Ukiingia kwenye Department stores au Boots (Duka la Dawa na Vipodozi) kubwa kwa sie wa Ulaya hii hapa....unakutana na MUA kwenye "viOSK" vyao wenyewe wamejiremba wamependeza....er kwa mbali!
Asa sinilikuambia tangu nigonge miaka 30....sasa ni 30na nimeanza "kuipenda" ngozi yangu ya usoni! "Mambo ya mwanamke reception".....sasa kama mtu hukujaaliwa "reception" nzuri au kurembeka(mimi) basi angalau Ngozi iwe nzuri na yenye afya kuwapotezea watu "focus".
Mwanamke nimejaribu bidhaa kibawoo za kufanya Uso wangu uwe laini na wenye rangi moja....maana...mmh!
Sijawahi kutumia Mkorogo (na sina mpango huo), sina tatizo na Chunusi (mpaka nile Chocolate), yaani ngozi yangu inakaribia ukawaida tu japo inatoa mafuta ya kutosha kukaangia Vitumbua....anyway!
Nimejaribu skin care nilizokuwa nikitumia miaka ya nyuma in my late 20s, sasa zinadunda, kitu cha uso ama kimekomaa au kimekuwa Sungu (Kisayansi ngozi hupoteza n...