Skip to main content

Posts

"Dayaspora" na Kuzikwa "Nyumbani"...

Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni  "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.  Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil

Jinsi ya kuheshimu Mkeo...

 Kwa kawaida huwezi kutana na Wanawake(Mkeo) akidai kuheshimiwa mpaka labda Mume utoke nje ya Ndoa ambapo uwezekano wa yeye kubaki Ndoani huwa ni  0.01%(that's me)....Hiyo haina maana kuwa Mkeo haitaji Heshima. Jaribu yafautayo kudhihilisha kuwa unaheshimu mkeo vile anavyo/utakavyo akueshimu wewe. Usimuudhi/Umize: Msome Mkeo ili ujue nini anapenda/hapendi Uwanjani na nje ya Uwanja na ujitahidi kutekeleza/kuacha vitu hivyo. Usimfokee/Karipia: Mkeo sio Mwanao/Mdogo wako bali ni mtu mzima mwenzio hata kama umemzidi miaka kadhaa, ongea nae kwa adabu kama Mwenza wako na sio mtu alie chini yako. Msikilize: Pamoja na kua wewe ni Kichwa na Kiongozi wa Familia haina maana kuwa Mkeo hana Sauti humo ndani.  Mkeo ni Mwanadamu na m-treat kama mwanadamu mwenzio ila  sio kwa Usawa (kama Mwanaume mwenzio) na sio kwa kiwango cha chini kama vile hana thamani ya Utu. Usilazimishe Itikadi(mf Ushirikina, Imani, Siasa n.k):   Usijione kuwa wewe  ndio mwenye kutoa Neno la mwisho bila kukuba

Amina wa Ali Kiba adai Talaka Mahakamani na Kiba(2)....

Soma Mosi na Pili hapa .... Tatu, Mtoto anamuhitaji Mama yake full time kwa Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake baada ya hapo PT sio mbaya. Malezi ni Kazi  kama kazi nyingine na inachosha Akili na Mwili, tofauti ni kwamba hakuna Likizo na huwezi kuacha/badilisha na pia kwa  Tz Mke (Mama wa Mtoto) huwa halipwi na hiyo inafanya kuwa "Kazi" hiyo kuonekana kuwa ni rahisi. Mkeo anapoamua au mnapokubaliana kuwa yeye abaki Nyumbani kulea watoto ni jambo zuri na la kuheshimika kwa Ulimwengu wa sasa. Mkeo akigoma kufanya Kazi ya Kulea na kuamua kwenda kufanya kazi/biashara nje ya nyumbani ni wazi kuwa mtahitaji "Mlezi" wa watoto wenu wa hapo nyumbani na yule wa "shule", na atalipwa kwa "rate" nzuri tu kulingana na Kipato/aina ya Maisha mnayoendesha. Wengi kwenye Mitandao wamelichukulia suala la Amina na Kiba kwa kuangalia Kona ya maisha waliyonayo wao kwa sasa, na sio Maisha ya Star Mkubwa mwenye Thamani ya Dollar  Millioni 5(11,570,000,000). Pi

Talaka ya Amina kwa Ali Kiba...

Mimi na wewe hatujui kwa Undani ni kitu gani hasa kilichopelekea wawili hao kufunga Ndoa 2018. Lakini kutokana na Maelezo ya Amina kwenye Hati ya Madai tunajua kuwa Kiba alikuwa Mtesi/Mnyanyasaji kwa Mkewe (Kiakili, Kimwili, na Kisaikolojia)baada ya Miezi 6 ya Ndoa. Kwa maelezo hayo inaonyesha kuwa Amina hakuwa "kipenzi" cha Familia ya Mumewe na hivyo kuhisi kuwa mahali walipo watu hao sio Salama kwake na kwa Watoto na hivyo kurudi kwao Mombasa*. Pia Amina ameongeza kuwa Mumewe(Kiba)ni Muasherati na hakuiheshimu yeye(Amina) wala Ndoa yao(alimdhalili adharani). Amina amedai kiasi cha Laki mbili kwa mwezi(Ksh) kwa ajili ya Matunzo yake na watoto. Madai ambayo yamesababisha Watanzania wa Twita kuhoji... Tu(na)jigunza nini kwenye tukio hilo. Moja, Kwa Msanii mkubwa kama Ali Kiba ambae ana Thamani ya Dollar Millioni 5(568,500,000Ksh) Laki mbili kwa mwezi kwa mahitaji ya Mtoto sio pesa nyingi, pengine haitoshi tukiongeza Ulinzi, Usafiri na Bima ya Afya.  Unalipa Matunzo