...uza uzoefu wako iwe wa mapenzi, magonjwa, uzazi, matatizo ya familia au hata disoders na matatizo ya akili! Mie sikujua kama kuwa home body(which I am) ina jina lake na kuna watu wanatoa "courses" kuwafunza wenzao ambao nao ni introverts(hawapendi watu wala kujichanganya nao kwa zaidi ya lisaa limoja) namna ya kuondokana na hali hiyo. Hakuna mtu anaweza kubadilisha vile ambavyo umeumbwa....kuwa mwenye aibu, mapole, mkali, mtembezi, mpenda ku-party, usiopenda ku-party n.k. binadamu tunatofautiana na that is okay.
Sio sahihi kutumia "kipaji" ambacho honestly huna na hata kama unacho sio muhimu na hakina faida kwa yeynote Duniani halafu ukaanzisha Kozi ili uweze kuwa tajiri, kwanza kwanini unataka kuwa tajiri? na ikiwa kuwa tajiri ni rahisi hivyo kwanini wengi wetu sio matajiri? Kuna ubaya gani kuingiza kiasi cha kutosha kuendesha maisha na kufurahia Holiday na kumaliza matizo yako ya kifedha mwenyewe bila kuwa tajiri? you know, kufanya kazi na biashara pembeni kihalali sio kwa kutumia u-expert ambao unajua kabisa huna kuuza kwa bei ghali?
Nakumbuka kuna Dada mmoja (Twita obviously) siku akaja na somo la namna ya kujua/gundua Old money na new money, wakati ukimuangalia tu anaonekana sio old money na anatumia platform hiyo ili kuuza kozi, kukuza brand ili akawe new money. Old money huwa hawanaga kelele na huezi mkuta online akifunza watu tofauti yake na sisi no money, old money utamjua tu kwa fashion ambao mara zote sio trendy, jinsi anavyoongea na anavyojichanganya na watu ambao kwa kiasi kikubwa ni old money wenzie ambao hawapo kwenye social media.
Hii new money na old money trendy imechanganya kweli kweli mwaka huu, kila mtu anataka kuonekana kuwa yeye ni old money lakini anafanya hivyo kwenye social media ili aingize pesa kupitia big brands sponsorship na google adsense.
Skia, hakuna ubaya kutoa uzoefu wako bure kuelimisha wengine wanaohitaji kama hobi au tufanye Sadaka. Sio kila ukijuacho lazima kikuingizie pesa, acha uroho, acha uongo na acha kuishi maisha ambayo hayaendani na kipato chako. Badilisha career, au rudi shule ukiwa na Kazi uliyonayo ili kuboresha ujuzi wako na kuendelea kusaka pesa kihalali na sio kwa uongo via google, nakuona wewe hapo medical school kid unajiita Doctor, akati ndio kwanza upo mwaka wa pili. too personal?
Haya basi, nikutakie siku njema. Bai!
Comments