Skip to main content

Posts

How is life as a mother to a third child (Maisha yakoje kama mama kwa mtoto wa Tatu)?

  Hello, jambo? Baada ya  kichwa cha habari hapo basi umejisema " watu wana watoto 7 na huoni wakitusimulia kuhusu maisha yao", labda hawana muda kama mimi au dada wa kazi ndio anawalea(atakusimulia aliyosimuliwa na dada wa kazi ambae ndio mlezi wa watoto)? achana na hili. Kiujumla maisha kama full time mother kwa watoto 3 chini ya miaka 15 ni magumu kwasababu watoto bado wanakutegemea kwa kiasi kikubwa  ila tegemeo ni tofauti na walivyokuwa wadogo(chini ya miaka 5). Pamoja na ugumu huo bado ukiwaangalia unahisi baraka ya kupata nafasi ya kulea, kukuza, kulemikisha na ku-shape vema wanadamu wengine kwa ajili ya manufaa ya Jamii. Wanao wanapokuwa nje ya nyumbani na wanaonyesha tabia njema, wasikivu, wanajiamini(sio kupita kiasi) na wenye wema ni wazi kuwa wanafanya maisha ya watu wengine kama vile walimu, marafiki zao kuwa rahisi na pengine yenye "furaha" na hata kuwafanya waendelee kutaka kuwa marafiki zao au (walimu) kutokuwa na hasira(maana kazi yao ni kama yangu

Mambo 10 kuhusu Ujauzito hakuna mtu atakuambia....

 ...isipokuwa mimi! Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo. Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa.   Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe.  Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....ha

Mambo 7 Mumeo angependa umfanyie, ila...

...anaogopa kukuambia. Heri ya Mwaka mpya 2023 kwanza, leo google wamenitumia "data" bana, wanasema mwezi wa january kumekuwa na watu Laki nane na Eflu 11(8.11K) wametembelea Blog hii....nikasema Mayooo wane nimezeeka! nilikuwa napata idadi hiyo kwa Siku😅anyways, kama wewe ni mmoja wao basi nasema ahsante sana. Naendeleaje bila twita kwa Miezi 7? Vema kabisa, ahsante kwa kujali. nimegundua kuwa nina Muda mwingi sana wa kufanya mambo mengine muhimu kwa ajili ya afya ya Akili yangu. Ila baada ya kugusa miezi 4 hali ilianza kuwa ngumu nikawa nawakumbuka wote ambao tulikuwa tunabadilishana twiti mara kwa mara nikataka kushusha App, nikapata nguvu za kughaili, nikashida.  Vipi Mumeo na wanenu 3? Bado tumeshikiliana kwa mapenzi ya dhati, wanetu wanaendelea vema pia shukurani. Sema nini gharama na uhitaji wa kugawa "attention" kwa individual's umri na mahitaji yao Kiakili, Elimu, Malezi na "daily Activities" yameongezeka hyuuu!! Ila kwenye mambo mengine wan

Namna ya Kumshukuru Mumeo bila kusema "Ahsante".

Ukiachilia mbali(naipenda hii msemo) kuwa Ahsante ni "common" kitu ambacho kinaondoa uzito na maana yake, pia neno hilo ni rahisi na kila mtu anaweza kuambiwa bila kumaanisha. Mumeo sio mmoja ya hao watu, Mumeo ana umuhimu na uzito tofauti na watu wengine wote Maishani mwako(ukute ni mimi tu ndio nahisi hivyo).   Sasa kuanzia leo acha kukimbilia Ahsante kwenye kila jambo analokufanyia kama Mkewe na mlezi wa Familia(watoto wenu) yake.  Moja, Wakati mwingine mpikie/andalie chakula/kinywaji anachokipenda. Mpokee kama vile wanao wanavyompokea(bila kusema babaaa)....hiyo Pili. Shikamaneni hivi ktk Ndoa. Tatu, akikuudhi au ukiudhika na mambo mengine(unakaribia Hedhi) usimfanye alipe, hasa pale anapofika Nyumbani kutoka Kazini. Jaribu kumjulia hali, kumuacha apumzike na kisha ongea nae vizuri na kwa upendo/heshima. Nne, Ilinde Ndoa yenu pale ambapo mambo yqmegona kuendi vema, mfano Kapoteza Kazi/Tenda/Biashara imabuma, badala ya kumpa Moyo, Matumaini na Ushirikiano....we