Skip to main content

Posts

Knowledge vs Ego....

Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako. Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana. Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!! Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto. Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/K

Ngono ya Usiku mmoja M'ke vs M'me....

...nani Malaya? Hello there. Kwenye harakati za Mpito za Ujana ni wazi unajifunza kwa kufanya mambo mengi kwa kupatia au kukosea. Sio mara zote unakosea ili kujifunza(usifanye makosa makusudi kwa kisingizo cha kujifunza), wakati mwingine unakosea kwa Uzembe(kutokujali). Kama ilivyo kwenye kila kipindi cha  " Mpito" mambo huwa magumu.....wakati mwingine mtu unajikuta unakata tamaa na kuamua kuwa LIWALO NA LIWE na hapo ndio maamuzi ya kizembe yanapojitokeza. Inaweza kuwa Pombe au Utumiaji wa madawa na Ngono Holela au vyote. Inawezekana kabisa kufanya hayo ni katika hali ya kutafuta "amani" au kuondoa "msongamano wa mawazo" na pengine ku-fit in na jamii inayokuzunguuka wakati huo wa Ujana wako. Kwaharaka haraka unaweza kudhani umepata "tiba" lakini katika hali halisi unajiongezea shida/majukumu kabla ya Muda wako. Sasa, kutokana na hali ilivyo siku hizi (Mambo ya Haki sawa sijui Usawa) inafanya mambo mengi ambayo awali yalifanyw

Weusi wa Ngozi sio Uchafu....

....ila usipokuwa muangalifu kwenye kuchagua Rangi za Mavazi/Nywele hakika utaonekana Mchafu(huvutii), hii  haina kujiamini.....nadhani ni muhimu kuchagua Rangi zinazoendana na Rangi ya Ngozi  yako. Mambo?!! Kuna siku nipo na mishughuliko yangu ya ndani wakati Asali wa Moyo anatazama Mashindano ya Tenesi ya Wibledoni. Anapendezwa sana na wale Williams Dadaz....mmoja wao alikuwa anacheza. Mwenyewe anafurahia uchezaji wake (au kuona Tako  kila kisketi chake kinapoinuka hihihihi maana mdada mMashallah). Sina hili wala lile nasikia mwenznagu anawasifia wadada Williams kwa kutokuwa kama Celebs wengine.....mie nkasema hao sio ma-Celeb ni Sports Stars (kwa Kiswahili ndio tunasemaje vile?) ila Media inalazimisha kuwaweka kwenye Kundi la M-aceleb kitu ambacho sio haki kwasababu wapo walipo kutokana na kazi/kujituma kwaoo na sio kuonekana kwenye Tv au kuuza Haidthi kwenye magazeti au....oh well kwa Umalaya. Katika kufunga maelezo yangu nikamalizia na....kiukweli mie siwaelewi

Je Unaogopa Kujaji watu(wenzio)?

Habari yako? Nilikuwa Likizo ya Kiangazi.....katika hali halisi  nilipaswa kukujulisha lakini nikahisi kama vile nitakuwa najionyesha au napitiliza ku-share so nikapiga kimya. Anyway habari kwa ufup,  kama bado unajali ni kwamba Madoa ya Tetekuwanga(Chickenpox) yamepungua Weusi. Ujisedhani hali ya Hewa ya UK inafanya Ngozi kutakata haraka ndugu, nilipewa Mkorogo(andikiwa dawa ya kuondoa Weusi) nitumie kwa Muda wa Wiki 8. Baada ya kugusa Wiki ya Pili nikaona Vijitundu vya ngozi(pores) vinapanuka! Aiiii nikautupilia mbali Mkorogo. Duania ya leo inamengi na kila kukicha tunaongezewa sheria za namna ya Kuishi vizuri au kuishi na watu kwenye jamii. Tunaambiwa tusiwajaji wenzetu kitu ambacho sio rahisi kwa sababu kujaji ni asili ya  mwanadamu, pia bila kujaji hakika utakuwa unafanya maamuzi mambovu na hivyo kuishi ukilalama "kwanini mimi". Nimekwishawahi kukuambia hapa(kwenye blog hii) kuwa mie huwa najaji watu/mtu kama wewe ila tofauti yangu mimi na wewe