Mtoto wa kambo...part 2.
Ukiachana na
misukosuko ya txt na simu za mama mtoto, kuna suala la kufanya mapenzi ambalo
wengi huwa hawalizungumzii sababu wanaogopa kuambiwa hawajiamini. Unless wewe
una-elements za kichawi au zile za ukimada ndio utaweza kuwa na a very good sex
life on the daily (kila anapowasiliana na mkimama wake wa awali kabla yako,
unapata mhamko).
Vinginevyo
bana the thought of dudu kuingia kwa mwanamke mwingine bila kinga itakuondolea
hamu na ile desire kwa mpenzi wako inatoweka, unaanza kujiambia “omg nimekosea
kuchagua”, kama umeshawi humuona ex unaanza kujiuliza kama jamaa ana type na
wewe umefanana na Ex wake, unapata kinyaa…unawaza “niingie mitini nini?”,
unaendelea kuwaza “yaani ndio nimejitolea mhanga maisha yangu yote yatakuwa kupambana
na drama za ex”, “si bora niwe single and happy” …yaani akili haitulii. Na kama
ujuavyo bila akili kutulia, hakuna ushirikiano na bila ushirikiano tendo
hakuna, ukifanya linakuwa doro.
Kwa uzoefu
wangu na wenetu watatu, napenda nikuambie kuwa Watoto wanakera, wanaudhi,
wasumbufu na wakati mwingine wanakukosea adabu(wanakujaribu)…sasa kwa sababu ni
wanao “reaction” yako inaweza kuwa kali na kuwaadhibu au ya wastani na kudharau
inategemea wamefanya nini kati ya hayo niliyoyataja. Kwa vile ni Watoto wako
utawaambia wamevuka mipaka/wamekosea nini (vitu ambavyo tayari umewafunza) na ndio
maana umewaonyesha ukali/adhibu. Wanasubiri baba yao aje halafu wanakushitaki
hihihihi...imagine huyo ni mtoto wa Mwanamke mwingine alielala na Mumeo kabla hamjakutana
iwe ilikua kwa bahati “mbaya”, makusudi au uzembe akazaliwa, vyovyote
utakavyofanya utaonekana umemuonea.
Watoto
kuanzia umri wa miaka 5 huwa na uelewa mzuri tu wa mambo, huwa na personalities
na huonyesha characters zao kulingana na malezi yao. Mtoto mwenye umri huu huwa
na attitudes ambazo huwa ni changamoto kwa wazazi na walimu wake, changamoto huzidi ikiwa wewe
sio mzazi wake. Mtoto wa umri huu na kuendelea ndoto yake ni siku moja baba na
mama yake kuishi pamoja kama familia(hii sio jamii imetuaminisha ni asili ya
mwanadamu)….mtoto katika umri huu hajakutana na Jamii kwa kiasi cha kuaminishwa,
ni hitaji asilia la mtoto yeyote yule bila kujali mzazi mmoja yupo hai ila haishi nae au amefariki.
Kila mtu aje na mtoto wake m-blend kwa usawa.
Huwezi
kumkataza mtoto huyo kumzungumzia mama yake kwa baba yake ambae ni mumeo(tunarudi
kulekule kwenye kuharibiana mambo), huwezi kumkataza mtoto huyo kukwambia kuwa
wewe sio Mama yake, na hata kukuhutumu kuwa wewe ndio sababu Mama yake na Baba
yake waliachana(haijalishi ulikutana na mumeo kabla au miaka 5 baada ya
kuachana na mama yake). Huwezi kumzuia mtoto huyo Kwenda kusema mambo negative
kuhusu wewe kwa mama yake hata kama ni uongo kitu ambayo itaendeleza drama kila
mtoto akija kwa baba yake ambae ndio Mumeo.
Kukabiliana
na stress kutokana na tabia za mtoto katika umri huo ambazo huwezi
kuzibadilisha na huna mamlaka ya kumrekebisha na kumfunza ni kazi ya ziada. Sasa
imagine wewe hujawahi kuwa na mtoto na pengine
huna mapango wa kuwa mama anytime soon, unalazimishwa kupenda mbegu(mtoto) ya
Boga ulilolipenda(mumeo).
Sio kila
mwanamke kaumbwa kuwa Mama wa kufikia,
na kwa vile tu kaoeolewa na mwanaume mwenye mtoto/watoto kabla yake haimfanyi yeye
kuwa mama yake wa kufikia automatically. Sio kila mwanadamu kaumbwa kupenda watoto wa
mwanadamu mwingine ambao hawna uhusiano nao biologically.
Utasema “mbona
wanaume huwa wanaishi vizuri tun a Watoto aliowakuta kwa mwanamke kabla yake”….ni
kwasababu mwanaume sio mtu anaetumia muda mwingi nyumbani kulea, kufunza,
kulinda, kukaa na Watoto, na mara zote kama kuna issue ya Watoto ambao sio wa
mumewe, mke mtu hawezi kuripoti malalamiko kwa mumewe kwa kuhofia wanae
kuadhibiwa na Watoto huwa wamekatiwa mawasiliano ya uso kwa uso na Baba yao
hivyo hakuna drama kutoka upande ule.
Kumuadabisha
mtoto ambae sio wako sio rahisi, na kumuacha aendelee kufanya ujinga na kukudharau ndani ya nyumba yako pia sio
sahihi, sasa suluhisho hapo ni nini? Ni Mtoto kukaa kwa mama yake halafu Baba
na mtoto husika kuwasiliana/kutana(bila mama mtu) mara kadhaa kwa mwezi kujenga
bond(inategemea na mama husika, kama mama mkorofi basi unaacha mazima) ila unaendelea kutimiza wajibu wako
mpaka mtoto awe mkubwa na kujitegemea na akakutafuta…I guess.
Watoto
ambao ni matokeo ya talaka(talaka ambayo
haihusishi abuse au cheating) au kifo huwa tofauti. Watoto hawa huwa wamelelewa
na wazazi wao wote na hivyo wana-values zilezile, japo kuwa kila mmoja as an
individual atakuwa personalities zake ila tabia zao zinaweza kufanana kiujumla
kwasababu wamelelewa na wazazi wote wawili. Baba yao anaweza kuwaadabisha na wewe
ukafuata mfano tofauti na “oops babies” ambao wengi wamelelewa na Mzazi mmoja
ambae mara zote huwa mama hivyo baba humpendelea zadi mtoto na kuogopa kumuadabisha ili mtoto
asijisikie vibaya kwasababu ya hatia aliyonayo kutokana na kufiwa.
Kwasababu tu
unatoka na baadae kufunga ndoa na mtu mwenye mtoto haikufanyi wewe kuwa Mama
yake wa kufikia moja kwa moja, kuolewa na mwanaume huyo haikupi haki wewe
kuchukua nafasi ya marehemu mama yake na kutaka sifa kutoka kwa jamii kuwa
“Bakari kaoa mwanamke kweli kweli, anapenda Watoto wa bakari kama wake” wakati
hujawahi kuzaa.
Muhimu ni
kumchukulia na kum-treat mtoto kama mtoto, kwa kuzingatia situation yake(kafiwa
na mama yake) nenda nae taratibu na kumuonyesha utu na upendo kama mwanadamu
mpaka mtoto/watoto atakapokuwa “comfortable” na wewe na kuanza kukuita Mama. Soma part 1 hapa
Hitimisho: Ni
vema kuwa na uhusiano na mtu asie na mtoto kama wewe ili kufanya Maisha yawe
rahisi kwenu kama wapenzi na hivyo kukabiliana kirahisi na changamoto za
muungano wenu(ni nzito). Ikiwa tayari una mtoto ni vizuri kuwa na mtu ambae nae
ana mtoto ili iwe rahisi kukabiliana na Watoto wenu kwasababu wote mnauzoefu na
pia wazazi wao na ninyi kama wazazi wa
blended family.
Kwasababu tu umeoa mwanamke mpya umpendae,
haina maana Watoto wako uliowazaa kabla yake watampenda pia hivyo
usiwalazimishe kumpenda na kumuita “Mama”, vilevile haina maana mkeo huyo atapenda
mtoto/watoto wako kutoka ujanani/talaka/kifo. Upendo haulazimishwi, waki-click
na upendo kuibuka kati yao great, ikitokea hakuna upendo pia poa, muhimu ni kuwa
na mipaka na mipaka iyo iwekwe wazi kwa Watoto na kuheshimiwa.
Nitakuona baadae wiki hii. Bai!
Comments