...hamaanishi kwamba ukatafute kweli mwingine, anachomaanisha ni kuwa "nibembeleze na unihakikishie kuwa utanivumilia" mpaka nitakapo kaa sawa Kihomono au kupona(kama alikuwa anaumwa)....Za Miezi Miwili/Mitatu? hello, jambo jambo!! Kwa kawaida Mume anapopatwa na tatizo kubwa litakalomfanya ashindwe kutekeleza Majukumu yake kama Baba na Mume, Mwanamke atavumilia na kumuuguza, kumpa Moyo na Matumaini. Lakini Mwanamke akijifungua(zaa) achilia mbali kuugua....katoa Uhai wa Mtu salama baada ya Miezi 9 kukaa na kulala kwa tabu. Mara zote kipindi hiki huwa Kigumu sana japokuwa kasumba ya Jamii "kukuharakisha" upone haraka huficha ukweli kuwa Mwanamke anapojifungua hukabiliana na mambo mengi Kiafya(kimwili, kihisia na kiakili). Hali ambayo hufanya baadhi ya Wanaume kuamini kuwa Mimba na kuzaa ni "cha mtoto" tu, sio kazi(kama alivyo pizi ndani ya dakika zake 3 kwa utambu uliodumu kwa sekunde 90)....hakuna ugumu wowote, fyatueni tu. Kwa kawaida(uzoefu wa