Skip to main content

Posts

Mango Vs Red Bull.....Boost Kitandani kwa busy mama wasio na Wasaidizi!

Sio mpenzi wa Soda au Vinjwaji vyovyote vyenye "Sukari" ambayo sio Asilia na mpaka nikaamua kutumia RedBull ili kujiongezea "nguvu" ili niende Sambamba na Asali wa Moyo, basi ujue hali ilikuwa mbaya! Oh nimesahau kusalimia, Habari za Mwezi mzima? ahsante kwa kunitembelea hata kama sijaweka Post. Nashukuru sana. Haya tuendelee;  Unajua unapokuwa na Watoto bana, wanakukamilisha. Kwamba wanakupa "Pure love" tena kwa vitendo(ukaribu, kumbatio,mabusu,kukuambia wewe ni Mzuri), huvuka mipaka na kuanza kuonyesha kujali  na kukusifia umependeza, kukutafuta mara tu ukitoweka(kwenda chooni) n.k....pamoja na hayo yote kuna kitu kinaitwa Ulezi(kazi yako kama Mama).....by the time wanakwenda kulala Mama unakuwa  hoi. Suala la Kufanya Mapenzi na Mumeo umpendae huwa sio Muhimu kiviiiile. Sio kwamba hutaki....la hasha! Bali huna Nguvu. Yaani ile umeingia Chumbani hamu zako zote na "plans" za kuwa Mpenzi ulizo-plan asubuhi zinawekwa pembeni....ile umegus

Jinsi ya kutojali.....au niseme jinsi ya kuto-give a damn?

....pengine how not to give a F*ck imekaa vizuri!! najua maana moja tu ya hilo neno F, nakumbuka Mwaka wa Kwanza Chuoni(when I was in London)....Jamaa mmoja alinambia "go f**k yourself" nkamwambia really?can you show me how?.....Darasa likawaka moto kwa kicheko. sasa sijui walikuwa wananicheka mimi(sijui Kiingereza) au jamaa. Achana na hili! Kujali kuhusu kila kitu au mambo ambayo watu wanajaribu kukufanyia na kwanini wanafanya hivyo husababisha maumivu ya Hisia.....unajua ile hisia unayoipata(ulipokuwa mdogo) pale unapomsalimia mtu Mzima halafu haitikii? Unaanza kujiuliza huku "umia" Baba/Mama nanilihu kwanini haitikii "shikamoo yangu"(labda alikuwa anakutaka) but kwa umri wako mdogo unahisi kama vile umenyang'anywa kitu cha thamani kinachoitwa "Heshima kwa wakubwa" ambacho Baba na Mama yako walikufunza. Mie binafsi nilikuwa nalalamika daily Watu Wazima wakinichunia, siku Marehemu Baba akanambia "kama hawaitikii Salam

"Sheria" ya wa Ughaibuni kuwaletea Zawadi/kuwalisha Bata...

....nani aliiweka? au ndio mambo ya Mgeni karibu wenyeji tupone? Nakubali upatikanaji wa vitu ni rahisi zaidi huku kuliko Tanzania, lakini hiyo haina maana kuwa ukusanyaji(ununuzi na utunzaji) wa  makorokocho(vitu) na kusafirisha ni Rahisi pia! Ukiachilia mbali hilo, pia badhi yetu tunapokuja Nyumbani ni kwa ajili ya mambo  mengine na sio kulishana Bata kwenye sehemu mbalimbali za Kisasa hapo Nchini. Tandika Sokoni Eti wanataka ujisikie kama "upo nyumbani" kwa kukupeleka/tembeza meneo ya "Kisasa" ambako wanauza mavyakula(sumu) na vinywaji kama vya huko utokakao. Ukweli hapa sio wewe, bali wao ndio wantaka kenda kufanya watakayo kwa kutumia Vihela vyako vya huko utokako. Stori time: Nimerudi zangu Bongo na Mwanangu wa kwanza, tena akiwa mchanga(miezi 8). Kiutamaduni ndugu na jamaa hakuna kumshika mtoto "mikono" mitupu si ndio? heeee! Mwanangu kashikwa na Mikoni Milioni na hakuna hata mmoja aliemshikisha "Senti"....well isipokuw

Kujua kila Kitu vs Kujua kila situation ya Watu....

....nirahisi kupatwa/kabiliana  na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually. Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia,  mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi. Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofau