Skip to main content

Namna ya Kumshukuru Mumeo bila kusema "Ahsante".

Ukiachilia mbali(naipenda hii msemo) kuwa Ahsante ni "common" kitu ambacho kinaondoa uzito na maana yake, pia neno hilo ni rahisi na kila mtu anaweza kuambiwa bila kumaanisha.


Mumeo sio mmoja ya hao watu, Mumeo ana umuhimu na uzito tofauti na watu wengine wote Maishani mwako(ukute ni mimi tu ndio nahisi hivyo).

 
Sasa kuanzia leo acha kukimbilia Ahsante kwenye kila jambo analokufanyia kama Mkewe na mlezi wa Familia(watoto wenu) yake. 


Moja, Wakati mwingine mpikie/andalie chakula/kinywaji anachokipenda.

Mpokee kama vile wanao wanavyompokea(bila kusema babaaa)....hiyo Pili.
Shikamaneni hivi ktk Ndoa.


Tatu, akikuudhi au ukiudhika na mambo mengine(unakaribia Hedhi) usimfanye alipe, hasa pale anapofika Nyumbani kutoka Kazini. Jaribu kumjulia hali, kumuacha apumzike na kisha ongea nae vizuri na kwa upendo/heshima.


Nne, Ilinde Ndoa yenu pale ambapo mambo yqmegona kuendi vema, mfano Kapoteza Kazi/Tenda/Biashara imabuma, badala ya kumpa Moyo, Matumaini na Ushirikiano....wewe unakimbilia kumpa suluhisho la wapi akatafute Kazi au "usijali kazi yangu itatulisha" na kuchukua nafasi yake au kumshutumu na kutishia kurudi kwenu(kuondoka).


Huo ni Wakati mgumu zaidi kwake kama Mwanaume hivyo wewe kama Mwenza wake unapaswa kumtuliza, mpa Moyo, Matumaini, Ushirikiano na Uhakika wa wewe kuendelea kusimama nae na kwamba unamuamini kuwa anaweza kurudi alipokuwa.


Baadhi hata hufikia mahali wanafananisha mafanikio ya Marafiki zao na anguko la Wenza wao. Ukiondoa anguko hilo la kiuchumi kabla, Mumeo alijitoa na anaendelea kujitoa kwa ajili yako na Watoto. Hivyo onyesha shukurani kwa kulinda Uhusiano wenu.


Kwa Mwanaume mwema, kuyumbika  kiuchumi ni Mzigo mkubwa sana unaokuja na Mwazo, Hofu na Uanaume wake kutetereka. Hali itakayomfanya ahisi kutoweza kuilinda na kuitubza Familia yake.


Hivyo wewe kama Mkewe unatakiwa kulinda Ndoa yenu, ili apate kujiamini nanhivyo kupata nguvu ya kufikiri, kusimama tena na kufanya awezalo ili kurudisha hali ya Uchumi kama ilivyokuwa awali na hata zaidi.


Tambua kwamba Muda wako hapa unathamani sana kwangu.
Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao