Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?
Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.
Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuangalia machoni, unaona aibu kisha unageuka upande mwingine unamuambia "nipe muda nifikirie" au "subiri nitakupa jibu"....anaanza kukubembeleza umkubali hapo hapo ili roho yake itulie....unang'aka...anakuomba radhi. Anauliza sasa lini utampa jibu...unamwambia labda wiki Ijayo...jamaa anaona ni mbali ila ndio inabidi aheshimu. Anakuaga na kukuuliza kama unataka akusindikize? Gentleman wa Kiswahili(as in culture not life style).
Mnaachana, anakupa tabasamu mwanana. Sasa presha inaanza ya kutoa jibu...unawaza mambo kibao ya sasa, shule, unoko wa wazazi na maisha yenu ya baadae....unajiuliza vipi kama hana kazi na tukapaya HIV? na ukashika mimba, je ataweza kunitunza mimi na mtoto wetu?
Baada ya kufika nyumbani unahisi baba na mama yako wanajua yaliyoujaza Moyo na akili yako, unajitahidi ku-act normal kumbe unakosea na wanakushtukia....lakini wanajua Binti yao anakua na anavutia "waharibifu" na hivyo kesho yake wanaongeza Ulinzi, hakuna kwenda kwa Mangi(Dukani) peke yako, baada ya siku kadhaa unasahau kuwa uliahidi limjamaa jibu lake, kama unamkubali awe mpenzi wako ama la! Miezi inapita ukimuomba Mungu akuepushe usije kutana nae. Picha ya jamaa inaishia hapo.
Siku unatoka zako sehemu sehemu, mara unakutana nae tena, kwasababu ulisahau/dharau ahadi uliyoitoa unakuwa huna la kusema/mjibu na kiukweli huna mpango wa kuwa na mpenzi, unaanza kujieleza kwanini ulimuacha solemba....anasikitika halafu bado anaomba jibu lake. Hapo unatamani ardhi ipasuke uingie, asikuone tena.
Halafu kuna wale wajanja ila wavivu, walijikuta Wamarekani wa Afrika eti walikuwa wanakutongoza kupitia Radio one sterioooooooo kipindi cha chombeza chombeza, unapatiwa dedication song hehehehe basi unajiskia special balaa japo huna mpango nae. !
Hii safari ya kutongozwa na watu(wanaume) mbali mbali, kukataa, kutaka kukubali kwasababu unamdondokea lakini kama vile haupo tayari, maana kuna jamaa mwingine bora zaidi kuliko yeye pale kwanini upoteze maisha yako ya ujana kwa kuwa na mpenzi halafu uolewe halafu uzae kabla hata hujaishi maisha yako kama mwanamke, halafu pia wazazi hawatokuelewa na utawatia aibu ikitokea umeshika mimba kabla ya ndoa na vilevile hujui shughuli zake wala familia yake...too much, si bora ubaki single hyuu! ilikuwa ndefu na yenye usumbufu sana.
Hivi umewahi kuogopa kuwa na favorite child? au pengine you pray that wanao wasije kukushutumu kuwa unampendelea mmoja wao zaidi kuliko wao? Au ni pre-Menopause imeanza?š
Bbai.
Comments