Skip to main content

Jinsi ya kuheshimu Mkeo...

 Kwa kawaida huwezi kutana na Wanawake(Mkeo) akidai kuheshimiwa mpaka labda Mume utoke nje ya Ndoa ambapo uwezekano wa yeye kubaki Ndoani huwa ni  0.01%(that's me)....Hiyo haina maana kuwa Mkeo haitaji Heshima. Jaribu yafautayo kudhihilisha kuwa unaheshimu mkeo vile anavyo/utakavyo akueshimu wewe.


Usimuudhi/Umize: Msome Mkeo ili ujue nini anapenda/hapendi Uwanjani na nje ya Uwanja na ujitahidi kutekeleza/kuacha vitu hivyo.



Usimfokee/Karipia: Mkeo sio Mwanao/Mdogo wako bali ni mtu mzima mwenzio hata kama umemzidi miaka kadhaa, ongea nae kwa adabu kama Mwenza wako na sio mtu alie chini yako.


Msikilize: Pamoja na kua wewe ni Kichwa na Kiongozi wa Familia haina maana kuwa Mkeo hana Sauti humo ndani. 


Mkeo ni Mwanadamu na m-treat kama mwanadamu mwenzio ila  sio kwa Usawa (kama Mwanaume mwenzio) na sio kwa kiwango cha chini kama vile hana thamani ya Utu.




Usilazimishe Itikadi(mf Ushirikina, Imani, Siasa n.k):  Usijione kuwa wewe  ndio mwenye kutoa Neno la mwisho bila kukubaliana Mkeo. Ndoa ni ya wawili hivyo ni Muhimu kuweka Mada mezani ijadiliwe na kukubaliana/kutokubaliana.



Uwazi bin Ukweli: Ndoa haina siri...siri za familia yako baki nazo, ila wewe na Mkeo hampaswi kuwa na Siri miongoni mwenu. Achana na "mambo ya kiume hutakiwi kujua", Mkeo anatakiwa kujua Kila kitu kuhusu wewe na uyafanyayo.


Usimzungumzie vibaya; kwa watu baki (online)hata kama ni rafiki ndugu au jamaa. Haijalishi amekuudhi kiasi gani na unahasira vipi!  Usitumie jina baya kumuwakilisha Mkeo.


 Jitahidi kutumia "Mke wangu" zaidi kuliko Mama watoto hasa kama ulizaa(ga) kabla yake(Mama mtoto/watoto linaondoa Heshima ya Ndoa kwa Mkeo).


Usitoke nje ya uhusiano wenu Kiakili  Kihisia au Kimwili:  "Social media" imefanya watu kudhani kumsaliti Mwenza ni pale tu unapofanya Tendo Kimwili(busy, shika, jigijika n.k)



Ukaribu unaokua nao na watu/mtu online with pic bin video na sauti ni sawa na kuwa nae/o Kimwili ila inaenda ndani zaidi Kisaikolojia na kubaki na wewe kwa muda mrefu kuliko tendo la dk 45. Kwenye  Jinsi ya kumheshimu Mume  ongezea hili.



Epuka taarifa baada ya maamuzi: Zungumza nae kuhusu jambo ambalo unataka kwenda kufanya kabla ya maamuzi(isipokuwa kama ni "sapuraizi").



Usimshushe mbele ya Watoto/Adharani: Kama amekosea na kuna hitaji la kumkosoa/rekebisha, ni vema kusubiri muda ambao mtakua peke yenu na kuwakilisha Hoja yako. 


Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao