Hello!
Ishi ujifunze au kua uyaone.....kuna wale jamaa(wake kwa waume) huwa wana uzoefu wa kila jambo linalotokea Duniani.
Au wao wanamjua kila mhusika anaepatwa na jambo lolote interesting kwa ubaya au wema. Sijui kuhusu wewe ila mie huwa wananiudhi sana!
Unaweza ibuka unazungumzia habari ya kushtusha kuhusu mtu fulani baada ya kusikia Taarifa ya Habari then "msikilizaji wako" anaanza kukupa historia nzima ya mtu huyo na matokeo yote maishani mwake.
Unamuuliza umejuaje yote hayo mwenzangu? anakuambia "aah niliwa kuishi nae mtaa mmoja" au "mama yake alikuwa mpangaji wetu" nakadhalika!
Haiwezekani umjue kila mtu kwa undani (dont you have life?)lakini inawezekana unajua habari za kila mtu au watu wengi kwasababu ya Umbea au kwasababu unafuatilia sana habari za Kidaku.
Wakati mwingine wewe sio mbea lakini marafiki zako ni wafuatiliaji wazuri wa habari za watu na kukupa "stori".....sasa wewe kujua stori za watu haona maana kuwa unawajua sema unajua habari zao.
Sio mbaya kufuatilia Gossip hasa kwa sisi Wakimama lakini unapoleta "ufahamu" wako kuhusu mtu uliepata habari zake kwenye Magazetibya udaku usijifanye unamjua au uliwahi kuishi nae...mmsema tu umesoma.
Kwa mfano wale wenye "akili" huwa wanasema wamesoma wapi (site gani) au kitabu gani ili nawe uende ukapate Ilimi.
Si unawajua wale wenye "idea" ya mambo mengi tofauti ya Kijamii na hivyo kuyazungumzia kwa urahisi lakini kwa undani....intellectuals (hawa nawapenda) kwasababu najifunza kila wanapoleta Siasa.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments