Skip to main content

Mtoto wa kambo...part 2.


Mtoto wa kambo...part 2.

Ukiachana na misukosuko ya txt na simu za mama mtoto, kuna suala la kufanya mapenzi ambalo wengi huwa hawalizungumzii sababu wanaogopa kuambiwa hawajiamini. Unless wewe una-elements za kichawi au zile za ukimada ndio utaweza kuwa na a very good sex life on the daily (kila anapowasiliana na mkimama wake wa awali kabla yako, unapata mhamko).

 

Vinginevyo bana the thought of dudu kuingia kwa mwanamke mwingine bila kinga itakuondolea hamu na ile desire kwa mpenzi wako inatoweka, unaanza kujiambia “omg nimekosea kuchagua”, kama umeshawi humuona ex unaanza kujiuliza kama jamaa ana type na wewe umefanana na Ex wake, unapata kinyaa…unawaza “niingie mitini nini?”, unaendelea kuwaza “yaani ndio nimejitolea mhanga maisha yangu yote yatakuwa kupambana na drama za ex”, “si bora niwe single and happy” …yaani akili haitulii. Na kama ujuavyo bila akili kutulia, hakuna ushirikiano na bila ushirikiano tendo hakuna, ukifanya linakuwa doro.

 

 Kwa uzoefu wangu na wenetu watatu, napenda nikuambie kuwa Watoto wanakera, wanaudhi, wasumbufu na wakati mwingine wanakukosea adabu(wanakujaribu)…sasa kwa sababu ni wanao “reaction” yako inaweza kuwa kali na kuwaadhibu au ya wastani na kudharau inategemea wamefanya nini kati ya hayo niliyoyataja. Kwa vile ni Watoto wako utawaambia wamevuka mipaka/wamekosea nini (vitu ambavyo tayari umewafunza) na ndio maana umewaonyesha ukali/adhibu. Wanasubiri baba yao aje halafu wanakushitaki hihihihi...imagine huyo ni mtoto wa Mwanamke mwingine alielala na Mumeo kabla hamjakutana iwe ilikua kwa bahati “mbaya”, makusudi au uzembe akazaliwa, vyovyote utakavyofanya utaonekana umemuonea.

 

 Watoto kuanzia umri wa miaka 5 huwa na uelewa mzuri tu wa mambo, huwa na personalities na huonyesha characters zao kulingana na malezi yao. Mtoto mwenye umri huu huwa na attitudes ambazo huwa ni changamoto kwa wazazi  na walimu wake, changamoto huzidi ikiwa wewe sio mzazi wake. Mtoto wa umri huu na kuendelea ndoto yake ni siku moja baba na mama yake kuishi pamoja kama familia(hii sio jamii imetuaminisha ni asili ya mwanadamu)….mtoto katika umri huu hajakutana na Jamii kwa kiasi cha kuaminishwa, ni hitaji asilia la mtoto yeyote yule bila kujali mzazi mmoja yupo hai  ila haishi nae au amefariki.

 

Kila mtu aje na mtoto wake m-blend kwa usawa.

Huwezi kumkataza mtoto huyo kumzungumzia mama yake kwa baba yake ambae ni mumeo(tunarudi kulekule kwenye kuharibiana mambo), huwezi kumkataza mtoto huyo kukwambia kuwa wewe sio Mama yake, na hata kukuhutumu kuwa wewe ndio sababu Mama yake na Baba yake waliachana(haijalishi ulikutana na mumeo kabla au miaka 5 baada ya kuachana na mama yake). Huwezi kumzuia mtoto huyo Kwenda kusema mambo negative kuhusu wewe kwa mama yake hata kama ni uongo kitu ambayo itaendeleza drama kila mtoto akija kwa baba yake ambae ndio Mumeo.

 

 Kukabiliana na stress kutokana na tabia za mtoto katika umri huo ambazo huwezi kuzibadilisha na huna mamlaka ya kumrekebisha na kumfunza ni kazi ya ziada. Sasa imagine wewe hujawahi kuwa  na mtoto na pengine huna mapango wa kuwa mama anytime soon, unalazimishwa kupenda mbegu(mtoto) ya Boga  ulilolipenda(mumeo).

 

Sio kila mwanamke kaumbwa kuwa Mama wa  kufikia, na kwa vile tu kaoeolewa na mwanaume mwenye mtoto/watoto kabla yake haimfanyi yeye kuwa mama yake wa kufikia automatically.  Sio kila mwanadamu kaumbwa kupenda watoto wa mwanadamu mwingine ambao hawna uhusiano nao biologically.

 

Utasema “mbona wanaume huwa wanaishi vizuri tun a Watoto aliowakuta kwa mwanamke kabla yake”….ni kwasababu mwanaume sio mtu anaetumia muda mwingi nyumbani kulea, kufunza, kulinda, kukaa na Watoto, na mara zote kama kuna issue ya Watoto ambao sio wa mumewe, mke mtu hawezi kuripoti malalamiko kwa mumewe kwa kuhofia wanae kuadhibiwa na Watoto huwa wamekatiwa mawasiliano ya uso kwa uso na Baba yao hivyo hakuna drama kutoka upande ule.

 

 Kumuadabisha mtoto ambae sio wako sio rahisi, na kumuacha aendelee kufanya ujinga  na kukudharau ndani ya nyumba yako pia sio sahihi, sasa suluhisho hapo ni nini? Ni Mtoto kukaa kwa mama yake halafu Baba na mtoto husika kuwasiliana/kutana(bila mama mtu) mara kadhaa kwa mwezi kujenga bond(inategemea na mama husika, kama mama mkorofi basi unaacha  mazima) ila unaendelea kutimiza wajibu wako mpaka mtoto awe mkubwa na kujitegemea na akakutafuta…I guess.

 

 Watoto ambao  ni matokeo ya talaka(talaka ambayo haihusishi abuse au cheating) au kifo huwa tofauti. Watoto hawa huwa wamelelewa na wazazi wao wote na hivyo wana-values zilezile, japo kuwa kila mmoja as an individual atakuwa personalities zake ila tabia zao zinaweza kufanana kiujumla kwasababu wamelelewa na wazazi wote wawili. Baba yao anaweza kuwaadabisha na wewe ukafuata mfano tofauti na “oops babies” ambao wengi wamelelewa na Mzazi mmoja ambae mara zote huwa mama hivyo baba humpendelea  zadi mtoto na kuogopa kumuadabisha ili mtoto asijisikie vibaya kwasababu ya hatia aliyonayo kutokana na kufiwa.

 

 Kwasababu tu unatoka na baadae kufunga ndoa na mtu mwenye mtoto haikufanyi wewe kuwa Mama yake wa kufikia moja kwa moja, kuolewa na mwanaume huyo haikupi haki wewe kuchukua nafasi ya marehemu mama yake na kutaka sifa kutoka kwa jamii kuwa “Bakari kaoa mwanamke kweli kweli, anapenda Watoto wa bakari kama wake” wakati hujawahi kuzaa.

 

Muhimu ni kumchukulia na kum-treat mtoto kama mtoto, kwa kuzingatia situation yake(kafiwa na mama yake) nenda nae taratibu na kumuonyesha utu na upendo kama mwanadamu mpaka mtoto/watoto atakapokuwa “comfortable” na wewe na kuanza kukuita Mama. Soma part 1 hapa

 

Hitimisho: Ni vema kuwa na uhusiano na mtu asie na mtoto kama wewe ili kufanya Maisha yawe rahisi kwenu kama wapenzi na hivyo kukabiliana kirahisi na changamoto za muungano wenu(ni nzito). Ikiwa tayari una mtoto ni vizuri kuwa na mtu ambae nae ana mtoto ili iwe rahisi kukabiliana na Watoto wenu kwasababu wote mnauzoefu na pia wazazi wao na ninyi  kama wazazi wa blended family.

 

 Kwasababu tu umeoa mwanamke mpya umpendae, haina maana Watoto wako uliowazaa kabla yake watampenda pia hivyo usiwalazimishe kumpenda na kumuita “Mama”, vilevile haina maana mkeo huyo atapenda mtoto/watoto wako kutoka ujanani/talaka/kifo. Upendo haulazimishwi, waki-click na upendo kuibuka kati yao great, ikitokea hakuna upendo pia poa, muhimu ni kuwa na mipaka na mipaka iyo iwekwe wazi kwa Watoto na kuheshimiwa.


Nitakuona baadae wiki hii. Bai!

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao