Skip to main content

Posts

Mwili ni Mashine....

......inayo-process Kemikali (chakula na mengineyo)....kuna wakati Machine inahitaji "huduma" ili kuendelea ku-process Chemicals ili uendelee kuwepo. Njia pekee ya wewe kujua kuwa Mwili(Mashine) inahitaji " huduma" no mwili huo kukuambia kwa ama kuumwa au kujisikia ovyo/vibaya. Hapa sizungumzii kuumwa Magonjwa ya kuambukizwa na Mbu au Virusi (Mafua, Tetekuwanga au hata HIV)au yale ya kurithi kama Moyo, Kisukari n.k. Kuna watu ambao wanaishi wakitegemea Dawa kusaidia Mashine zao kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu.....kwamba mwili unaposema "mamaa nimechoka nahitaji kupumzika"....mwenye mwili ana pop a Chidonge au Mavidonge. Celebs wanakuambia ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi bila kuchoka (wana pop pills hao).....katika hali halisi mtu huwezi kusafiri kila siku na kufanya shows usichoke! Huwezi ku-pop pills kila siku za maisha yako kwasababu unaongeza Chemicals mwilini na hivyo mwili kufanya kazi ya ziada na hivyo ku-over choka. Nachukua a year o

Bahili, Mchoyo au Mbinafsi...

Heeiyaaa! Shukurani kwa uwepo wako siku ya leo. Watu wa hivyo tunaishi nao lakini kwasababu tunawapenda(Mapenzi upofu) inakuwa ngumu kujua au kutambua. Hawa bwana wanaweza kukufanya uishi maisha ya kiupweke kabisa na huzuni na hivyo kuondoa maana ya Umoja wenu. Sasa leo nataka ujue kiduchu tu. Wale majaa wanaotaka kujua umetumiaje Pesa na wakigundua umetumia senti kwa matumizi yako binafsi ambayo wao (wanaume) wanaamini kuwa sio muhimu wanaanza kung'aka! Wakati mwingine unaona unaongeza mavazi ya watoto ili wapendeze lakini bado mtu anakuambia "mbona wanakila kitu"....Inafikia mahali unaanza kuhisi kama vile unasimangwa na hivyo unaamua kutumia pesa zako. Akiona Pesa anazotoa zinatumika kwa kile anachodhani au kuamini kuwa ni "muhimu" lakini bado unapendeza na watoto wanapata vitu vipya na vizuri mara kwa mara anaacha kutoa Pesa za Matumizi.....huyu ni Bahili! Mchoyo; Mara zote akirudi nyumbani baada ya Kazi....unamuandalia chakula  anakuambia "nilipi

Maisha ya sasa ni kusaidiana...

When it suits them.... Sina uhakika na wenzetu wa Nyumbani ila wengi wetu wa Ughaibuni (wanawake) tunalaliwa na Wanaume tunaoishi nao aka Wenza/Waume. Maisha ya Ughaibuni ni Magumu sana japokuwa upatikanaji wa vitu basic ni rahisi.....kwamba huwezi kuvaa nguo/viatu vilevile au kutumia Friji/Jiko/Kochi lilelile kwa miaka mitatu. Lazima kutakuwa na hitaji la kununua vipya(ni kwasababu ubora wake ni wa chini) lengo la Makampuni mengi nikuwawezesha Wananchi "wa kawaida" kumudu vitu ambavyo vinafanya maisha yao kuwa rahisi(kurahisisha maisha). Au tuseme ni "kiwango cha ubora wa maisha" kwa kila mwananchi kilichowekwa na Serikali.......sasa ukiamua kuibuka na Sumsang Fridge sababu unamudu hakika utakuwa nayo kwa miaka 10 zaidi. Turudi kwenye Kichwa cha Habari; Ughaibuni sote tunafanya kazi (mimi bado ni Temp Mama wa kunyumba)na tuna-share majukumu Kiuchumi  lakini linapokuja suala la majukumu ya kuangalia/kulea watoto tunaambia ni "jukumu la mama". Kwamba

Aah namjua yule....

Hello! Ishi ujifunze au kua uyaone.....kuna wale jamaa(wake kwa waume) huwa wana uzoefu wa kila jambo linalotokea Duniani. Au wao wanamjua kila mhusika anaepatwa na jambo lolote interesting kwa ubaya au wema. Sijui kuhusu wewe ila mie huwa wananiudhi sana! Unaweza ibuka unazungumzia habari ya kushtusha kuhusu mtu fulani baada ya kusikia Taarifa ya Habari then "msikilizaji wako" anaanza kukupa historia nzima ya mtu huyo na matokeo yote maishani mwake. Unamuuliza umejuaje yote hayo mwenzangu? anakuambia "aah niliwa kuishi nae mtaa mmoja" au "mama yake alikuwa mpangaji wetu" nakadhalika! Haiwezekani umjue kila mtu kwa undani (dont you have life?)lakini inawezekana unajua habari za kila mtu au watu wengi kwasababu ya Umbea au kwasababu unafuatilia sana habari za Kidaku. Wakati mwingine wewe sio mbea lakini marafiki zako ni wafuatiliaji wazuri wa habari za watu na kukupa "stori".....sasa wewe kujua stori za watu haona maana kuwa unawajua sema un