Skip to main content

Ndugu anaposema "ndugu" yake fulani ni attractive....

.....ni kwamba yupo attracted nae. Yaani anavutiwa nae na uwezekano wa yeye kuwa na "wivu" wa Kimapenzi au Kumtaka kimapenzi ni mkubwa.



Hawa watu wapo kwenye Jamii na nina uhakika inagusa watu wengi ikiwemo mimi mwenyewe na ndio maana Daima huwa nasema Mjomba/Binamu/Mpwa sio Ndugu wa damu kwasababu hatuchangii Damu kwa asilimia 50 au zaidi(hii haina Usayansi).




Kamakawaida nitakupa Mifano au "story" ili kukuburudisha na wakati huohuo kukusaidia unielewe ninaposimamia. Nina wajomba kama most of you, but nilikuwa na Mjomba mmoja(wa mwisho kwa kina Mama) ambae nilimpenda na tulielewana nahisi kwa sababu kiumri tuliendana, kwamba mie nilipokuwa Kidato cha Tatu, Yeye alikuwa Chuoni Mwaka wa Pili.



Tulikuwa tunapatana na kwangu mie alikuwa kama "Kaka" mkubwa kabla ya Kaka yangu (wa damu)ambae ndio Kifungua Mimba wetu. Alikuwa akinifunza Hisabati (unajua mie na Hesabu tulivyo) na pia alikuwa akinisimulia Hadithi za Shida, Kuli, Thing fall a part etc(mie sikuwa nasoma hivyo Vitabu). Simulizi hizo ndizo zilizofanya nifanye vema kwenye Lugha heeey(you wonder why sijui kuandika? hihihihihi pole!).



Anyway....siku Moja sasa Bibi akaitisha Kikao cha Wanawake, akasema "Mama Dinah usimuaminii sana Mdogo wako mbele ya Binti yako(mie), Mwanaume ni Mwanaume tu hata kama Binti ni Mpwa wake".  Mama akanipiga marufuku ku-hang na Mjomba.....nkalia kwa uchungu(nilikuwa sielewi kwanini). Nikalalamika nani atanifunza Hesabu na kunisimulia Kuli etc. Kwani hata alijali?!!





FastFooward: Memaliza Kidato cha Nne, sina Boyfriend wala nini (wachelewaji oyeee)....tupo kwa Bibi tukisheherekea Krismasi. Mojomba akatoa Siri kwangu....kwamba alipokuwa Kidato cha Sita alimpa Mimba Binti wa "kataja Kabila la Baba yangu ambalo ndio langu"....akasema "anaumbo kama wewe"....mie sina hili wala lile nachekaaaa! Akanipa stori yote yaani mpaka yale ya ndani ndani(weka emoji ya kushangaa).


Nkasema Hee! Mjomba unaenda mbali sasa, mie sipaswi kuyajua hayo.....nikaingia mtini. Nkaenda kumsimulia Mama, Mama akasema "Huyo ni mdogo wangu sio Ndugu yako, ni mwanaume kama wanaume wengine, kaa mbali nae". Mkimama nkaanza kujitenga.



Kupunguza Urefu wa Hadithi sasa ili nisikuchoshe. Si nkaolewa bwana.....nilipoolewa kuna Wapwa pia na kuna Mpwa mmoja ambae anampenda sana Mjomba wake ambae ndio Mume wangu. Kabla ya hapo (ndoa) Mume wangu walikuwa akimzungumzia yeye tu akati ana wapwa mia na mbili hehehehe. Nkauliza jamani kwanini ni huyu tu utadhani yupo peke yake? kasema sababu anamuona yeye ni cool Ankal kuliko wengine.




Siku anaongea nae kwa kumkanya, mie Nkamwambia hebu Mwache Binti ajifunze mwenyewe, acha kumfuatilia....akasema "unajua ni binti anaevutia sana na nina hofu watu watamchezea"......akanipeleka nilikotoka. Nkajua hii inatokea kwenye Familia nyingi, lakini kwasababu watu hatujui au hatujali.....tunachukulia Poa na kuamini Mabinti zetu kwa Wajomba zao.





Sasa kwa upande wa Asali wa Moyo ilikuwa tofauti, inaelekea Mpwa alikuwa deep kwa Mjomba wake zaidi yangu kwa Mjomba wangu hehehehe. Binti Mpwa akaanza kufananisha uhusianoo wetu na wake, alipojifungua kaboom akamtumia Mjomba wake Picha ananyonyesha.....sio Titi bali titi na Chuchu(toa macho emoji). Nkashanga mnoooooooo! Nkahoji.....nkaambiwa ni "innocent" picha ya mtoto ananyonya. Nkamsamehe kwani ndio katoka Kujifungua....homono kila mahali.



Nawapenda Wapwa wangu....but am a Woman na the oldest is 7 the youngest is Seven months.....Mwisho.


Ahsante kwa Kuichagua Blog hii, nathamini nakuheshimu muda wako hapa!

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao