Skip to main content

Posts

Sababu Kuu ya Kumchukia Ex wake...

.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni  sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini. Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi). Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) ba

Presha ya kuweka/toa info zako vs Ukarimu....

...enzi za DHB, Yahoo/MSN chatrooms (heeey Maajuza wenzangu hihihihi) ilikuwa ni kawaida kuulizawa upo wapi na unafanya nini au umefikaje huko uliko, wengine wanapitiliza mpaka kwenye unakuja lini Bongo n.k. Kwa baadhi yetu ilikuwa sio big deal kwasababu info hazikuwa muhimu kivile(kabla ya Google haijatufanya Kijiji) kuorodhesha Nasoma, mwaka wa pili  na huwa narudi Home kila Christmas. Jisni siku zilivyozidi kwenda na Maendeleo kuongezeka  na watu wengi kuwa na wasaa wa kufikia Mitandao na hivyo kuweka mengi kuliko wanavyohitajika. Siku hizi imefikia mahali wewe mwenyewe kwa hiyari yako unahisi kusema/share kila kitu, ikitokea mtu kauliza basi unajimwaga kwa uhuru kabisa, which is okay maana info ni zako bwana. Tatizo  ni kwamba wengi mnatoa mengi kuliko mnavyohitajika na matokeo yake baada ya muda wale wale mliowaambia wanatumia hayo kukuumiza au kukudharau. Hakika kila mtu ana haki ya kusema atakacho kuhusu maisha yake Halisi  au ya Kimtandaoni  ili tu awemo anapotaka

Scandals: Binti ajiua kisa B'friend+...Miaka 20 Tangu Secondary!

Hello tena, karibu  tuendelee na "series" sehemu ya maisha yangu ya Shule. Baada ya Muda si watu wakaanza ku-date bana.....unasikia tu gossip kuwa fulani anatoka na fulani, tulipotoka wao walienda kujibanza kwenye ma-bin na kufanya yao. Unaangalia Darasani(wa Asubuhi na Mchana) huoni hata Kijana wa kutoka nae(hakuna anaekuvutia(well mie nilikuwa mdogo Sec, 1st Bf alikuja nilipomaliza Kidatoo cha Nne huko mbele....Team Wasiona haraka. Achana na hili! Kanisa la Mtakatifu Joseph Wanafunzi wa nyuma yangu walikuwa Mapepe sana, na wengi walitokea palepale (Forodhani Msingi) hivyo walikuwa na Mahusiano na Wakaka wa Vidato vya juu  na mmoja wao aliekuwa akipiganisha Wadada wa kila Shule pale Mjini. Aliitwa JJ (sitasema alipokuwa akiishi wala alivyofanana)....alikuwa Mbele yangu Kidato. Huyu jamaa alikuwa napiganisha sana Mabinti wa Msingi na Wale wa Secondari(si unajua kuwa Foronda kuna Msingi na Sekondari eeh). Mwaka wao hawa akina JJ kulikuwa na wakaka "fresh"

Kijinyama/Ngozi kutoka K-ini...

...pengine hujawahi kuambiwa kuhusu hili la "kijinyama", "Kijingozi" lakini lipo na huwatokea wanawake wengi tu, tatizo ni kuwa wengi hawapendi kulizungumzia.....Uanake ni zaidi ya Makeup, Matiti na Kuvaa Magauni na Blauzi. Umewahi kujiswafi na ukakutana na kitu cha ajabu ukaanza kuogopa n a kudhani Kizazi kimetoka(hahahaha) au Mimba imeharibika bilakujua kama ulikuwa  nayo au ukadhani Umelogwa ili upate Hedhi ya Manyama badala ya Damu? Mara nyingi hii hutokea mara tu baada ya Kumaliza Hedhi na kufanya Mapenzi, au pengine umefanya Mapenzi na Mwenza akaenda "mbali" na baada ya kumaliza ukaona Damu na baada ya kujiswafi ukatoa "kijinyama" ambacho hakiterezi kama Ute Mzito au Damu nzito......usiogope hasa kama Umeruka Hedhi. Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke Ukuta wa Mji wa Uzazi(Uterus/Womb) hujijenga kila baada ya siku 23 na baada ya hapo  hung'oka na kuteremka sambamba na Damu pale unapokuwa Hedhini....sasa ikiwa umepitiliza au