Skip to main content

Posts

Jinsi ya kutojali.....au niseme jinsi ya kuto-give a damn?

....pengine how not to give a F*ck imekaa vizuri!! najua maana moja tu ya hilo neno F, nakumbuka Mwaka wa Kwanza Chuoni(when I was in London)....Jamaa mmoja alinambia "go f**k yourself" nkamwambia really?can you show me how?.....Darasa likawaka moto kwa kicheko. sasa sijui walikuwa wananicheka mimi(sijui Kiingereza) au jamaa. Achana na hili! Kujali kuhusu kila kitu au mambo ambayo watu wanajaribu kukufanyia na kwanini wanafanya hivyo husababisha maumivu ya Hisia.....unajua ile hisia unayoipata(ulipokuwa mdogo) pale unapomsalimia mtu Mzima halafu haitikii? Unaanza kujiuliza huku "umia" Baba/Mama nanilihu kwanini haitikii "shikamoo yangu"(labda alikuwa anakutaka) but kwa umri wako mdogo unahisi kama vile umenyang'anywa kitu cha thamani kinachoitwa "Heshima kwa wakubwa" ambacho Baba na Mama yako walikufunza. Mie binafsi nilikuwa nalalamika daily Watu Wazima wakinichunia, siku Marehemu Baba akanambia "kama hawaitikii Salam

"Sheria" ya wa Ughaibuni kuwaletea Zawadi/kuwalisha Bata...

....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone? Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa  makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo  mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini. Tandika Sokoni Eti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako. Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuw

Kujua kila Kitu vs Kujua kila situation ya Watu....

....nirahisi kupatwa/kabiliana  na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually. Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia,  mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi. Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofau

Mtoto "anaechagua" Vyakula....

....ndio mnaita "Fussy eater" eti? Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika! Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake. Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed). Ukichanganya Mchuzi au Mbog