Skip to main content

Endelea mtongoza Wife...


Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.

 

Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.

 

 Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka wawili nawaheshimu sana, walikuwa wanazungumzia kuhusu “kuna umri ukifikia mambo kadhaa kwenye ndoa yanakuwa hayana uzito tena, unakuwa unazingatia zaidi  uhakika wa kipato, afya njema na furaha ya familia”, wasingegusia ndoa ningekubaliana nao kuwa kweli baadhi ya marafiki wapenda starehe wanakuwa hawana uzito(unawakwepa), kukaa Baa(au online) baada ya Kazi kila siku kunapoteza thamani(unakunywa ukiwa home(unacheza na wanao).

 

Basi mie na umbeya wangu nikarukia “Convo” nikawauliza inamaana siku hizi hamtongozi wake zenu humo ndoani? Wakachekaa, wakasema huo muda hawana….nikashangaa  hihihihi. Nikawauliza hamuhofii wake zenu kutongozwa huko nje? Kama msemo unavyokwenda, usipompatia nyumbani/ndani, wenzako watakusaidia huko nje.

 

Huenda mkeo hakuambii, ila napenda ujue Kaka yangu mpendwa, Mkeo anahitaji kutongozwa mara kadhaa kwa Mwaka, sio kila siku ila once in a while hasa akiwa kwenye mood mbaya(anakaribia Hedhi)…usimtongoze kama vile ulivyoanzanga miaka 15 iliyopita, mtongoze kulingana na alivyo sasa.

 

Mfuate-fuate(siku hizi ndio mnaita ku-stoku? Unamstokuje mkeo), msumbue kwa kuonyesha mapenzi iwe kwa vitendo au kwa maneno, pia unaweza kumtongoza wakati unamuandaa na wakati tendo linaendelea. Nyumbani(Asili yetu) kuna msemo “ikiwa mumeo hakufuati-fuati kwa maneno kutaka tendo basi ujue kuna tatizo”!

 

Ni muhimu sana kwa mkeo kuona kuwa bado unampenda na kumtamani kama ilivyokuwa awali pamoja na mabadiliko yote aliyopitia kwa sababu yako na kwa ajili yako…you know, Kubeba mimba na kukupa Watoto. Kurudi nyumbani kwa wakati kila siku au kusema “ahsante mke wangu kwa chakula” sometimes haitoshi(sio kila mwanamke anahisi kutakwa sexually kwa kupewa shukrani au kushikwa tako, wengine wanapenda kushawishiwa/tongozwa.

 

Je unaujua Mzunguuko wa Mkeo wa Hedhi na unakabiliana nao vipi mwanzo mpaka mwishoni? Au na wewe unaamua kukaa Kazini/Bar mpaka usiku wa manane halafu unakutana nae mlangoni na Panga? (Natania).

 

 Huo mzunguuko ndio sababu kuu Wanawake na Uongozi is a Scam, we cannot make Big maamuzi bila kuweka Mahisia mbele, kama sio hasira bin visirani au furaha kupitiliza basi  huruma kupitiliza. Wanaume homono zake zipo vilevile, hazibadiliki mara 4 kwa Mwezi kama sisi. Nimetoka kwenye topic, sorry.

 

Takuona wiki ijayo.

Bbai. 

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao