Skip to main content

Posts

Kuzuia Mimba au Kupoteza Hamu?

Habari ya sasa! Utasema hee Dinah mbona umeshupalia Topic hizi? Well....ninachoandika hakitobadilisha Maisha ya watu na kuwa Bora zaidi ya yalivyo sasa, lakini naweza kusaidia mtu mmoja kuelewa kwa kiasi kidogo....yule ambae ame-google "kupoteza hamu" kwa mwanamke si eti! Kuna ulalamishi kuwa Dawa za kuzia Mimba(pamoja na matatizo mengine kwa baadhi) husababisha Mwanamke kupoteza hali ya kutaka/tamani Ngono. Hakuma chunguzi ambayo ina-support hili ila Wanawake wengi hulalamikia kuwa Hamu hupungua au hutoweka kabisa mara tu baada ya kuanza kutumia Njia za kuzuia mimba Zenye Homono(hata zisizo na Homono huingilia "hamu" ya mwanamke"). Do I look like I am busy? Ukweli ni kwamba kama hali ya kutaka  Ngono ilikuwa juu au chini basi haitobadilika......isipokuwa utaratibu wa Mwili wako ndio utabadilika na hivyo wewe Mkimama kulazimika kuanza kujifunza upya(wengi huwa hawalijui hili) namna mwili wako unafanya kazi. Tena sio Dawa za kuzuia m

Umuhimu wa Furaha ya Mke....

....wengi huchukulia suala hili juu juu tu, labda hushindwa kuelewa kwasababu Jamii (ikiongozwa na wanawake wenyewe) huwa  hailizungumzii sana kama wazungumziavyo Furaha ya Mume. Furaha ni hitaji la wote lakini nadhani kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwasababu bila furaha kwake ni wazi watoto  na baba mtu hatokuwa na furaha. Pia furaha kwa mwanamke inahusika sana kwenye masuala ya kufanya mapenzi.....kama mwanamke hana furaha ni ama hakutakuwa na Tendo au Tendo halitokuwa la kufurahia na badala yake litakuwa ni la kumaliza haja tu kwa Mwanaume(maliza nilale arrg hihihihi). Wanaume wachache ambao wameshuhudia baba zao wakihakikisha Mama zao wanafuraha mara zote iwezekenavyo, hujitahidi na kuwa hivyo au zaidi kwa wake zao. Hawa hujua namna ya kujali  na kuheshimu hisia za mwanamke. Kwabahati mbaya sehemu kubwa ya Wanaume wamelelewa kwenye Mazingira ya kumuona Mama  ni mtu mmoja mvumilivu, mpole na muelevu.....wakati Baba Mkali na Bingwa wa kudharau. Kwamba Mama anapochoshwa n

Kufutiwa Matokeo Kidato cha 2.....Miaka 20 Tangu Secondary!

Ni Ijumaa nyingine tena ambapo tunaendelea na "Series" yetu. Unakumbuka nilikuambia kuwa pale Shuleni kwangu kwa zamani kulikuwa na Watoto wa watu Wazito na wale wa Mabalozi wa Tz Nje(waliokuwa wanasubiri kupewa Ofisi).....Tulipokuwa Kidato cha Pili kikaja kimtoto kina miaka Nane kilikuwa kinatokea Nchi gani sijui huko. Kilikuwa kinashuka mahisabati kwa Kiingereza hicho hihihihihihi. Aliondoka baada ya Wiki 6. anyway. Kusoma na watoto wa watu wazito ni raha, unapata kujua mambo mengi sana kuhusu maisha yao na(sio muhimu kivile lakini ndio hivyo), unakula maCandy na Majuisi ya Ulaya bana.....hasara yake inakuja kwenye Mitihani, sio siku ya Mitihani bali kwenye Matokeo. Kama unakumbuka mwaka wetu(piga mahisabati mwenyewe) baada ya Matokeo kufutwa(sote tukafaulu) ndio Mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili ukafutwa, sababu zilikuwa nyingi kwanini hakukuwa  na umuhimu wa Kukaa Mtihani wa Kidato cha Pili. Nakumbuka siku tunaenda kuangalia Matokeo(ilikuwa siku ya s

Sababu Kuu ya Kumchukia Ex wake...

.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni  sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini. Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi). Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) ba