Skip to main content

Posts

Scandals: Binti ajiua kisa B'friend+...Miaka 20 Tangu Secondary!

Hello tena, karibu  tuendelee na "series" sehemu ya maisha yangu ya Shule. Baada ya Muda si watu wakaanza ku-date bana.....unasikia tu gossip kuwa fulani anatoka na fulani, tulipotoka wao walienda kujibanza kwenye ma-bin na kufanya yao. Unaangalia Darasani(wa Asubuhi na Mchana) huoni hata Kijana wa kutoka nae(hakuna anaekuvutia(well mie nilikuwa mdogo Sec, 1st Bf alikuja nilipomaliza Kidatoo cha Nne huko mbele....Team Wasiona haraka. Achana na hili! Kanisa la Mtakatifu Joseph Wanafunzi wa nyuma yangu walikuwa Mapepe sana, na wengi walitokea palepale (Forodhani Msingi) hivyo walikuwa na Mahusiano na Wakaka wa Vidato vya juu  na mmoja wao aliekuwa akipiganisha Wadada wa kila Shule pale Mjini. Aliitwa JJ (sitasema alipokuwa akiishi wala alivyofanana)....alikuwa Mbele yangu Kidato. Huyu jamaa alikuwa napiganisha sana Mabinti wa Msingi na Wale wa Secondari(si unajua kuwa Foronda kuna Msingi na Sekondari eeh). Mwaka wao hawa akina JJ kulikuwa na wakaka "fresh...

Kijinyama/Ngozi kutoka K-ini...

...pengine hujawahi kuambiwa kuhusu hili la "kijinyama", "Kijingozi" lakini lipo na huwatokea wanawake wengi tu, tatizo ni kuwa wengi hawapendi kulizungumzia.....Uanake ni zaidi ya Makeup, Matiti na Kuvaa Magauni na Blauzi. Umewahi kujiswafi na ukakutana na kitu cha ajabu ukaanza kuogopa n a kudhani Kizazi kimetoka(hahahaha) au Mimba imeharibika bilakujua kama ulikuwa  nayo au ukadhani Umelogwa ili upate Hedhi ya Manyama badala ya Damu? Mara nyingi hii hutokea mara tu baada ya Kumaliza Hedhi na kufanya Mapenzi, au pengine umefanya Mapenzi na Mwenza akaenda "mbali" na baada ya kumaliza ukaona Damu na baada ya kujiswafi ukatoa "kijinyama" ambacho hakiterezi kama Ute Mzito au Damu nzito......usiogope hasa kama Umeruka Hedhi. Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke Ukuta wa Mji wa Uzazi(Uterus/Womb) hujijenga kila baada ya siku 23 na baada ya hapo  hung'oka na kuteremka sambamba na Damu pale unapokuwa Hedhini....sasa ikiwa umepitiliza au ...

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!

Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaan...

Siku ya kwanza Kidatoni...Miaka 20 tangu Secondary!

Mwaka huu November inatimia Miaka 20, sasa sio mbaya kama nikiweka kumbukumbu zangu za safari yangu ya Shule kuanzia Msingi mpaka Secondari(intro hiyo hihihihi). Siku ya kwanza naingia kama Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza ili kuwa ngumu maana hakukuwa na mtu nilietoka nae Msingi. Wengi walikuwa wanajigawa kwa makundi kwasababu wanajuana kwa kutoka shule moja ya msingi ama shule zao zilikuwa jirani. Kulikuwa na Wanafunzi kibao kutoka Mlimani Shule ya Msingi, Olympio na Upanga(wajuajiii, mabishoo, Kiingereza kingii). Ikabidi nitafute namna ya kujiunga nao, maana kati yao watakuwa na mimi Darasa moja.....nikaanza kutumia Tiketi ya Kuiba (naongea Kiingereza kwa Nyimbo hihihihihi). Nilikuwa najua nyimbo nyingi ahsante  "Double Compact something Cassete Music system".....unaweka Compact yako halafu unasimamisha ili kuandika mstari wa Wimbo husika. Nilikuwa na "book" full of nyimbo za RnB. Baba(Mungu amrehemu) alikuwa anatununulia hizo eti tujifunze Kiinger...