwamba mimi nikikataza Watoto wasifanye jambo, wanakimbilia kwa Asali wa Moyo(baba yao) na yeye anawakubalia. Ikafikia Dad akawa their best friend na mie nikawa sio Friend of any sort hihihihi.
Ikabidi "Work as a Team" iingizwe ili Watoto wajue kuwa Mama akisema HAPANA basi hata wakikimbilia kwa Baba ni HAPANA. Haikuwa rahisi kama kwenye kila kitu unachowafunza kwenye Umri huo mdogo.
Pamoja na ukali wangu, sijawahi kuwachapa, vitisho kama "I will call Nunda for you", "will give you Time out", will taka away Toys au Tablets bado zinafanya kazi. Sasa wewe ni Mzazi wa aina gani/ Mkali/Mnoko au Mpole?
**Nunda= to them is like a Monster
Ahsante kwa Muda wako hapa, nathamini na kuheshimu uamuzi wako wa Kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments