Skip to main content

Posts

Kila Familia/Ukoo ina mtu huyu...

  ...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama  ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(ina

Mtoto wa kambo...part 2.

Mtoto wa kambo...part 2. Ukiachana na misukosuko ya txt na simu za mama mtoto, kuna suala la kufanya mapenzi ambalo wengi huwa hawalizungumzii sababu wanaogopa kuambiwa hawajiamini. Unless wewe una-elements za kichawi au zile za ukimada ndio utaweza kuwa na a very good sex life on the daily (kila anapowasiliana na mkimama wake wa awali kabla yako, unapata mhamko).   Vinginevyo bana the thought of dudu kuingia kwa mwanamke mwingine bila kinga itakuondolea hamu na ile desire kwa mpenzi wako inatoweka, unaanza kujiambia “omg nimekosea kuchagua”, kama umeshawi humuona ex unaanza kujiuliza kama jamaa ana type na wewe umefanana na Ex wake, unapata kinyaa…unawaza “niingie mitini nini?”, unaendelea kuwaza “yaani ndio nimejitolea mhanga maisha yangu yote yatakuwa kupambana na drama za ex”, “si bora niwe single and happy” …yaani akili haitulii. Na kama ujuavyo bila akili kutulia, hakuna ushirikiano na bila ushirikiano tendo hakuna, ukifanya linakuwa doro.     Kwa uzoefu wangu na wenetu wat

Mtoto wa kambo(part 1)...

Mtoto wa kambo sehemu ya kwanza.... Kambo maana yake nini? Ikiwa mtoto alizaliwa nje au kabla ya ndoa nae anaitwa mtoto wa kambo? au ni kwa wale waliozaliwa ndoani halafu  ndoa ikafeli au mzazi mmoja kafariki halafu  baba/mama kaoa/olewa tena?  Mnaona mlivyo haribu/changanya mambo baada ya kuua umuhimu wa ndoa na kujenga familia? Mtoto kabla na nje ya ndoa (Wanaharamu) huwa hawajulikani/hawana umuhimu(kwa Waislamu hii bado imesimama). Nimekukwaza? ndio ukubwa huo.😁 Mama/baba wa kambo inatumika zaidi Mikoani, huku kwetu Pwani tunatumia sana Mtoto wa kufikia(kwamba umefika   kimapenzi kwa mwanamke/mwanaume ukamkuta mtoto kutoka ndoa iliyopita?)…sina uhakia. Nitatumia maneno mtoto na watoto interchangeably. Nani alipitisha sheria ya kulazimisha watu wawapende watoto waliowakuta kwa watu waliowadondokea kimapenzi? Yaani ukionyesha huna habari na uzao wa mwanamke/mwanaume kabla yako basi unaitwa Mwanga, unaroho mbaya n.k. Utapendaje mtu wala humjui na hana faida kwako?  Natambua kuna msemo

Jinsi ya kujenga/kuza“character” ya mtoto wako.

Jambo wewe, Kulea Watoto Ughaibuni ambako kuna Kacha tofauti na Kacha tuliokulia nazo inaweza kuwa a bit confused, hasa kama umetoka zako Afrika (bongo as in Tz ikiwepo) na Kacha ya U-marekani mweusi. Unazaa Watoto na hujui uwalee katika kacha gani, nap engine unajiuliza hivi huku ulipo wanao wana kacha yeyote au wafuate kacha ya watu wanaofanana nao(Weusi wenzao aka Black Culture)? Unasahau kuwa kila mweusi wa Ulaya ana kacha yake aliokuzwa nao kulingana kabila lake na wapi anatokea Afrika.     Kwa kifupi nchi kama UK hakuna Black culture (wanalazimisha kuuingiza U-black Amarekan) bali kuna Culture za Afrika na Caribbean ila kwa wale wazazi waliokuja na U-black amerika kutoka Afrika basi huamini kuwa Culture ya Black amerika ndio Black culture Dunia nzima na hivyo kuindeleza. Hizo kacha   zetu za Afrika na Caribbean hazidumishwi na Taifa zaima la UK isipokuwa jamii husika ni kama ambavyo jamii nyingine ya wazungu kutodumisha Kacha zao Kitaifa kwasababu UK ina mataifa mengi hivyo k