Skip to main content

Posts

Huge Microphones na yupo youtube...Kero zangu.

...ndio mnaita podcasts?  wameharibu youtube eti, au nimezeeka niachane nayo kama nilivyoiacha twita? Anyways, hujambo? Unaendeleaje na u-pre-menopause? Kama binadamu hakika kuna vitu vinakukera, binafsi nakwerwa na sehemu kubwa ya jamii ya online, hasa mamilionea na wamarekani weusi wanaoijua Afrika na kacha zake zote (nchi 57?) baada ya kwenda Ghana kwa wiki moja wa youtube na mi-microphone yao makubwa ka' wapo Mawingu FM. Halafu usinikumbushe wale wanajipanga kwenye vibox(zoom meetings) wanaanza kubishana oh my days.,,,ukute ni wivu wangu tu, maana  wanangu wakienda shule na Baba yako Kazini nabaki hapa sina hili wala lile. Ukiachana na hao kuna wale young single men and women wanashauri/fundisha wenzao namna ya kuishi maisha ya ndoa(Well I did that when I was younger but kama unakumbuka nilishauri kuhusu mahusino na ngono nilikuwa in one na was doing it). Najua unatambua kua sio tu Ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, pia Ndoa sio mahusiano japokuwa mahusiano ni sehemu ya ndoa. N

Kutoa ushauri wa Mapenzi, Ngono na Ndoa...Elimu, Uzoefu na Mazingira vinatosha?

  Za leo? Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.   Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani   kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi   mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa. Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana   kutoka kwa mtu na mtu na kutoa matokeo t

How is life as a mother to a third child (Maisha yakoje kama mama kwa mtoto wa Tatu)?

  Hello, jambo? Baada ya  kichwa cha habari hapo basi umejisema " watu wana watoto 7 na huoni wakitusimulia kuhusu maisha yao", labda hawana muda kama mimi au dada wa kazi ndio anawalea(atakusimulia aliyosimuliwa na dada wa kazi ambae ndio mlezi wa watoto)? achana na hili. Kiujumla maisha kama full time mother kwa watoto 3 chini ya miaka 15 ni magumu kwasababu watoto bado wanakutegemea kwa kiasi kikubwa  ila tegemeo ni tofauti na walivyokuwa wadogo(chini ya miaka 5). Pamoja na ugumu huo bado ukiwaangalia unahisi baraka ya kupata nafasi ya kulea, kukuza, kulemikisha na ku-shape vema wanadamu wengine kwa ajili ya manufaa ya Jamii. Wanao wanapokuwa nje ya nyumbani na wanaonyesha tabia njema, wasikivu, wanajiamini(sio kupita kiasi) na wenye wema ni wazi kuwa wanafanya maisha ya watu wengine kama vile walimu, marafiki zao kuwa rahisi na pengine yenye "furaha" na hata kuwafanya waendelee kutaka kuwa marafiki zao au (walimu) kutokuwa na hasira(maana kazi yao ni kama yangu

Mambo 10 kuhusu Ujauzito hakuna mtu atakuambia....

 ...isipokuwa mimi! Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo. Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa.   Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe.  Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....ha