Wednesday, 27 January 2016

Mtoto wa Kiume vs Wa Kike....

....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi.
Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja).
Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume.  Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika  kuwa huyu Mvulana(mtoto wa Kiume) nae ni Mtoto, hakuzaliwa Mwanaume na kujua kujilinda, hakuzaliwa tu na kuwa Imara,Kujiamini n.k. Huyu Mtoto wa Kiume anajifunza haya mambo kutokanana mazingira yanayomzunguuka lakini zaidi ni jinsi Wazazi wake mnavyomfunza  (kama mfanyavyo kwa mtoto wa kike).

Waharifu/Watu wabaya/Waovu siku zote hutafuta mbinu mpya ili kufanya Ushetani wao, sasa tangu Wazazi tume-relax kwenye Ulinzi kwa Watoto wa Kiume dhidi ya Watu waovu, tumefanya watoto wetu wa Kiume kuwa "easy target"! Kwa maana nyingine tunakuwa Sexit kwa watoto wetu. Umesikia mara ngapi Vijana wa Kiume wa miaka 8-16 wanajiua au wanauwawa kutokana na Unyanywasaji wa "Wavulana" wenzao(wengi ni Wanaume watu wazima aka Pedo).
Kutokana na Era ya "Smart kilakitu", unaweza kusema Malezi yamekuwa rahisi, lakini mimi binafsi naona kuwa Malezi kwa Watoto wa leo ni Magumu kwasababu, ili kuenda sambamba  na Wanao nilazma ujifunze masuala ya "code" na kwenda nao sambamba na Technology....kwa maana hivyo tunarudi "shule" kila siku ili ku-keep up.....juu ya Kazi zako, wajibu wako kama Mzazi kwao, Bills, Majukumu ya Nyumbani  kama Mke/Mume n.k.

Sasa hii "Smart kilakitu" inapendwa zaidi na Watoto wa Kiume, kwasababu naturally wao ni "fixers"  na "Technical" sio (weka Ufeminist kando),  wengi wao wanapenda Games na ku-code, kutengeneza Apps, kujenga TV au PC n.k. wenyewe katika Umri mdogo.
Mara nyingi  yote hayo hupatika kwa urahisi ikiwa Mtoto atakuwa connect Online na huko ndiko hujenga urafiki na "watoto wengine" ambao actually sio wa Umri wake bali ni watu Wazima wanaopenda watoto wadogo wa Kiume(Pedos). Nia yao ni ku-Groom watoto hao na kuwa-abuse na pengine kuwaua au kuwasukuma  wajiue kwa kuwa-troll ili majamaa waendelee kufanya Uhalifu wao.kama ambavyo baadhi ya Wanaume hufanya kwa watoto wa kike ambao luckly tunawalinda zaidi ya wenzao wa Kiume.
Watoto wa Kiume wanahitaji Ulinzi sawia kama wale wa Kike, Watoto wa Kiume wanakuwa Groomed pia. Nimechoka ku-type, naamini umepata Mwanga wa nini hasa nilitaka kusema. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Wednesday, 20 January 2016

Mpenzi akuone uKizaa vs uKinya.....


Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora  Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi.

Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake.Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki).Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni.

Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka "kupumua" toka nje au nenda chumbani/chooni na ubaki huko mpaka harufu iishe au fungua dirisha na jipepee. Hitaji la kujamba huwa haliji unless nipo peke yangu......hihihihi najua, Kipaji hiki.Pamoja nakusema hivyo bado kuna wakati (kwa Wanawake)unaeza kujisaidia(kutokwa na Haja kubwa) wakati wa Kujifungua.....yeah hii haina kuTigOliwa, kuna Wanawake hawajawahi guswa Tigoni na bado ile siku ya siku(Kuzaa) wanaanza na Dinfi(Kinyesi) kwanza......tunaita "safisha njia".


Mama na Bibi yako na Somo yako aliekufunda kamwe hawawezi kukuambia hili(Hongera kwa kuichagua Blog hii sasa unajua).....wao husisitiza kula ushibe ili upate nguvu ya kusukuma pale Uchungu unapoanza hihihihihi ukila Mkimama umekwishaaaaa, lazma ushundi kabla Mtoto hajatoka.

Sisemi usile ila ni muhimu kuepuka vyakula vigumu au vya Wanga unapofikia Wiki ya 39. Kunywa sana Maji na kula Matunda(utaishia kukojoa) usiku kabla ya siku siku unayotarajia kujifungua.....vinginevyo jiachie tu.....kuleta kiumbe  Duniani sio kazi ndogo na hata kama Mpenzi akiona unavyojikamua na Mavi kukutoka sio kwa Kunya bali kuzaa Mwanae si ndio!......haiesabiki!!

Sasa ikiwa na wewe unaamini kuwa Kujisaidia Haja kubwa ni vema Mwenza asijue aunkuona unavyojikamua, usijione wa ajabu au Mpweke. Mie pia naamini hivyo.


Kuna vitu vingine vinapaswabkutoonwa au shuhudiwa, haijalishi mnapendana lwa kiasi gani(kama ni mgonjwa sasa hivyo ni anaza kesi).

Naheshimu nankuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Wednesday, 13 January 2016

Je! Mume huvutiwa na "u-Wife material" wa dada wa kazi?

Heri ya Mwaka Mpya!

.....yanasemwa mengi juu ya Wasichana/Dada wasaidizi wa Kazi na kwanini hasa wengi huchukua "nyumba" na kuacha wenye nyumba(Wake) wakishangaa. Wengi hudhani kuwa shughuli anazozifanya Msaidizi ni shughuli ambazo Mama mwenyewe nyumba (ambae ni wife material) ndio hupaswa kuzifanya. 
Sasa ikitokea Msaidizi anafanya kila kitu kuanzia kuwa "mama" mpaka Usafi wa nyumba na msimamizi wa Bajeti ya Chakula. Msaidizi huyu hana "nguvu"  ya kulalamika, kutoa changamoto au kubishana na wenye nyumba.....hasa Baba. 


Msaidizi huyo siku zote huonyesha Shukurani na Heshima hata pale anapocheleweshewa Malipo(Mvumilivu). Huenda Msaidizi anafanya yote hayo kama sehemu ya Kazi yake, lakini sehemu ya Kazi yake haiji yenyewe. Kila nyumba/familia ina utaratibu wake na Mkuu wa taratibu za nyumbani huwa Mama/Mke. Mama mwenye nyumba ndio humuelekeza Msaidizi afanye nini kwa siku husika......anamwambia afanye yale ambayo anajua Mumewe atafurahi na hatohoji ikiwa atakuta yapo vizuri. Mfano nguo zake kuwa safi na tayari, aina ya chakula/upishi aupendao, usafi wa nyumba n.k.Ni asili ya Mwanadamu wa Kiume(weka Ufeminist wako kando) kwenye Ndoa kujiona "Mwanaume" pale mwanamke anapoonyesha kujali.....eer kwenye malezi ya watoto,  Chakula, kuandaliwa mavazi(fua/nyoosha) kuwepo kwenye Mazingira mazuri/safi.


Ikiwa Msaidizi anafanya kila kitu nyumbani kwako hakika anakuwa "wife Material" kuliko wewe ambae ni Mke, ni rahisi kwa Baba mwenye nyumba kuhamisha hisia.....kumbuka Ndoa sio Uzuri wa Sura, Umbile na Mapenzi pekee! Kuna Mawasiliano, Ushirikiano, Ulevu na mengineyo kibao lakini pia  Uwepo wako wewe kama Mke na kutimiza sehemu ya Majukumu yako anayofanya Msaidizi wenu ndio husimamisha Ndoa.

Kwa wasaidizi wa Kiume kuchukua Nyumba, ni vema ikazungumziwa na Mwanaume. Mie sijui Majukumu ya Mwanaume.....ila najua kuwa Mwanaume anaemsaidia "Mke" kufanya kazi ngumu "za kiume" mfano anaelinda" iwe Getini au Shambani, ajituma kwenye Mapishi, mwenye kuonyesha Heshima, Asiekufokea au kuhoji umetumiaje Pesa, Halalamiki na kuwa available kwa ajili yako is sexy. Hayo pia yanaweza kumvutia Mwanamke Kimapenzi.
Haijalishi.....hata ukijaribu kuleta Msaidizi wa Kike au kiume "mbaya" bado haizuii kwa Mwanadamu kuvutiwa nae ikiwa afanyayo ni mambo ambayo Mke/Mume anadhani ni sababu ya yeye Kuolewa/Kuoa(nani anafunga Ndoa kwasababu ya Uzuri, Mapenzi na Ngono tu? Ndoa ni zaidi ya hayo).
Kama unamsaidizi ni vema usijisahau. Natambua maisha ya leo ni kusaidiana, kwamba sote tunafanya kazi na tunakuwa na muda mdogo wa ku-catch up kama wapenzi na Wazazi. Lakini hii isiwe sababu ya kumuachia Msaidizi afanye kila kitu......ndani ya siku 7 za Wiki tafuta Muda Kuwa Mke na Mama kamili kwa siku mbili.Nafurahi umebarikiwa kuwepo nami 2016, naheshimu na kuthamini Muda wako, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 5 January 2016

Je ni lazima atiki viboksi vyako vyote vya Mr wright?


Mwaka ukianza ila mtu hujitahidi kujiwekea List ya mambo/vitu ambavyo angependa kuvifanya au kufanikisha Mwaka husika. Mimi Binafsi kinachobadilika huwa  ni Namba tu na hivyo Mipango yangu huwa haitegemei Mwanzo wa Mwaka. Naweza kuanza Machi nikafanikisha June au nisifanye lolote la ziada kwa mwaka mzima. Furahia maisha huku ukipiga hatua taratibu bila kujiwekea "dead line"(ndio naamini).Pamoja na kusema hivyo bado siwezi kukataa kuwa sote huwa tuna "aina" ya mtu ambae tungependa kubarikiwa enough na hivyo kuwa  nae na kuchangia yale Mazuri, Mabaya na ya Ovyo maishani na hata kuanzisha Familia pamoja. Tena ukiwa katika umri mdogo (miaka 21-30)hali huwa mbaya ziadi.....unatolea  nje watu kibao kwasababu sio "type" yako. Yaani kwnye viboksi 10 anatick 2 tu!Sikuzaliwa tu nikawa 30+ nilipitia unayopitia wewe, na hakika list yangu ya Mr right ilikuwa ndefu kuliko yako.....na hiyo ndio sababu sina List ya Exes kwasababu nilitaka yeyote atakae "nigusa bega" lazma atick angalau viboksi 15(who is that pafekiti?).Jinsi miaka ilivyozidi kwenda ndivyo ambavyo nilikuwa na kua sio, na hivyo kuelewa kuwa unless najiumbia mwenyewe Mwanaume ninae mtaka, hakuna Mwanadamu atatick viboksi vyote 30 vya nimtakae. Kwenye hiyo list hakukuwa na "lazma awe na kazi au pesa" though(I've got my own....well I used to). Pia nilitaka asietaka Watoto(yep sikutaka kuzaa mie kabsaaa).Nivema  kujiwekea Viwango na Ubora wa mtu umtakae na ujitahidi kuwa na list ndefu ya kutosha ili angalau atick viboksi 5.....list yako itakusaidia kuendelea kusubiri zaidi na hivyo kupata muda wa  kujijua/tambua na kufurahia Maisha yako kama Binti (kwa wanaume sigusi sababu sijui) kabla hujawa Mke wa, Mpenzi wa na baadae Mama wa.
Nikiwa wazi kutoka rohoni, napenda kukuambia kuwa Penzi la kweli hujitokeza mahali popote, Penzi la kweli halijali "list"....ukimdondokea mtu na yeye akakudondokea hakika "list" yako ya "mr wright" haitoleta maana kwako.
Kwa ninyi young Women (and Men am not judging)ambao mnadhani mnayajua sana Mapenzi na mnajua mtakacho out of Uhusiano kwa sababu ya kusoma love quotes kwenye Social media na kuangalia Tv programs, napengine kuvaba few times.....na  sasa mmejiwekea List kwa kuamini kuwa kuna Mr Wright mahali atatick viboksi vyako vyote 20? anza kudhani upya. Kuwa na msimamo na simamia unachoamini lakini usijiwekee limit.....akigonga 5 muhimu kwako  kati ya 10, you are good to go....mengine mtajifunnza mbeleni mkiwa pamoja. Fuata Moyo....usiache akili Nyuma.Ahsante kwa kuichagua Blog hii, Naheshimu na kuthamini Muda wako Mahali hapa.

Babai.