Skip to main content

Posts

Chochote ukijuacho/ulichopitia make money out of it...

 ...uza uzoefu wako iwe wa mapenzi, magonjwa, uzazi, matatizo ya familia au hata disoders na matatizo ya akili! Mie sikujua kama kuwa home body(which I am) ina jina lake na kuna watu wanatoa "courses" kuwafunza wenzao ambao nao ni introverts(hawapendi watu wala kujichanganya nao kwa zaidi ya lisaa limoja) namna ya kuondokana na hali hiyo. Hakuna mtu anaweza kubadilisha vile ambavyo umeumbwa....kuwa mwenye aibu, mapole, mkali, mtembezi, mpenda ku-party, usiopenda ku-party n.k. binadamu tunatofautiana na that is okay. Sio sahihi kutumia "kipaji" ambacho honestly huna na hata kama unacho sio muhimu na hakina faida kwa yeynote Duniani halafu ukaanzisha Kozi ili uweze kuwa tajiri, kwanza kwanini unataka kuwa tajiri? na ikiwa kuwa tajiri ni rahisi hivyo kwanini wengi wetu sio matajiri? Kuna ubaya gani kuingiza kiasi cha kutosha kuendesha maisha na kufurahia Holiday na kumaliza matizo yako ya kifedha mwenyewe bila kuwa tajiri? you know, kufanya kazi na biashara pembeni kih

Mind your Ughaibuni business...

 Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae. Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania  wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini  Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heathcare

Kila Familia/Ukoo ina mtu huyu...

  ...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama  ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(ina

Mtoto wa kambo...part 2.

Mtoto wa kambo...part 2. Ukiachana na misukosuko ya txt na simu za mama mtoto, kuna suala la kufanya mapenzi ambalo wengi huwa hawalizungumzii sababu wanaogopa kuambiwa hawajiamini. Unless wewe una-elements za kichawi au zile za ukimada ndio utaweza kuwa na a very good sex life on the daily (kila anapowasiliana na mkimama wake wa awali kabla yako, unapata mhamko).   Vinginevyo bana the thought of dudu kuingia kwa mwanamke mwingine bila kinga itakuondolea hamu na ile desire kwa mpenzi wako inatoweka, unaanza kujiambia “omg nimekosea kuchagua”, kama umeshawi humuona ex unaanza kujiuliza kama jamaa ana type na wewe umefanana na Ex wake, unapata kinyaa…unawaza “niingie mitini nini?”, unaendelea kuwaza “yaani ndio nimejitolea mhanga maisha yangu yote yatakuwa kupambana na drama za ex”, “si bora niwe single and happy” …yaani akili haitulii. Na kama ujuavyo bila akili kutulia, hakuna ushirikiano na bila ushirikiano tendo hakuna, ukifanya linakuwa doro.     Kwa uzoefu wangu na wenetu wat