Saturday, 28 May 2016

Kubishana/Fokeana Mbele ya Watoto...


....kuna Ubaya?
Baadhi ya watu wanasema SIO vema kwa Watoto wenu kuwaona mkigombana iwe ni Ugomvi Mkubwa(Pesa za Savings acc zimenda wapi?) au ule mdogo(kwa makusudi hujasafisha Bafu). Nyie huwa hamgombani? Kama hamgombani basi mmoja wenu anaishi "kisiri", ulie nae sio yeye...au mmoja wenu anamuogopa mwenzie.Mie ni that Woman ambae nina Sauti kali/ya juu which is a shame kwasababu huwezi kujua kama ninafoka au ninaongea kawaida, sasa ukitaka kuongea kama mimi ni wazi kuwa Utakuwa unanifokea kitu ambacho kitanikera na hapo moto kuwaka...umeona? hihihihihi nataia!!
Wazazi wengi hujizuia  kuanzisha "Mabishano" mapema na hivyo, husubiri mpaka Watoto watakapokwenda Kulala ndio wanaanza kubisha/fokeana. Nakumbuka wakati nakua Baba na Mama walikuwa wakifokeana Chumbani kwao(wakiamini tumelala) kumbe some of us (Mie) tulikuwa tunaenda kusimama Mlangoni na kuwasikilia ili tujue kama wanabishana/gombana au wanaongea kawaida tu na kama wanagombana, wanagombania nini?....haiwezekani iwe ni mimi tu? hehehehe.
Wakifungua Mlango ghafla najifanya nilikuwa naenda Chooni, nimepotea njia....Sikuwahi kuwaona Wazazi wangu wakifokeana/bishana/gombana mbele yetu, lakini najua kuwa walikuwa wanafokeana time to time.Unapokuwa na Watoto(Mzazi), wakati mwingine inakuwa ngumu "kugombana" na kumaliza Ugomvi kwasababu watoto wanaingilia (huyu anakuja nakuambia anaaka Maziwa, mwingine  hivi na vile)na hivyo kuharibu "ugomvi" na matokeao yake "issue" inabaki inaning'inia. Hii ni moja ya sababu ya Wazazi wengi kusubiri mpaka Watoto walale ndio "wagombane" kwa "uhuru".
Sasa, inasemekana/Aminika kuwa ni vizuri Watoto wakijifunza "real life" kutoka kwa Wazazi wao na hivyo inashauriwa kuwa ni Salama kwa Watoto kuona Baba na Mama wakibishana/gombana kwa Maneno(bila kutumia matusi), kupena nafasi ya kila mmoja wenu kujieleza ili kwa pamoja kufikia Muafaka na kumaliza tofauti zenu zilizosababisha mkwaruzane.Pamoja na kugombana huko hakikisheni kuwa hamdhalilishani kwa kuitana majina Mabaya/Machafu au kutumia Matusi, Watoto ni kama Sponji.....wanachokisikia na kukiona kutoka kwa Wazazi (watu wa kwanza kuwaona, kuwapenda na kuwaamini) "hukinyonya" na kukitunza. Kwao itakuwa ni kawaida kwa sababu Baba na Mama hufanya hivyo pia!Mambo vipi lakini?

Tambua kuwa Nathamini sana Muda wako hapa, Mwambie na Mwenzio. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Friday, 27 May 2016

Je ni Muhimu kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mpenzio....

...just incase? Mie binafsi siwapendi Rafiki zake wote...well sio wote, wapo  ninaowapenda ila Asali wa Moyo hayupo karibu nao so nimebaki na nisio wapenda which means siwapendi WOTE!! anyway...Siku nkaenda shiriki Semina ya Wanandoa Wachanga(mie mepita Miaka Saba so nilienda kama Mzoefu). Dunia ya leo watu wanadanganyana sana aisee. Mke wa Pastor aliedumu kwenye Ndoa kwa Miaka 28, akawa anashauri Wanawake walio Ndoani ambao hawana "uzoefu".Mengi yalisemwa ila lililonigusa ni hili la LAZIMA na MUHIMU sana kuwa karibu na Rafiki wa Mumeo, just incase siku moja mkikorofishana na wewe ukashindwa kuongea moja kwa moja na Mumeo. Kwamba unaenda kwa Rafiki yake/zake na kuwaomba wamfikishie ujumbe....au "Ongea na mwenzio, maana mimi hanielewi" Kweli Mama Pasta? kweli kabisaa??
Huyu ni Mume wangu(najisema kimyomoyo Seminani), tulipokula Kiapo ilikuwa kati yake Yeye, Mimi na Mungu  na tuna-share kila kitu(isipokuwa Miswaki na DNA?) ikiwa kuna issue kati yetu Mama Pasta tunaiweka Issue Mezani, tunazungumza na kufikia muafaka wenyewe na Mungu wetu. Ndoa ni ya Watatu Mama Pasta, Mungu, Mume na Mke, ikitushinda tunaipeleka kwa alietufungisha ndoa, akishindwa(which is rare) basi tunarudi Nyumbani kwa Wazazi.....huko nako ikitokea Sufuri basi tutajaribu Kansela ambae ni Mtaalam na hatujui sote(hatopendelea)....duh! mpaka tufike huko Ndoa itakuwa imekwisha uwawa...mie Mwenyewe Mshauri hihihihihihi!
Hakuna Uhusiano usio yumba, sema miyumbisho inatofautiana. Jambo kubwa kwenye Ndoa yetu huenda ni dogo sana kwenye Ndoa ya Watu wengine. Mfano mie sipendi kutukanwa au kudharauliwa, sasa siku Asali wa Moyo akinitukana au kuonyesha dharau huo utakuwa Mwanzo wa Mwisho wa Ndoa yetu! hii haina Kansela wala Mfungisha ndoa....Kuvumilia? vumilia wewe....mie sijui kuvumilia matusi wala dharau.
Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji na sio lazima kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mkeo ili tu iwe rahisi ikitokea mmepishana/kosana/gombana na mwenzio. Kama ilivyo kwenye Mapenzi, Urafiki/Ukaribu na Mtu  haulazimishwi....ni ku-click au unclick!Kwa wewe ambae hukufundwa na Bibi/Shangazi yako labda (Kama Somo la Sayansikimu, sio muhimu ila inasaidia sana Maishani) na unategemea/amini zaidi Wake wa Mapasta/Wachungaji wakushauri kutokana na "umri mkubwa" wa Ndoa zao. Tambua kuwa Umri wa Ndoa sio kielelezo cha Ndoa Imara yenye Furaha, Upendo na Amani. Wengi hubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine nyingi tu ambazo hazihusiani na Maana wala Lengo la Ndoa.Pia kumbuka kuwa Uzoefu wa Mtu sio mara zote muhimu bali Elimu. Kufundwa ilikuwa ni Elimu  ya Kijadi ya Awali ya kumuandaa Binti Kimaisha(sio kingono pekee kana wengi wanavyofanya siku hizi) atakapokwenda kuwa Mke na Mama.Sijui nyie, lakini jinsi mnavyokuwa pamoja kwenye Ndoa ndivyo ambavyo mnajifunza zaidi kuhusu  mambo mengi kimaisha kama Pea, vilevile inafikiwa mahali mnajikuta hamuendani tena na "marafiki" zenu wa zamani ambao kila mtu "alikuja nao". Mara nyingi mnaachana na baadhi as you grow older na kutengeneza Marafiki Wapya kama Mke na Mume by the time umefikia utu Uzima mnajikuta na Marafiki wa kweli wa chache na wengi wao ni wale mliotengeneza Pamoja kama Wanandoa.
Sikutumi uwafukuze rafiki wa Mumeo ambao labda (kama mie) huwapendi, bali husihisi presha ya kujenga urafiki nao, ila ni muhimu Mumeo aelewe kuwa Humpendi fulani na fulani ili ikiwezekana apunguze kuwaleta kwenu.....you know some watu wana bad energy, ukiwaona tu energy yako na yake zina-crush(weka Smile Emoji)!!"Waheshimu Ndugu na Rafiki wa Mumeo, lakini usirafikiane nao"-Marehemu Bibi yangu Binti Z.K.Waulize Google for me, kwanini hatuna Emojis kwenye Blog via PC ambayo ni Google Product?

Babai.

Monday, 23 May 2016

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo?


Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo.


Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k.Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke!Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi nae...ananiuDhiiii( ndio love___ but don't like___?)....Kizungu sijui, Kiswahili sijui....nipo nipo tu sijui kama naenda au narudi....anyway!Kununa kwako huwa hakuna faida(Machoni mwao) lakini huwa kuna sababu ya Msingi tu kwanini hasa Mkeo/Mumeo kakununia. Unajua unapokuwa kwenye "Ngazi" ya Urafiki na mapenzi ni rahisi kupata nafasi ya "kufikiria" Tusi au kosa/kwazo alilokufanyia Rafikio wa Kiume/Kike....so hata ukinuna utakuwa kwenu na yeye Kwao.Lakini unapokuwa kwenye Ndoa na Mnaishi kwenye "Kanyumba"....Nafasi hiyo hupotea, huwezi kuikimbia Nyumba yako kila mara ambapo Mumeo/Mkeo wako anakuudhi! Mbaya zaidi ikiwa wewe kama Mie hapa, unaishi Ughaibuni....hakuna "kwenu" kule alipo Mama yako ambako ungeweza kwenda na kupumzika kidogo ili kufikiria mpaka Hasira ziishe(Uache kununa) hivyo unaishia kupishana na Mwenza wako bila Jambo wa Habari.Kwa kawaida, Mnapopishana Maneno na kupelekea Mabishano  na labda mmoja wenu hatoi nafasi ya mwingine kujieleza, ili kukunyamazisha....anatupia "tusi" na Maneno mabaya ambayo pengine yataumiza Hisia zako.....Maumivu hayo hukufanya uamini kuwa Mumeo/Mkeo atagundua kuwa amekukwaza/kosea na hivyo atakuomba Msamaha.
Siku inakaribia kuisha na hakuna Msamaha wala Dalili yake.....kinachofuta hapo ni "Kula Bati"....yaani unamnunia....akiwahi kulala wewe una-stay late watching Tv, aki-stay late wewe unaenda kusoma Kitabu. Hakuna kula pamoja wala kupika(kwa Mwanamke kupika ni sehemu ya kupendezwa na mwenza, kama hakupendezi kwa maudhi yake kwanini Umpikie eti?) kwa Wanaume huja na chakula chao au hula Nje(kwanini ale chakula chako wakati hujamuomba msamaha).Sasa kuna watu wameumbwa kusoma wenza wao na kugundua kuwa wamekosea mahali, wengine huuliza "nimekukosea nini Mpenzi, mbona unaonekana haupo sawa" na wengine huwa hawana habari mpaka uwaambie makosa yako(kama vile wewe ni Mzazi kwao). Wengi hasa Wanaume hawajui au niseme Wazito kuomba Msamaha? au Wanaomba Msamaha kwa vitendo?


Haombi msamaha mpaka umwambie amekukosea wapi, which inaondoa uzito wa Msamaha wake.....kwasababu Msamaha mzuri ni ule unaotoka kumoyo bila kulazimishwa au kuambiwa sio ndio?!!Nukta ya Post hii ni hivii.....unapomnunia mwenzio kwasababu amekuudhi sio Utoto na wala sio Ujinga. Ni sehemu muhimu kwako ili kuweza kutuliza Akili na Hisia zako zilizoumia  na kufikiria Kosa(kauli yake chafu iliyo kukwanza) na hivyo kuwakilisha issue Mezani tena katika hali ya Upole lakini Firm.


Fundisha Mwanao umuhimu wa Kuomba radhi/Msamaha, na ikiwa wewe Mzazi umemkosea mwanao usisite kumuomba msamaha, kwani "tufanyayo kwa Vitendo ndio hufanywa/igwa  na Watoto wetu"-Christian Bwaya.


Shukurani kwa Muda wako hapa ambao nauthamini pia Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Baibai.

Tuesday, 3 May 2016

Kurekebisha/Komesha Tabia online, inawezekana?

Habariyo!

Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako).Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu  kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya.Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included.Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatwa na Msiba. Sasa jamaa walikuwa wakiishi kivyao-vyao(hawana habari)na hawakujichanganya na Watz wenzao huko waliko Ughaibuni. Inasemekana walikuwa hawashiriki "Sosho events" za watu soooo walipofikwa na hiyo "life situation". Watu wakaamua kuwafunza "adabu Online".
Mie nilipoambiwa nikawashangaa watoa Adabu. Kwanini mtumie Maumivu ya watu kuwadhalilisha.....sawa nyie ni Watz zaidi yao(Wafiwa wanaishi Kizungu) basi toeni Adabu kiTz, Kijadi. Unakumbuka Utani Msibani? yep watu bado wanafanya haya na tulipofiwa na Mzee(Baba RIP) watani walitutania na kumuigiza marehemu Baba, baadhi unacheka na mengine yanakuongezea Uchungu zaidi.Watani hutumiwa Misibani kufikisha Ujumbe/Funzo/Tia Adabu  "live" uliochanganyikana na Utani, sasa kama alietangulia alikuwa wa kujidai-Pua juu ndio mtajuzwa siku hiyo, Kutokana na Utu Washiriki watakuja Msibai lakini watafanya kwa "utani" vile ambavyo ulikuwa ukifanya kwenye matukio kama hayo kwa wenzako na mwisho kususia "Shughuli" ili kuwafunza  Adabu Waliobaki. Baada ya tukuio kupita utaanza kuona Wanafamilia wakianza "kubadilika" na kuanza kushiriki Matukio ya Kimaisha ya Jamii inayowazunguuka.Hili haliwezi kuhamishiwa Online, unachokifanya Online ni kuiaibisha Familia ya mwenzio kwa kisingizio cha Kufunza tabia. Asilimia 99.9 wahusika hawatosoma/ona na wengi watakaosoma sio wahusika uliowakusudia. Kwa maana nyingine wale uliowakusudia wataendelea na "Uzungu wao" kama kawaida.Mie binafsi sio Mtu ninaependa Mikusanyiko lakini huwa nashiriki kwenye Matukio ambayo nahisi kuwa ni Muhimu kama vile Msiba au Michango kwa ajili kusaidia Matibabu. Kwenye sherehe-sherehe hunikuti.


Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa ni sawa kabisa  kujitenga(kutokuwa mtu wa mikusanyiko) lakini mtu unaemfahamu anapopatwa na Shida ni vema kutafuta muda na kushiriki. Natambua maisha ya Ughaibuni yanabana sana linapokuja suala la Muda(nafasi), Ugumu huongezeka mnapokuwa na Watoto.Lakini ni muhimu kujigawa, hii ita-sound kizungu pia hihihihihihi tupo Uzunguni babu wee hehehehe. Kama ambavyo tunajigawa kwenye maswala mengine ya kimaisha kama vile bills, shopping....mjigawe, nani atakuwa anawakilisha Familia kwenye "life situation" kwenye jamii inayokuzunguuka iwe ni ya Wabongo wenzako au mchanganyiko.


Wakati mwingine sio rahisi kuwepo "live" kwenye tukio kutokana na Umbali wa Jimbo to Jimbo, Mkoa toMkoa, kwa UK ni Nchi na Nchi, basi tumia Simu eeh, shiriki ki-Digital.


Nashukuru na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 2 May 2016

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....


Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)!


Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze!

Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya).
Kuna wakati tulikuwa tukinunua aina Juice ya Matunda"asilia"bila kuongezewa Sukari, maalum kwa Watoto. Matokeo yake (bilakujua) Babuu akawa na Homa zisizokwisha, yaani karibu kila siku Anachemka. Siku moja tulipoenda "Manunuzini" ile Juice haikuwepo in Stock hivyo tukanunua Brand nyingine ambayo ilisema kuwa ni  jutoka kwenye Matunda Halisi aka "Natural" hakuna addictives. Babuu hakuwa na Homa tena. Ziporudi  zile zilizokuwa out of stock tukanunua tele(maana alikuwa akizipenda), Homa zikarudi, hapo ndio nikagundua kuwa Zile Juice zina kitu ambacho sio Salama!Kama Kacha(kawaida, Utamaduni) nikaenda Gugo, na kuuliza sababu ya juice "husika" kusababisha Mtoto kuchemka/Homa. Nikakutana na "Aspartame" ambayo ni Sweetner wanayoweka kwenye Juice kuongeza Utamu badala ya kutumia Sukari ya Kawaida. Na huu ndio ukawa Mwazo wa mimi kuwa "Mlevi"wa Kusoma Ingredient(Vitu walivyotumia kutengeneza Bidhaa husika). Natumia muda mwingi kusoma "ingredient" zaidi ya kulinganisha Bei.Nia ya Post hii ni kukupa mwanga kuwa sio Soda tu zinazoweza kufanya Mtoto "achangamke" sana hata zile Juice laini zinazosema "no Sugar added" zinamadhara kwa Watoto kwa namna tofauti. Mwanangu Homa(naturally ni very active), Wengine wanakuwa too High/Over activeBaada ya Muda nikaja gundua lingine, Mwanangu Hapatani(Allergic) na Karanga au anything Nuts....kuwa na Watoto ujifunze eeh! Tulipiga sana Misele kwa Dermatologist nikaja kugundua Mwenyewe kuwa tatizo ni Karanga(nilizila sana nilipokuwa Mjamzito) na Ngozi yake ni Sensitive na hivyo haitaji Hash Soaps,Lotion etc....hii ni Topic ingine(nikumbushe nikusimulie na nikuambie tunatumia nini ku-keep ngozi safi na yenye afya, no miwasho wala ukavu).


Pamoja na kusema hivyo, usitumie Post hii kama Ushauri wa Daktari, Ikiwa Mwanaoa anaugua Homa mara kwa  mara nenda kwa Daktari kwa Ushauri wa kitibabu na Vipimo/Tiba. Lakini pia ondoa vinjwaji ambavyo sio "Asilia".


Unaweza kutengeneza Juice mwenyewe kutokana kwenye Tunda Fresh. Natambua kuwa kila tulacho siku hizi kina Kemikali(sio natural), lakini mpaka sasa hakuna Issue kiafya inayotokana na Maji ya Matunda kutoka Tunda asilia.


Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa na heshimu na kuthamini Muda wako hapa!

Babai.