Skip to main content

Posts

Ndugu anaposema "ndugu" yake fulani ni attractive....

.....ni kwamba yupo attracted nae. Yaani anavutiwa nae na uwezekano wa yeye kuwa na "wivu" wa Kimapenzi au Kumtaka kimapenzi ni mkubwa. Hawa watu wapo kwenye Jamii na nina uhakika inagusa watu wengi ikiwemo mimi mwenyewe na ndio maana Daima huwa nasema Mjomba/Binamu/Mpwa sio Ndugu wa damu kwasababu hatuchangii Damu kwa asilimia 50 au zaidi(hii haina Usayansi). Kamakawaida nitakupa Mifano au "story" ili kukuburudisha na wakati huohuo kukusaidia unielewe ninaposimamia. Nina wajomba kama most of you, but nilikuwa na Mjomba mmoja(wa mwisho kwa kina Mama) ambae nilimpenda na tulielewana nahisi kwa sababu kiumri tuliendana, kwamba mie nilipokuwa Kidato cha Tatu, Yeye alikuwa Chuoni Mwaka wa Pili. Tulikuwa tunapatana na kwangu mie alikuwa kama "Kaka" mkubwa kabla ya Kaka yangu (wa damu)ambae ndio Kifungua Mimba wetu. Alikuwa akinifunza Hisabati (unajua mie na Hesabu tulivyo) na pia alikuwa akinisimulia Hadithi za Shida, Kuli, Thing fall a part etc(mi

Kristmas mwaka huu ni tofauti....

Yeboyebo hihihihi bado mnatumia hili neno? Wasukuma wa Shinyanga (enzi za Usichana) walikuwa wakisema Yebaaa as in Yeah....."Wananchi Mpo?" "tupo tupo kabisa kwa Jeuri ya Chama yee yee yeebaa". Twende kwenye Krismas sasa. Kwa kawaida mie huwa siandiki kuendana na Nyakati lakini Mwaka huu ni tofauti kwa sababu Waanangu has huyu Mkubwa kanifanya nianze kuipenda na kuifurahia Krismas tena. Miaka 3 nyuma alikuwa Mdogo so hakujali mapambo wala Santa, Mwaka huu anakaribia  miaka 5 na yupo Shule ambako wanafunzwa kama sehemu ya Utamaduni. Babuu akaandika(makorokocho) Barua yake kwa Santa akiorodhesha zawadi aitakayo na akatengeneza na Bahasha kisha kuiweka na kumpa Baba yake akaipost(which he did, huruma kwa postman mkusanya barua hihihi). Sasa kila leo anamzungumzia Santa na kudai atakuwa extra nice na kunisaidia kusafisha(anaacha toys kila kahali) ili Santa asibadili mawazo na hivyo yeye kukosa Zawadi siku ya Krismasi. Walipoanza kupamba Shuleni kwako akaja

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua Update (Bidhaa)....

Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya. Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda. Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi! Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua. Utaratibu wangu Rahisi. Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond. Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo

Tumezaliwa ili tuzae....

....ndio Asali wa Moyo anaamini hivyo, which is Sad really.....but hey mepata topic! Wazazi wako walipoamua kuanza familia nadhani ilikuwa ni maana ya Ndoa, kwamba mtafanya Tendo hilo ili kuzaliana. Nia na dhumuni la Tendo la Ngono ni kuzaliana, kama hutaki kuzaa basi tumia Kinga (usiolewe/usioe) si ndio?!! Kwasisi wa kileo ambao tunabaki Shule kwa muda mrefu, Muda wa kufanya Tendo kwa "haki" (kuzaliana) huwa  sio muhimu, lakini pia sio wote tunaweza kuvumilia mpaka muda ufike...hivyo tunaanza Ngono kabla ya Ndoa nakujikinga "Kizungu" Dhidi ya "kuzaliana". Wazazi kutuzaa sisi ilikuwa uamuzi wao, haikuwa lazima na hakuna aliewalazimisha, sasa kwasababu tu nilizaliwa haina maana na mimi ni lazima nizae. Suala la kuzaa sio rahisi (kwa mwanamke ambae ndio anaezaa)kama ambavyo wengi wanafikiria. Mwili wa Mwanamke ni wa ajabu in a good way, Ukiachilia mbali Athari na Mabadiliko makuu(mengine yanahatarisha uhai) kwa Mwanamke kwa ndani baad