Skip to main content

Posts

Religious vs Believe in God

Nilikuambia nipo Michezoni Glasgow-Scotigo, basi bwana si nkakutana na jamaa wakaniuliza kama mimi ni Religious, nkasema hapana ila naamini Mungu.....acha washtuke!!! Udini unatutenga, Udini unasababisha watu wasifanye mambo kwa uhuru, Udini hukosesha watu wake/waume wema n.k. Hivi unajua kuwa Dini zililetwa na Wageni ambao sasa ama hawazifuati au wameamua kubadilisha waliotuaminisha kuwa "yaliandikwa" na nani sijui nani. Halafu Waafrika tunaanza kuwaona namna gani vipi hawa jamaa wanatubadilishia Maneno ya kwenye Vitabu vyetu vitakatifu ili kuendana na "maisha" ya sasa! Ama kweli Dunia imefikia mwisho. Tunajipa Moyo na kushikilia Imani zetu tukiamini kuwa ni za kweli na kuponda hao Wageni (Wamagharibi na Waarabu waliotuletea hizo Dini) kuwa ni Wafuasi wa Shetwani. Baada ya wao kuchoshwa na Imani mbili tangu Miaka 2000 iliyopita wengi wao wakaamua ama kuachana nazo au kuanzisha nyingine ili ku-suit maisha yao ya Nyakati hizi. Sasa wewe unapoteza Muda wako wote kuja

Review Undugu wako...

Familia/koo nyingi huwa kuna mtu ambae karibu wote wanaMshuku....wanamuona hatari....kutokana na mambo yake Kiuchumi kuwa safi na kila anachosema basi ni "sheria" au hupewa "umuhimu" au "umakini" hata kama alichosema ni upuuzi! Yaani watu kwenye Familia\Ukoo husika hawaishi kwenda kwa huyo mtu, watoto wake, Mke/Mume wake wote wanapewa attention tofauti na akina nyie Hohehahe. Mtu huyu na Familia yake hufurahia yote hayo na huwa on the look out kuona nani anakuja speed ili kuwa kama yeye au kumpita Kiuchumi....basi akigundua atafanya kila alijualo kuzuia Ndugu (tumbo moja) au Jamaa(ndugu wa mbali wale wa kuunganisha mjomba, binamu etc) asifanikiwe. Umewahi kumpa Ndugu yako wa hivyo idea ya Biashara au Mradi halafu akakukatisha tamaa kisha yeye anaifanya hiyo Biashara au ule mradi ambao alikuambia kuwa huwezi kufanikiwa ukiufanya, kwamba utapoteza pesa tu??.....hihihiihi sasa amka na review Undugu wenu! Mtu

Glasgow 2014....

Siku ya Pili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola, nipo eneo la Tukio kwa Wiki 2....interested?....me neither! Kama umewahi kufanya kazi au kutembelea Jiji la London au NY au hata Dar(City Centres sio Keko sijui Masaki huko, nazungumzia "kiini")....ukija Glasgow bana.....ka' sio Jiji, yaani hakujachamgamka kiviiiiiile(ka' Jiji)..... Ila kuna kama "fun fair" kwa kids(sijui wanaitaje bana), nadhani hiki ndicho kitakachonileta huku mara kwa mara. Michezo imeingiliwa na watu kutoka "Makabatini" bwana, wamefanya watu tushindwe ku-concentrate na Mashindano.....yaani "ukorosho" wao una distract kimtindo....maana wengine tulikuwa tunapenda Mbio na Kuogelea....kuangalia "zile maumbile" za Wakaka pale kati na Miguu (au ni mimi tu nakua pervert wa Kike....hihihihi). Siku hizi bana mtu unajisikia vibaya hata kuangalia mchezaji, akili kama inahamia kwenye akifanyacho private! Kwani lazima watuambie wao wana

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi