Skip to main content

Mtoto wa kambo(part 1)...

Mtoto wa kambo sehemu ya kwanza....

Kambo maana yake nini? Ikiwa mtoto alizaliwa nje au kabla ya ndoa nae anaitwa mtoto wa kambo? au ni kwa wale waliozaliwa ndoani halafu  ndoa ikafeli au mzazi mmoja kafariki halafu  baba/mama kaoa/olewa tena?  Mnaona mlivyo haribu/changanya mambo baada ya kuua umuhimu wa ndoa na kujenga familia? Mtoto kabla na nje ya ndoa (Wanaharamu) huwa hawajulikani/hawana umuhimu(kwa Waislamu hii bado imesimama). Nimekukwaza? ndio ukubwa huo.😁


Mama/baba wa kambo inatumika zaidi Mikoani, huku kwetu Pwani tunatumia sana Mtoto wa kufikia(kwamba umefika  kimapenzi kwa mwanamke/mwanaume ukamkuta mtoto kutoka ndoa iliyopita?)…sina uhakia. Nitatumia maneno mtoto na watoto interchangeably.


Nani alipitisha sheria ya kulazimisha watu wawapende watoto waliowakuta kwa watu waliowadondokea kimapenzi? Yaani ukionyesha huna habari na uzao wa mwanamke/mwanaume kabla yako basi unaitwa Mwanga, unaroho mbaya n.k. Utapendaje mtu wala humjui na hana faida kwako? Natambua kuna msemo mashuhuri wa "ukipenda bonga basi upende na Ua lake, sidhani kama walimaanisha watoto, bali  wazazi….maana kabla ya boga kuna Shina (baba), Majani(mama) kisha maua(Womb) theeen Boga(mtoto). Pamoja na kusema hivyo bado upendo haulazimishwi, unaweza kumpenda mtu na hata mkafunga ndoa lakini wazazi wake wakakakuchukia…unaanzaje kupenda wazazi wa mkeo/mumeo ambao hawakupendi? 


Linapokuja suala la mtoto wako uliemzaa kabla hamjakutana na mpenzi wako mpya, msemo wa "ukipenda boga penda na ua lake" hauna
  mashiko kwasababu boga(mtoto) ni wewe na kwenye msemo hatujaambiwa kupenda mbegu za boga(watoto wako) bali ua lake(mama yako). Kumlazimisha mtu baki kumpenda mtoto ambae alipatikana baada ya wewe kumuingilia/ingiliwa na mama/baba yake inaeza kuwa Mzigo mzito kiakili na kihisia kwa mtu huyo baki ambae ni mpenzi wako mpya.

 

 Uhusiano unapoanza na mwenzio akakuambia ana mtoto(kama ni mmoja, zaidi ya hapo good luck), katika hali halisi utaulizia uhusiano wake na Mama mtoto uliisha lini na mtoto husika upoje(mara nyingi wanadanganya kuhusu uhusiano wao kabla na baada ya mtoto/watoto) ili wasikutishe, ila kwa wanawake wengi wakijua mtoto yupo kwa mama yake na hawana uhusiano/wanachukiana kwa angalau miaka miwili huwa inapunguza “uoga”  na wanakubali kuendelea  na uhusiano mpya.  Kwa upande wa mwanaume sina uzoefu ikiwa uliemdondokea ana mtoto, kwa maana hiyo leo nitaegemea Zaidi upande wa Mwanamke ambae ni childless anakutana na mwanaume mwenye Mtoto/Watoto.

 

Kama mwanamke ambae umekwepa kushika mimba usichana wako wote,  sio haki kwako kuingia kwenye uhusiano na mtu akiwa tayari ana mtoto, Tumaini na chaguo la kwanza kwako ni kuwa na mwanaume  ambae hana uzoefu na watoto ili muanze kuwa wazazi pamoja katika Ndoa. Ukisha jua “situation” ipoje kati ya mwanaume uliemdondokea kimapenzi na mwanamke alie zaa nae (mtoto mmoja tu) anakuwa chaguo la pili na la mwisho ni kuwa na Kibabu mwenye watoto wenye umri kama wako(wanajitegemea na wana familia zao hivyo hakuna Drama kutoka kwa mama yao au wao wenyewe). Zaidi ya hapo wewe utakuwa una elements za uchawi, upo desparate(umekata tamaa na hujipendi) yaani unamkubali Mkibaba ana watotot 4 kutoka mama 3 tofauti na wote wapo chini ya miaka 20 hehehehe NO!

 

 Ukiwa nje, unatazama ndani ni rahisi kusema “kama unampenda bakari basi lazima upende wanae, kama hupendi wanae basi achana nae” ...lakini ukiwa ndani ya situation hali ni tofauti. Sio rahisi kumpenda mtoto ambae humjui(hujawahi kuishi nae, hujamlea, humjui), upenzi haulazimishwi….upendo unakuzwa kulingana na matendo ya pande zote mbili. Sababbu tu yeye ni mtoto haina maana basi anapendwa automatically…. ukute hata baba yake hana upendo isipokuwa anahisi hatia moyoni na pia anatimiza tu wajibu wake kama Baba (huwezi kumpenda mtoto halafu umchukie mama yake).

 

 Kuna drama za Mama yake iwe ni wazi anahitaji kuongea na mzazi mwenzie sababu ya  mtoto au anafanya makusudi ili wewe na mzazi mwenzie mgombane(lazma mtazozana) akijua kuwa atatetewa sababu ana “connection” ya kudumu na huyo mkibaba na wewe huna(huu ndio muda wa kuongeza mipaka, kama hukuweka tangu mwanzo iweke sasa na kuhakikisha inaheshimiwa na Mpenzi wako ambae ni mzazi mwenzie yule dada).


Nitakuona sometime wiki hii kwa part 2.

Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao