Skip to main content

Asking for money, mmepoteza aibu online?

Majuzi nilikuwa nakatiza mitaa ya YouTube  nikitafuta best  Female TV talk show Bongo Tanzania baada ya kukumbuka enzi nikiwa msichana kulikuwa na kipichi cha wanawake, siku mbuki jina wala Host wake ila Jaquline Ntuyabaliwe (sasa Mrs Mengi) alikuwa mshiriki, ilidumu kama episodes 3 hivi(kila Ijumaa/Jumamosi)..unfortunately sikupata nilichokuwa natafuta ila  nikakutana na podcast/Youtube Channel ya Salama, nikawa nasikiliza mazungumzo na mgeni wake, which was quite interesting then kwa chini I saw there were kijibango anaomba "kuchangiwa" as in donate to the channel/podcast, I thought these people have no mshipa wa aibu. 



Am used to other youtubers asking for money or as they demand "cash Up me:, "donate first ndio nitaanza kuongea", "join my channel  for elfu 3(£1) kwa mwezi to get exclusive"...but Dada si Muajiliwa kule Sekta ya private which they pay better than Serikalini...No? au mazungumzo yake na Mastar ni side haso? 






Huwa najiuliza, I (you) subscribed to a few youtube channels, say 25 na they all ask for £5 a month depends on how popular they are and their Content quality na juu ya hapo nalipia YouTube  premium(I don't) family plan £18 which makes £143, so nikulipe wewe pound  5 per month kwasababu unabwabwaja ubeya wa wasanii, showing your beautiful life style or whatever you do in front of a Microphone baada ku research your ( kuokoteza) info which I can do that myself if I want? No.  ila ukute ni wewe na mimi tu ndio we ain't got money so wivu unatusumbua ndio maana hatutaki kulipia memberships.


Sababu ni nini?

Sijui maana mie sio mtaalamu, ila imefika mahali sasa naamini kuwa social media imefanya watu wapoteze haiba na values zao, kwamba ime desensitised watu na hivyo they don't have shame anymore. Sio shame tu hata ile huruma(Utu) ilibaki kiasi hakuna tena. Kuna mtu alisema Social midea imejaa psychopaths au inafunza watu kuwa self-centred na u-psychopath(sio wote wanazaliwa hivyo, sometimes malezi na mzingira yanaweza kukubadilisha/athiri). Maisha yako ya online ni sehemu ya mazingira yako.



Kwanini imekuwa rahisi kwa watu kuomba-omba online?

1-Muibuko wa "influencer as a career" kwamba ukiwa na follower wengi unaeza watumia kujiingizia kipato kwa kuwauzia bidhaa kutoka kwa Kampuni mbali mbali. Ile connection uliyonayo naukaribu"fake" wako na wao unaweza kuwafanya followers kuamini kuwa wanakujua nje-ndani na hivyo kujenga "mahusiano" na wewe via support. Inafikia mahali watu wananunua bidhaa/huduma ili tu waku-support na kuwa karibu nawe. Easy money.



2-Upweke wa Watu wa Ughaibuni; Mtu alie nyumbani anaona anawafuatiliaji wa kipindi au account yake akionyesha kusaidia watu wenye matatizo kiuchumi/maradhi au maish akwa ujumla(unakumbuka how Shogongo alivyoanzaga na gazeti lake la Ujumaa?). Sasa watu elfu kadhaa wamejiunga kwenye Acc, anapiga mahesabu kwamba ikiwa kila mmoja anatoa £3 which is very small amount and anybody wa Ughaibuni can afford,  hakika nalipwa mshahara wa Laki kadhaa kwa mwezi. 


Kwasabau katika hali halisi YouTube halipi watu kiasi hicho, ukiona watu wanasema YouTube inawalipa na wamekuwa mamilionea, ni wazi kuwa wana direct sponsorship and as you buy what they sell you(from the sponsorship) the sponsor get what they paid for kwa client wao, a YouTube channel you subscribed to.


Sio tu kwenye Kipato kutokana na content creation, siku hizi watu wamekuwa wepesi  kuomba senti hasa kutoka kwa wabongo wa Ughaibuni, kila wakipatwa na Gonjwa, Bill ya matibabu, wakifiwa mbio online. Hawa wabongo wa zamani(wamejilipua hehehehe) ambao sasa wanaishi maisha comfortable wanasumbuliwa na upweke, au midlife crisis wanataka kujisikia vema na kuwa karibu na nyumbani kila kuwa wamechangia, si ujajua homesick na hawawezi kurudi nyumbani? Huwa wepesi sana kujitolea kwasabu wanajua ugumu wa Maisha kwa baadhi ya watu Tanzania, wanaamini wakijitolea angalau wanakuwa wamesaidia wenzao kama Sadaka maana  mchango wao wa £100(tSh 300k*) is nothing. 



Nini kifanyike?

Utamaduni na Mila; kurudi nyuma na kujitahidi kujenga mahusiano mazuri na watu wanaotuzunguuka kwenye jamii, kabla ya internet wazazi wetu(waliozaliwa 1950s/60s) walifanya nini? walichangishana wenyewe kwa wenyewe kwenye familia na koo zao, majirani, mtaani, kazini, Kanisani/Msikitini, shuleni n,k. 


Politically yanatakiwa kufanyika Mengi, tukianzia na Mfumo mzima wa Elimu, Ajira, Tax na Afya ili watu wawawe na  Elimu, vipato vya uhakika, kuwa na huduma bora za afya na Bima ya Afya bure kwa kila mwananchi ambae hana ajira au ana kipato cha chini.


Kwasababu tu watu wa kwenye internet wanafanya haina maana kuwa hata wewe ufanye, wabongo tuna Mifumo yetu Asilia kwenye kila jamii(depends na Mkoa/Kabila), sio unakaa sana online to the point  that you forget who you are,  your values, principles and culture. Stop Americanise ya self.


Hitimisho;
Ukute I look at this on a poverty mindset au tuseme eye, maana I guarantee you  nina Material nyingi tu za kutengeneza pesa, sema nini sina that confidence to take a step further and asking people for money so we can all be abundant and live our best soft life.😉


Bbai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao